Pongezi nyingi kwa jitihada unazofanya za kuongoza nchi yetu na kurudisha hali nzuri ya mahusiano na uongozi wa kidemokrasia na kisheria. Najua una mambo mengi ila nitaandika kwa kifupi kabisa ushauri wangu walau kwa jambo moja tu kwa leo.
Ni kuhusu shirika la ndege ATCL. Ukweli unaojulikana na wachache kuwa hali ya ATCL sio nzuri. Shirika hili linaendeshwa kwa kulazimisha sana, shirika halina bussiness plan nzuri, wataalamu wazuri; watu wenye ujuzi, weledi na nia thabiti ya kufanya biashara. Wengi waliopo kwenye nafasi za uongozi au utendaji ATCL ni watu wa kuletwa au kwa maneno mengine ni wale waliopewa nafasi hizo kama zawadi. Hili jambo ni hatari mno kwa maendeleo ya shirika hili.
Ushauri: Mheshimiwa rais ni vigumu mno kuweza kuendesha ATCL ikawa na mafanikio wakati bado ATCL ni shirika linalomilikiwa na serikali 100%. Hili likiendelea, tutegemee hasara kila mwaka, na itafika mahali itakuwa kero kwako na utaishia kumbana CAG katika report zake kama ilivyokuwa awamu iliyopita, ukweli ulifichwa! Biashara ya ndege ni moja kati ya biashara ngumu sana duniani! Ninashauri ubinafsishe ATCL mara moja. Serikali imiliki share tu kwa ubia na mashirika na watu binafsi. Fanya ubia na wenzetu kutoka nchi zilizoendelea na zenye mafanikio katika sector ya usafiri wa anga.
Mashirika ya ndege kutoka nchi zilizoendelea kama British Airways, American Airlines, KLM, Lufthansa, South African Airways, etc yote ni ubia wa serikali na secta binafsi. Tena mara nyingi share za serikali ni chini ya 40%.
Ushauri wangu mheshimiwa rais, fanya kwa ATCL kama unavyotaka kufanya kwa Bandari, binafsisha ATCL Ili kuongeza ufanisi. Biashara ya ndege ni ngumu sana na inahitaji umakini na weledi mkubwa sana wa kiuongozi, management, utafutaji wa masoko, ujuzi mkuwa wa biashara, na uchukuaji wa maamuzi sahihi. Huwezi kuwapata watu hawa bila kushirikiana na watu kutoka nchi zilizofanikiwa katika secta ya usafiri wa anga. Kama tunavyohitaji ujuzi kutoka nje ya nchi katika kujenga madaraja makubwa, majumba makubwa, reli, bandari, mifumo ya mawasiliano, n.k., hivyo hivyo tunahitaji ujuzi kutoka nje ili tufanikiwe ATCL.
Pia mheshimiwa fikiria kubinafsisha mashirika mengine kama TTCL, TRC na mengineyo ili nayo yasife kibudu. Kwa wenzetu walioendelea kama Marekani, Ulaya, n.k. serikali imeacha uendeshaji wa biashara ufanywe kwa sehemu kubwa sana, >90% na secta binafsi. Hapa kwetu bado serikali inang'ang'ania kufanya biashara kwa hasara kwasababu ni rahisi kuendelea kubaki madarakani hata kama makosa yale yale yanajirudia kila mwaka.
TUSIPO BINAFSISHA ATCL AU KUSHIRIKIANA NA WALIOFANIKIWA KWENYE AVIATION INDUSTRY NINA UHAKIKA BAADA YA MIAKA MICHACHE VIWANJA VYETU VYA NDEGE VITAGEUKA KUWA PARKING LOTS ZA NDEGE MBOVU ZA ATCL NA NCHI ITAPATA HASARA YA MATRILIONI.
Ni matumaini yangu kuwa utafanyia kazi ushauri huu kwa ajili ya kuboresha utendaji na matokeo ya mashirika yetu ya Umma.
Asante.