Ushauri: Mama mkwe kaniambia nimpe mwanae talaka

Ndio nimezaa nae mtoto mmoja na nimefunga ndoa ya kidini!
Mna Muda Gani umemrudisha Kwao? Je utaratibu wa Kumrudisha kwao uliwashirikisha washenga? au Wazee waliosimamia ndoa yako? au Ulijiamlia tu na mihasira yako kufanya hivyo??
 
Mkuu toa tu hiyo talaka mapenzi yameshaisha hapo
 
Mkuu ndoa ni Changamoto,wewe ndie unayejua hli ikoje...kaa chini na ujitathmini,nani tatizo katika ndoa yenu,huenda ukawa ni wewe au yeye...ukweli munaujua wewe na mkeo na mungu wenu...kama umemchoka na tabia Zake zimeshakua sugu basi MUACHE...kama bado moyo wako unamhitaji basi ongea na mkeo nyinyi wawili tu,mueleze unavyojisikia,unavyokèrwa,na usivyovipenda..kama hataki kubadilika akueleze anatakaje ili amani iwepo

Kua makini sana,sisi baadhi ya wanawake tunatabia ya kujaribu nguvu ya mwanaume,tukikuona unayumba yumba hujiamini tunakupindua na mamlaka ya uongozi tunayachukua[emoji23][emoji23]!!kama ni ndoa ya kiislamu mwisho talaka 3,mtandike nayo moja halafu uone moto wake,atakuja kwako anatambaa...Labda kama unamtegemea yeye kiuchumi,ila kama wewe ndie mzalishaji mkuu wa kipato cha familia na yeye ni Housewife basi atarudi..

Chunguza,Jitathmini,Fanya maamuzi ya kiume
 
Hivi ujiulize unataka nini

Umemrudisha kwao na wanataka talaka sasa unataka nini haswaaa... ungempenda na kuweza kutatua matatizo husingemrudisha kwao.. haya mpe talaka wameshaona njia ingine ya wao kuchukua na mkeo kuendelea na maisha..

Unachekesha kweli kweli kabisaaaaaa
 
Mama mkwe wangu ameniambia nimpe mwanae talaka yake!Kiufupi nilishaleta uzi wa swaala langu hapo nyuma.

Mke wangu alikua ananifitisha na familia yake hadi ikawa pande mbili za wazazi hazielewani.

Kwa ubusara nikaona nirudishe kwao akapumzike kidogo. Chakushangaza leo mama mkwe ananipigia simu nakuniambia kwa hasira na maneno makali sana nimpe mwanae talaka yake.

"Nikamuuliza mama unadai talaka wewe au mwanao?" Akanijibu ndio nimeshakuambia!

Na huyo mwanae akadakia ndio nataka talaka yangu! Sasa nikabaki njia panda ni kipi kiaendelea hadi saivi na kipi nikifanye?

NAOMBENI USHAURI
Jiwe likishajitokeza haliwezi tena kuharibu jembe. Mke akishakuwekea wazi hakutaki, kuendelea kumkumbatia ni kutafuta majuto ya kujitakia. Sishabikii talaka na haaa kama mna watoto lakini sometimes talaka ndio the only best option. Shukuru amekwambia waziwazi. Wengine hufanya vitimbwoi vingine mpaka vya kuhatarisha maisha kabisa. Ukichelewa kupata ujumbe lolote baya laweza kukutokea.
 
Mkuu kwanini usiongee na babaye or ulioa mtoto wa single mama
 
Sasa siumpe una ngoja nini? Si kataka mwenyewe? MPE baba wala usirudi nyuma. Wanataka uwabembeleze na wakupande kichwani sasa wanakutingishia kibiriti. Waonyeshe kuwa kimejaa full. Yani ningekua Mimi ni dk hiyo hiyo na nafata taratibu zote. Mwanamke anayedai talaka ni mzuri maana hawezi kudai chochote katika Mali zako.
Yaan straight no kuchelewesha. Huko mbeleni kikinuka ndiohuwa wanaanza kujikomba ohhh unajua alikuwa shetani, ohhh ilikuwa ni mama
 
Mkuu ndoa ni Changamoto,wewe ndie unayejua hli ikoje...kaa chini na ujitathmini,nani tatizo katika ndoa yenu,huenda ukawa ni wewe au yeye...ukweli munaujua wewe na mkeo na mungu wenu...kama umemchoka na tabia Zake zimeshakua sugu basi MUACHE...kama bado moyo wako unamhitaji basi ongea na mkeo nyinyi wawili tu,mueleze unavyojisikia,unavyokèrwa,na usivyovipenda..kama hataki kubadilika akueleze anatakaje ili amani iwepo

Kua makini sana,sisi baadhi ya wanawake tunatabia ya kujaribu nguvu ya mwanaume,tukikuona unayumba yumba hujiamini tunakupindua na mamlaka ya uongozi tunayachukua[emoji23][emoji23]!!kama ni ndoa ya kiislamu mwisho talaka 3,mtandike nayo moja halafu uone moto wake,atakuja kwako anatambaa...Labda kama unamtegemea yeye kiuchumi,ila kama wewe ndie mzalishaji mkuu wa kipato cha familia na yeye ni Housewife basi atarudi..

