Ushauri kwa IGP: Ukitaka uwazi katika uwajibikaji wa Polisi ruhusu wawe wanarekodiwa na Raia hata ndani ya kituo cha polisi

Hata video zikiwepo hakuna lolote litakalofanyika. Kama kuna video za ngono za wanasiasa na bado wana nafasi zao mnafikiri video za polisi zitawafanya wawajibike?
 
Nikikuta polisi anapigana na jambazi, namsaidia jambazi tumuue polisi. Halafu namshauri jambazi aache uharifu. Akifanya uhalifu namuitia mwizi.
 
IGP Ukitamani uwajibikaji na uwazi kwa jeshi lako we tangaza kwa vyombo vya habari kuruhuri matumizi ta teknolojia yaan Raia waruhusiwe kurekodi matukio ya polisi akiwa katika kazi zake hata ndani ya kituo cha polisi

Na iwe ni sheria na pia marufuku kumkataza raia kurekodi matukio hata ndani ya kituo cha polisi.

hakika utapata jeshi ambalo litakuwa na nidhamu ya hali ya juu!

matukio ya polisi kunyanyasa raia hasa kama amepishana nae lugha kidogo ni mengi sana!
polisi wanabambika kesi watu na kuna walio jela kwa sababu ya maamuzi ya hawa polisi wetu

kuna matukio hasa ya kuuana polisi kwa polisi kutokana na unyanyasaji wa wenyewe kwa wenyewe!

IGP ukitaman uwajibikaji wewe tangaza uwazi tu
Hakuna sababu ya kurecord, zifungwe CCTV camera mpaka mahabusu na maeneo yote ya polisi
 
Ni hatari kurekodi maeneo nyeti bro
Maeneo nyeti yapi, vituo vya polisi au?
Kuna unyeti gani wakati hapa nilipo naweza kuangalia hadi ikulu kwa msaada wa teknolojia?
Hakuna maeneo nyeti. Haya ni maeneo ya umma na tunapaswa kuchukua video mambo yakiwa hovyo
 
Kupiga ni iwapo umekataa kutoa ushirikiano, sio hiyo ya kupiga ili kumtia mtu hofu akiri kosa ambalo hajatenda, ama kujiwekea mazingira ya kupata rushwa. Kwasasa polisi wetu wanachojua ni kupiga tu pindi wanapokamata mtuhumiwa jambo ambalo si sahihi.
Na polis huwa hawawezi tu kuanza kupiga bila kumletea ukinzani
 
Back
Top Bottom