Ushauri kwa wanaotaka kuagiza magari japan

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Watanzania wengi hupendelea kuagiza magari yao Japan aidha moja kwa moja au kwa kutumia maajenti. Hivi karibuni Japan imekubwa na maafa ya matetemeko ya ardhi ambayo madhara yake yameifanya dunia nzima kutafakari kama matumizi ya nuklia ni sahihi katika hali kama ya Japan. ikumbukwe kuwa Japan ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea saana kwenye teknolojia lakini nuklia imewafanya wasiwe chochote na kubaki kuhangaika kuhakikisha madhara ya nuklia ile yanapungua.
Tukienda kwenye mjadala hasa wa mada, sehem ile iliyokumbwa na mafaruki yale kumetokea uharibifu wa magari saana na kwa vyovyote vile mengi miongoni mwao hayafai kwahiyo wanatakiwa wanunuzi ili yaondoke pale. Kwahiyo yoyote atakayetaka kununua magari inabidi kuwa muangalifu huenda ukauzia gari ambalo baada ya muda mfupi bei ya matengenezo ikafanana na bei ya gari.
Lakini pia Yen imekuwa na nguvu saana kuliko wakati wowote kutokana na speculation kuwa insurance firms zitarepatriate yen kwa ajili ya re-construction. Kwahiyo value ya yen against dollar imezidi kuyoyoma. Kwa wale wafanya biashara wa huko ambao walinunua magari kwa ajili ya kuyauza inamaana walinunua ghali mno kulinganisha na thamani ya pesa sasa hivi. Kwahiyo watakachofanya ni kuhakikisha wanrecover pesa zao kwa kuongeza bei za magari yao. Kwahiyo magari yatapanda bei kama hali hii itamudu kwa muda mrefu. Sasa kwenye hili cha kufanya ni kutafuta venues nyingine ambapo mtu unaweza kununua gari lako au bidhaa nyingine.
 
hapa ndio umuhimu wa nyungo sasa unapoonekana, itabidi tuwasiliane na Majimoto tuone bei ya nyungo sasa imefika kiasi gani!
Mkubwa Majimoto ukisoma thread hii hembu tupatie bei ya nyungo maana magari ndio hivyo tena.
 
Ushauri wako ni mzuri lakini bado pamoja na kiswangilish chako waeleze watu wajue uwanja mwingine ni upi.
 
Ushauri wako ni mzuri lakini bado pamoja na kiswangilish chako waeleze watu wajue uwanja mwingine ni upi.
UK is better, japo mengi ni manual kwa wale wasiopenda manual sasa shughuli!
 
Back
Top Bottom