Ushauri: Malasusa atimuliwe KKKT kutengwa pekee hakutoshi

Nadhani atapewa onyo tu, maana watachunguza nini kilijiri. Huwezi jua chini ya kapeti. Tusihukumu saaana
 
Sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU; out of 27 upo pekee yako; what would you do??

MUNGU hutetea sauti ya wengi of course baada ya kujiridhisha.

By the way sisi waumini hatujaona tatizo la ule waraka, kwanza ulichelewa mno.
Mungu anasikiliza hata mtu mmoja mwenye kweli yake, sio lazima asikilize sauti ya wengi katika hao 27 huyo mmoja anaweza kua sahihi mbele za Mungu na akasikilizwa.
 
KKKT ikichelewa kufanyia kazi ushauri huu itavuna mabua , tayari jamaa kaingiza mamluki ili kuvuruga kanisa
 
Ukicheka na nyani utavuna mabua , huyu hakutakiwa kuwepo mpaka muda huu , njama zote hizi anashiriki kuzipanga
 
Malasusa kafanya kosa gani la kumfanya atengwe? Ni makosa ya kawaida ambayo yanahitaji kutatuliwa kwa njia ya maongezi! Hili jambo lione limetokea kwa mwenzio, na usiombe likutokee! Mbona kuna maaskofu kibao wanatembea na wake za watu lakini hawatengwi? Kuna maaskofu kibao wanafanya maovu hata sshetani cha mtoto! Sembuse Malasusa? Kama kuna askofu anaona hana kosa lolote kwenye utumishi wake wa uaskofu basi ajitokeze na atangaze kumtenga Malasusa! Nayaongea haya si kwamba nina udugu na Malasusa la hasha, ni kwa mtazamo wangu tu kwa jinsi nilijuavyo kanisa la KKKT.
Kwani kanisa unalijuaje wewe! Pengine unaufahamu uongozi wa kanisa, uongozi wa dayosisi mbalimbali, majengo ya kanisa, miradi ya dayosisi mbalimbali, waumini wa dhehebu la Lutheran, n.k. Epuka sana "sweeping statements na generation ". Je, ukiambiwa uthibitishe hayo unayosema kuwa maaskofu wanafanya maovu (shetani ni cha mtoto) utathibitisha??). Naomba kama hujui ni bora uulize wanaojua mfumo na utawala wa kanisa la KKKT. Please avoid character assassination.
 
Tulionya mapema sana tukapuuzwa , haya sasa kiko wapi ?
 
Mtu yeyote anayesaliti msimamo wa wenzake kwenye kikundi chochote hata kama ni maskani ya kunywa kahawa hastahili kunyamaziwa ama kutengwa pekee , anatakiwa kutimuliwa ndani ya kikundi hicho

Pamoja na ukweli kwamba Mungu amewaasa wanadamu kuwa na moyo wa kusamehe , LAKINI HAKUNA MAANDIKO YOYOTE KWENYE BIBLIA YANAYOMUAGIZA MWANADAMU KUMSAMEHE SHETANI , ndani ya maandiko matakatifu kumeelezwa ukubwa wa dhambi ya usaliti , hakuna msamaha na laana hii inatembea mpaka kwenye kizazi cha 4 , huwakumba hata wasiohusika , Mungu aliweka adhabu hii makusudi ili kukomesha wanadamu wenye tabia hii.

Ukiacha msaliti ndani ya Kanisa ni sawa na kulisha kanisa usaliti wake

Mungu ibariki KKKT
Tulionya mapema sana
 
Tulionya kitambo mno!
 
ameharibu kabisa legacy yake.
Malasusa amepata huo uaskofu kwa kuchaguliwa, hivyo wale waliomchagua wana uwezo wa kumuondoa na kama atakataa kuondoka washirika watagomea kanisa lake kupata sadaka na mwenyewe ataondoka!!! Waumini wakigoma kutoa sadaka hapo Azania front , Malasusa ataondoka!
 
Mtu yeyote anayesaliti msimamo wa wenzake kwenye kikundi chochote hata kama ni maskani ya kunywa kahawa hastahili kunyamaziwa ama kutengwa pekee , anatakiwa kutimuliwa ndani ya kikundi hicho

Pamoja na ukweli kwamba Mungu amewaasa wanadamu kuwa na moyo wa kusamehe , LAKINI HAKUNA MAANDIKO YOYOTE KWENYE BIBLIA YANAYOMUAGIZA MWANADAMU KUMSAMEHE SHETANI , ndani ya maandiko matakatifu kumeelezwa ukubwa wa dhambi ya usaliti , hakuna msamaha na laana hii inatembea mpaka kwenye kizazi cha 4 , huwakumba hata wasiohusika , Mungu aliweka adhabu hii makusudi ili kukomesha wanadamu wenye tabia hii.

Ukiacha msaliti ndani ya Kanisa ni sawa na kulisha kanisa usaliti wake

Mungu ibariki KKKT
uliona mbali sana mkuu..
 
Hawa TEC wanaotukana watu kanisani hv ni maaskofu kweli au ni makateksta?
 
Back
Top Bottom