Chunguza,Jitathmini,Fanya maamuzi ya kiume
Dada zamda nilichokiona tangu awali nikwamba wazazi wake wote wawili ndio wako nyuma ya mtoto wao na visa vngi amenifanyia hadi kufikia mimì kumpeleka kwao ni kwamba alikataa hadi kwenda kwetu likizo decmber mwakajana. Mama ya baba yake wamekua chanzo cha hili 100%
 
Kila kitu hapo kimekwisha, huna sababu ya kung'ang'aniza ndoa hapo vinginevyo itakugharimu sana baadae, kubali yaishe uanze maisha mapya maana hujui Mungu anakuepusha na nini na anataka kukufanyia nini ili maadai zako waone.
 
Bora umpe talaka mapema mkuu alafu kuoa/ kuolewa/ kuishi unyumba sio kila mtu kaumbiwa hivyo, bora ya nusu shari kuliko shari kamili/ bora kinga kuliko tiba muwahi kabla ajakuwahi maana akikuwahi utaishia kujinyonga/ kujiua/ maradhi yazinaa/ maradhi yamoyo kama sio uchizi kabisa!!
 
Hivi ujiulize unataka nini

Umemrudisha kwao na wanataka talaka sasa unataka nini haswaaa... ungempenda na kuweza kutatua matatizo husingemrudisha kwao.. haya mpe talaka wameshaona njia ingine ya wao kuchukua na mkeo kuendelea na maisha..

Unachekesha kweli kweli kabisaaaaaa
Ndugu kurudi kwao haikua kwenye tatizo hili alidaianaumwa nikamwambia twende kwetu dcmbr likizo akagoma yeye kwenda kwetu akahitaj kwenda kwao. Tukafanya mawasiliano ya wazazi wote kwetu na kwao tukakubaliana kua kwakua anahitaji kwenda kwazo zaid ya kwetu aruhusiwe aende. Nikampeleka hadi kwao mimi nikarudi zangu kwetu na baadae nikarudi kazni kwangu.
 
Mama mkwe wangu ameniambia nimpe mwanae talaka yake!Kiufupi nilishaleta uzi wa swaala langu hapo nyuma.

Mke wangu alikua ananifitisha na familia yake hadi ikawa pande mbili za wazazi hazielewani.

Kwa ubusara nikaona nirudishe kwao akapumzike kidogo. Chakushangaza leo mama mkwe ananipigia simu nakuniambia kwa hasira na maneno makali sana nimpe mwanae talaka yake.

"Nikamuuliza mama unadai talaka wewe au mwanao?" Akanijibu ndio nimeshakuambia!

Na huyo mwanae akadakia ndio nataka talaka yangu! Sasa nikabaki njia panda ni kipi kiaendelea hadi saivi na kipi nikifanye?

NAOMBENI USHAURI
Delete huyo haraka lazima wanae mtu tayari, itakusumbua sana uking'ang'ania watakuendesha kitumwa
 
Hapo njia panda unasubiri nini hadi muda huu huja-take action kama mwanaume?ni dharau kubwa sana mama mkwe kuanza kukupigia wewe simu na kudai talaka ya mwanae,mimi ningemjibu njoo wewe uichukue nikiona anachelewa nampa bodaboda awapelekee.na kosa ulilifanya mwenyewe toka mwanzo,unapiga piga simu ukweni kwa week mara mbili ooh nilikuwa nawasalimia mara blah blah blah ukawapa nafasi ya kukuzoea vibaya hasa mama mkwe,me ukweni napiga simu kwa mwaka mara moja labda nisikie kuna tatizo maradhi etc.inatakiwa mama mkwe akuogope yaani anakaa hajui kama wewe kichwani ni mzima au hapana hii scene kwamba akupigie wewe simu ingetakiwa aiogope aione simu ya moto.
 
Umetishia kujamba haya yamekukuta.....!!!!!
Jipe muda huku ukiwa umewakalia kimya, wanaume wa siku hizi mioyo laiiiiiini masikini
 
Hapo njia panda unasubiri nini hadi muda huu huja-take action kama mwanaume?ni dharau kubwa sana mama mkwe kuanza kukupigia wewe simu na kudai talaka ya mwanae,mimi ningemjibu njoo wewe uichukue nikiona anachelewa nampa bodaboda awapelekee.na kosa ulilifanya mwenyewe toka mwanzo,unapiga piga simu ukweni kwa week mara mbili ooh nilikuwa nawasalimia mara blah blah blah ukawapa nafasi ya kukuzoea vibaya hasa mama mkwe,me ukweni napiga simu kwa mwaka mara moja labda nisikie kuna tatizo maradhi etc.inatakiwa mama mkwe akuogope yaani anakaa hajui kama wewe kichwani ni mzima au hapana hii scene kwamba akupigie wewe simu ingetakiwa aiogope aione simu ya moto.
Mwenyewe nilishangaa sana mama mkwe kuniambia eti nitafute utaratibu wa tutoa talaka nimpe mwanae. Nikamwambia mama wewe ndio unadai nikupe talaka au mwanao akajibu nimeshakuchoka mpe talaka yake! Nikamjibu sawa nikakata simu yake!
 
Mkuu ukisikia Mwanamke anatamka neno talaka zaidi ya x3 MPE, akahangaike na Dunia. Maana kinyume na hapo atakuletea ugonjwa wa #Dr.Robert Gallo
 
Ndugu kurudi kwao haikua kwenye tatizo hili alidaianaumwa nikamwambia twende kwetu dcmbr likizo akagoma yeye kwenda kwetu akahitaj kwenda kwao. Tukafanya mawasiliano ya wazazi wote kwetu na kwao tukakubaliana kua kwakua anahitaji kwenda kwazo zaid ya kwetu aruhusiwe aende. Nikampeleka hadi kwao mimi nikarudi zangu kwetu na baadae nikarudi kazni kwangu.
Pole ndugu
 
Back
Top Bottom