Ushauri kwa vikosi vya uokoaji: Majina ya mamlaka muhimu kama TMA yasitumike

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Kumekuwa na mazoea ya kutumia majina ya mamlaka muhimu kama TMA, GST, polisi nk katika mazoezi ya utayari kama ndiyo vyanzo vya taarifa za kufanya mazoezi hayo. Kwa ujumla habari hizi huleta taharuki kwa wananchi na kuwasababisha waache kufanya shughuli zao.

Athari ya habari hizi kwa wananchi ni kutokuaminiwa kwa taarifa zinazotolewa na mamlaka hizi hata kama ni kweli! Hivi sasa TMA inatoa taarifa za kuwepo kwa El Nino katika baadhi ya mikoa hapa nchini. Na kwa kuwa hali ya El Nino inakuja taratibu watu wanaweza kuanza kutokuiamini taarifa hii kwa kuwa wanaweza kudhani ni mzaha wa mazoezi ya utayari.

Kwa hiyo ni vema kuepuka kutumia majina ya mamlaka na badala yake itafutwe mbinu mbadala ya kuhalalisha mazoezi ya utayari!
 
Utetezi wa Waziri Jennister Mhagama hautoshi!
 
Back
Top Bottom