Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,396
- 829,697
- Thread starter
- #61
Hata mimi piaKweli uhalisia upo lakini wengi maisha tumeanzia huko mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi piaKweli uhalisia upo lakini wengi maisha tumeanzia huko mkuu.
Sometimes hata hilo godoro huna unaenda kuomba mabox kwa wauza fridge unatandika siku zinaenda. "Adui hana alama"
Ukiwa mwema hakuna shida kabisaSometimes hata hilo godoro huna unaenda kuomba mabox kwa wauza fridge unatandika siku zinaenda. "Adui hana alama"
Hivyo vyombo vya ulinzi vinatakiwa kuwa much active kumjua adui wa kweli.
SawasawaHivyo vyombo vya ulinzi vinatakiwa kuwa much active kumjua adui wa kweli.
Shukrani kwa Mungu kwa watoto wako kurudi salama,na kumaliza mhula wa shule salama, wako watoto wengine hawakuweza waliuugua,walifariki nk
Najua kweli mzazi upo bize kutafuta ridhiki ya kila siku,lakini wape muda watoto wako kipindi Cha likizo,kaa nao,angalia Kama Kuna mabadiliko yoyote ya kiroho au kimwili. Wape muda punguza ubize.
Jamani wazazi tuwe na tabia ya kusikiliza watoto wetu,wana mengi wamepitia wakiwa mbali na wewe,hebu wape muda wa kuwasikiliza basi,wanatamani kusema Ila hawana pa kusemea wape mudaa..
inawezekana umengua kitu,ambacho sio kizuri,usiwakalipie,usifoke ovyooo,hata Ni kosa ongea kwa utulivu,Jifunze kutuliza hasira yako,mfano unakuta binti yako au kijana ameeanza mahusiano ya kimapenzi,so wewe unatakiwa umwambie madhara ya kufanya sex kabla ya wakati,ataelewa zaidi kuliko kumpiga...ongea na kwa upole.

Kweli watoto walikuwa shule Sasa wamerudi,basi sio vibaya wakishiriki kazi za nyumbani ikiwa ni kupika,kuosha vyombo,kupanga sebule, vyumba vyao kuwa safi,kuosha vyombo nk wasimuachie dada wa kazi, kumbuka huu muda ndio mzuri wao kujifunza,usiwaache .
Kweli likizo watakuwa na muda wa kuangalia sanaa tv,Ila kuwa Makini na carton,move nk wanazoangalia,zingine hazina maadili mazuri,jilizishe kwa kile wanachoaangalia.
kipindi hiki Kama muda upo wapeleke wasalimie ndugu,Kuna familia watoto hawajui kabisa ndugu zao,hii hatari sababu hao watoto ujue wanakua na watakuwa na tabia ya kutowatembelea ndugu Wala kuwajali.
Kama mzazi lazima mtoto anaporudi uangalie vizuri bag ambalo amerudi nalo,je amerudi na vitu vyake,? Wengine wanaanza tabia ya wizi au kuazimana anarudi na vitu sio vyake,Ila ktk kupekua bag Kuna vitu unaweza Kukutana navyo pia,Kuna watoto ambao wameaanza mahusiano utawakuta na vidonge vya majira, condoms nk so check up muhimu sanaa.
Ibada muhimu sanaa , hakikisha unaomba nao,pia kila mmoja mwambie akuandikie kwenye karatasi ombi ambalo anataka Mungu amtendeee nk omba nao wafundishe neno la Mungu nk wekeza vitu vyema kwa watoto wako...
wakati wa magufuli ndio tuliishi sana kwa hofu,ya kutekwa,kupewa kesi ukikosoa, na mauchafu kibaoFuraha inatoka wapi kama unaandika mambo ya uhalifu kuongezeka kwa kasi!???
Hii si ni dalili ya kuanza kuishi kwa hofu
Mbona unajikanganya kwenye maelezo mkuu
dah,basi inaonyesha washawapiga wengi kwa style iyoUTAPELI UMERUDI KWA KASI
Kwa wakazi wa Dar es Salaam, chukueni tafadhari.
Hii imenitokea leo, kwenye mataa ya mtaa wa Lindi na Msimbazi. Nilifanya kosa pale (nilitakiwa kunyoosha moja kwa moja kutoka Kkoo kuja Karume, mie nikapinda kulia kuyafuata mataa ya Uhuru na Msimbazi). Nilipofika mataa ya Uhuru, mara wakatokea vijana wawili watanashati, wakiwa na pikipiki. Wakazuia gari kwa mbele; wakatoa vitambulisho, mmoja ni mfanyakazi wa UDART na mwingine ni askari wa Usalama barabarani. Kisha wakasema umefanya kosa kwa mujibu wa sheria za UDART. Hivyo unapaswa kwenda kizuizini kwa siku 14 kisha utalipa faini tsh 850,000 ndipo utakuwa huru. Haya ongoza Yadi. Kijana mmoja akapanda garini, yule mwingine akawa anatufuata nyuma na pikipiki. Nikatumia muda huo kuomba msamaha na kuomba kupunguziwa faini ili tumalizane yaishe. Lakini afisa yule alikuwa mkali, King'ang'anizi. Mara akapiga boss wake, akiagiza nipelekwe haraka Yadi, nikaomba kuongea na boss. Sasa ikabidi nipaki maeneo ya jirani na uwanja wa Karume (TFF). Katika maongezi yetu boss yule alitaka nilipe fine ya tsh laki 6 badala ya 860,000/=
Lakini wakati hayo yanafanyika kichwani nilikuwa nawaza "Hawa jamaa wanaweza kuwa matapeli". Sasa nikazima gari. Nikawaomba hawa jamaa wawili nishuke nikatafute pesa kwa ndugu yangu ambaye anafanya biashara hapo jirani ( kwenye kituo cha daladala cha karume). Jamaa wakakubali. Tukaongozana; nilipomkuta dada nikamsimulia tukio hili kwa kifupi, kisha nikamwambia aende pale kituo cha polisi (jirani) aulize uhalali hii operation ya maafisa wa UDART. Wale jamaa walipoona dada anaenda kituoni wakanifuata, wakasema niwape hela yoyote niliyonayo ili mambo yaishe.. tukiwa bado tunabishana mara akatoka askari mmoja namimi nikaitwa kituoni. Wale jamaa walipoona hayo wakakimbia kwa kasi. Kumbe walikuwa Matapeli tu, sio UDART wala sio askari, ni Matapeli.
Basi nikawashukuru wale askari kisha nikaondoka.
Mtaarifu na mwingine, asije akaibiwa kizembe.
Copy & Paste as received
️NENO LA LEO,2021
️
Alhamisi,July 01
Tunaitwa kutenda
haki na huruma
️Kutoka 23:1-5
TAFAKURI;
Tunatakiwa kutenda haki na huruma, na wala si kutenda mambo ya ukatili na udhalimu hata dhidi ya wanyama, mifugo wasio na hatia.
Somo la leo linatukataza kutenda uovu wa kupotoa hukumu.Tunatakiwa kutenda haki wala tusifanye upendeleo.Tukiona ng'ombe au punda wa mtu amepotea au amepata shida tumsaidie na tumrudishe salama nyumbani kwake. _
Jamani Wapendwa wana wa Mungu tusaidiane, tusifanyiane mambo ya hiana na udhalimu bali tutende haki na huruma sisi kwa sisi, lakini pia kwa viumbe wasio na hatia.
Bwana Yesu Kristo, asante kwa kunihurumia mimi mwenye dhambi.Unisaidie mimi na msomaji Huyu tutende haki na huruma kwa jirani zetu katika jina lako takatifu
AMINA