Serikali ije na utaratibu mpya wa ununuzi wa magari yaliyotumika

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
381
763
Siyo kuwa Mtanzania anapenda kununua gari lililotumika la hasha. Kinachopelekea Mtanzania kununua gari lililotumika na hali ya kipato chake. Kwa Mtanzania kama mimi siwezi kununua gari jipya la toleo la toyota kwa gharama ya Tshs.120,000,000 au Toyota Landcruiser hard top kwa Tshs. 160,000,000 n.k.

Nimeshudia magari ya aina ya mahindra kutoka India ni magari ambayo hayadumu kabisa hata ukiyanunua yakiwa mapya na ni afadhali ununue gari lililotumika ya Japan kuliko Mahindra. Ninaishauri Serikali kuwa ili kuruhusu wananchi kununua magari yaliyotumika basi iweke ukomo wa mwaka.

Leo nimesoma gazeti moja la Kenya na Serikali ya Kenya imetoa taarifa kuwa kuanzia 1 Januari, 2024 magari yatakayoingizwa nchini Kenya yawe ya kuanzia 1 Januari, 2017. tunatakiwa tuige mfano huo wa Kenya. bado watanzania hatuna uwezo wa kuagiza au kununua magari mapya.
 
Uwezo wa mwananchi kununua hata IST tu 2017 ni tatizo, hapo sana sana serikali itakuwa inachukua pesa kubwa kwenye pesa za uchakavu Ila hilo suala la mfanyakazi wa middle class kununua gari la 2017 kwenda juu ni mtihani.
 
Siyo kuwa Mtanzania anapenda kununua gari lililotumika la hasha. Kinachopelekea Mtanzania kununua gari lililotumika na hali ya kipato chake. Kwa Mtanzania kama mimi siwezi kununua gari jipya la toleo la toyota kwa gharama ya Tshs.120,000,000 au toyota landcruiser hard top kwa Tshs.160,000,000 n.k. Nimeshudia magari ya aina ya mahindra kutoka India ni magari ambayo hayadumu kabisa hata ukiyanunua yakiwa mapya na ni afadhali ununue gari lililotumika ya Japan kuliko Mahindra. Ninaishauri Serikali kuwa ili kuruhusu wananchi kununua magari yaliyotumika basi iweke ukomo wa mwaka. Leo nimesoma gazeti moja la Kenya na Serikali ya Kenya imetoa taarifa kuwa kuanzia 1 Januari, 2024 magari yatakayoingizwa nchini Kenya yawe ya kuanzia 1 Januari, 2017. tunatakiwa tuige mfano huo wa Kenya. bado watanzania hatuna uwezo wa kuagiza au kununua magari mapya.
H
 
Mambo ya kupangiana magari ya kununua me sijapenda. Kimsingi, mtu ananunua gari ambayo roho yake inapenda. Mfano, naweza nunua Rav4 ya mwaka 1992 na mambo yakawa fresh tu sababu ndio gari napenda kutumia.

Swala la uchakavu ni maigizo tu, ni vipi kama gari ni ya mwaka 2000 ila ilikuwa imepaki tu yard ikipewa service ndogo ndogo bila kutumika.

Concept ya uchakavu imekaa kisiasa sana maana gari zinazoingia nyingi zipo kwenye ubora. Magari chakavu yanajulikana hata mtoto wa miaka 10 anaweza kukuonyesha.

We unasema gari chakavu na gari ni pisikali kabisa ina m'ng'ao wa kiwandani kabisa.
 
Kodi ya uchakavu ni mpango wa wizi wa serikali kumvuna mwananchi.
Fikiria ukishalipa hiyo kodi ndio gari linakuwa jipya? Au ndio gari linaacha kuchafua mazingira?

Nchi zenye akili, zikiona haziwezi kuwapa wananchi wake kitu fulani basi huamua kuruhuhsu utaratibu rafiki wa wananchi kukitafuta hicho kitu sehemu nyingine bila kuwaongezea gharama za ziada

Sasa hili linchi letu, limejaa ubabaishaji na kupenda kuvuna lisipopanda
 
Back
Top Bottom