Baba mkwe anataka nimpe talaka mwanaye ili tugawe mali. Mama mkwe anaenda kwa waganga aniue ili mwanaye arithi mali zangu

Oct 5, 2019
36
33
Kiufupi nimeoa mwaka 2017 na tumejaaliwa mtoto mmoja, ila kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana nimekuwa katika hali ngumu na mke wangu katika ndoa, amekuwa hanisikii mimi kama mmewe kila kitu anaendeshwa na wazazi wake .

Sasa imefikia baba yake kumuambia adai talaka arudi nyumbani, nilipojua hiyo njama nikawahusisha wazee wa pande zote mbili ,ila kule kwao wakakataa kuhusika, siku sio chache mke wangu akanishitaki kwenye baraza la wazee kuwa anataka haki yake amechoka kuishi na mimi. Nikaitwa kwenye kikao cha wajumbe, akaulizwa aseme shida yake nini , akajibu kuwa anataka tugawe mali zote kila mtu ajue maisha yake, akaulizwa hizo mali mmechuma na mmeo au ulizikuta? Akajibu nimezikuta.

Akaulizwa ni mali gani mmechuma na mmeo tokea mmeoana? Akajibu hatukacha mali yoyote. Wajumbe wakamjibu kuwa kulingana na alikuta hizo mali zote basi hizo mali hazikuhusu.

Tokea hapo alibadili upepo akawa mtulivu hata ile hali ikaisha, sasa kumbe ile hali ilibadilishwa upepo na kuelekezwa kwa ushirikina, ushahidi niliupata kutoka kwa mtu wa karibu na mama mkwe wangu( mama wa mke wangu) kuwa mama mkwe wako anakuendea kwa waganga akuue mwanae arithi hizo mali.

Sasa kwa haya mafupi naombeni maoni na ushauri.

Nawasilisha!
 
Mpe anachotaka aende mali hutafutwa uhai hautafutwi ndugu. Umeoa mke masikini wa mawazo yeye na familia yake. Pole sana

Kuna aliyekuja na kesi kama hii hapa jukwaani. Alisema alipojua kuwa shida ni mali alimwambia mkewe abebe kila kitu. Yeye alianza moja.

Baada ya miaka mitano ndugu na jamaa walimuomba amuonee huruma yule mama kwani ameuza kila kitu na hali yake ni ngumu ilhali ana watoto wadogo.
 
pole sanaa...ndoa zinakuwa na changamoto pale ndugu waanzapo kuingiliaaaa...Nashisi huenda ata akikupikia chakula unakuwa na mashaka mashakaaa...

SALI sali ....Funga siku 7 kuomba Mungu aangaze familia yako na kuijalia maamuzi yenye hekima....
 
Duh! Sasa kama watu mlioana na kuunganishwa kuwa kitu 1 mpaka mnafikia hapo halafu bado unaomba ushauri? Labda nikuulize unaamini katika upendo? Na je, ushawahi kupendwa na kujisikia kabisa kwamba unapendwa katika maisha yako? Na wewe je, ushawahi kupenda? Inawezekana tatizo ni kubwa zaidi hasa upande wako!
 
Ushauri wangu kwako, hakikisha unamtafuta mwanasheria mzuri nenda kabadilishe majina ya mali zako zote zihamishie umiliki kwa dada yako au mdogo wako/au mama yako/baba awe ndiyo mmiliki wa hizo mali....

Kama imeshindikana nenda bank kakope hela nyingi halafu uweke mali zako zote bond halafu ufungue akaunti nyingine bank hizo hela utakazo zikopa uzihamishie huko kwa siri.... Hapo hata ikitokea ulazma wa kugawana mali.. Mwisho wa picha mali zitarudi bank......

Zipo njia nyingi sana ambazo haziumizi kichwa za kideal na vichwa nazi
 
Hapo hakuna ushauri zaidi ya kwamba piga chini huyo mwanamke,

Maandiko yanasema Mwanamke mpumbafu ataivunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe.


"KIFO"sio kitu cha kuchezea ata kidogo hakuna mbadala wa uhai mimi mtu akinitishia kuniua tu ni mistake lazima nimuanze yeye kwanza kabla hajanifikia na hiyo ndio destiny yangu.
 
Back
Top Bottom