Ushauri kwa wanaotaka kuagiza magari japan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa wanaotaka kuagiza magari japan

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, Mar 17, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi hupendelea kuagiza magari yao Japan aidha moja kwa moja au kwa kutumia maajenti. Hivi karibuni Japan imekubwa na maafa ya matetemeko ya ardhi ambayo madhara yake yameifanya dunia nzima kutafakari kama matumizi ya nuklia ni sahihi katika hali kama ya Japan. ikumbukwe kuwa Japan ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea saana kwenye teknolojia lakini nuklia imewafanya wasiwe chochote na kubaki kuhangaika kuhakikisha madhara ya nuklia ile yanapungua.
  Tukienda kwenye mjadala hasa wa mada, sehem ile iliyokumbwa na mafaruki yale kumetokea uharibifu wa magari saana na kwa vyovyote vile mengi miongoni mwao hayafai kwahiyo wanatakiwa wanunuzi ili yaondoke pale. Kwahiyo yoyote atakayetaka kununua magari inabidi kuwa muangalifu huenda ukauzia gari ambalo baada ya muda mfupi bei ya matengenezo ikafanana na bei ya gari.
  Lakini pia Yen imekuwa na nguvu saana kuliko wakati wowote kutokana na speculation kuwa insurance firms zitarepatriate yen kwa ajili ya re-construction. Kwahiyo value ya yen against dollar imezidi kuyoyoma. Kwa wale wafanya biashara wa huko ambao walinunua magari kwa ajili ya kuyauza inamaana walinunua ghali mno kulinganisha na thamani ya pesa sasa hivi. Kwahiyo watakachofanya ni kuhakikisha wanrecover pesa zao kwa kuongeza bei za magari yao. Kwahiyo magari yatapanda bei kama hali hii itamudu kwa muda mrefu. Sasa kwenye hili cha kufanya ni kutafuta venues nyingine ambapo mtu unaweza kununua gari lako au bidhaa nyingine.
   
 2. M

  Matarese JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hapa ndio umuhimu wa nyungo sasa unapoonekana, itabidi tuwasiliane na Majimoto tuone bei ya nyungo sasa imefika kiasi gani!
  Mkubwa Majimoto ukisoma thread hii hembu tupatie bei ya nyungo maana magari ndio hivyo tena.
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ahsante mkuu!
   
 4. I

  Ipole JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ushauri wako ni mzuri lakini bado pamoja na kiswangilish chako waeleze watu wajue uwanja mwingine ni upi.
   
 5. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  UK is better, japo mengi ni manual kwa wale wasiopenda manual sasa shughuli!
   
 6. b

  ben van mike JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 471
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 33
  asante kwa ushauri mkuu , ni kweli UK is better ..........kwa sasa
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,362
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  agiza china bei poa saaana ::tongue:
   
 8. locust60

  locust60 Senior Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  China? bidhaa mpya toka china hazifai unasema used sipati picha
   
Loading...