isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,250
Habari đź‘‹
Naomba siku ya leo nitoe ushauri na mapendekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kuhusu wizara hii ya teknolojia, mawasiliano na habari.
Sifahamu Dr. Faustine Ndugulile kipi kimemtatiza katika hii wizara. Sina shaka na utendaji wake lakini nadhani kutokana na yeye kuegemea zaidi katika afya maybe uelewa zaidi katika teknolojia, mawasiliano na habari sio katika wigo mpana au perspective tofauti.
Pili naona naibu waziri na katibu mkuu katika wizara hii hawashauri vyema au kufanya mapitio yenye kuhusu teknolojia, mawasiliano na habari.
USHAURI | kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan:
1. Apitie wizara husika na kufanya mabadiliko katika nafasi za katibu mkuu wa wizara na naibu waziri kuweza kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji.
2. Wizara husika usukwe upya kwa kujumuisha masuala ya teknolojia na mawasiliano kwa wigo mpana, ibebe dhima ya teknolojia, mawasiliano na habari kwa uzito tofauti.
3. Wizara husika ikaimiwe na naibu waziri wawili na makatibu wakuu wawili. Mmoja akihusika zaidi katika teknolojia combined na mwingine akijizatiti katika mawasiliano na habari.
MAPENDEKEZO | Kutokana na kupitia watu tofauti katika wingi huu wa watu million 60+
Naomba Rais. Mama Samia Suluhu apitie majina ya wafuatao kuweza kuchukua nafasi za Naibu Mawaziri na Katibu Wakuu.
1. Maxence Melo 2. Salim Kikeke 3. Benjamin Fernandes 4. Charles Hillary 5. Millard Ayo na 6. Mimi ili kusudi tuweze kumsaidia Dr. Faustine Ndugulile na taifa katika nyanja hizi.
Naona naweza kufanya kazi katika mtiririko na kasi ya teknolojia, mawasiliano na habari na nipo tayari kwa uapisho Jumanne hii Dodoma.
Asante.