Mababa,
Huu ni ushauri mdogo kwenu maana naamini mmejaa hekima na elimu ya kutosha kufahamu kinachoendelea. Ombi langu kwenu ni moja tu!
Msitoke kutetea hiyo document iliyotolewa na Vatican bali simamieni mafundisho ya Kanisa tuliyopokea ama kwa maandishi au kwa mapokeo kama anavyosema mtume Paulo.
Ni vizuri kuongea kuliko kukaa kimya huku waamini wakiwa kwenye mtanziko wa yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandao.
Kwa waamini wenzangu, kama huwezi kuipata na kuisoma mwenyewe hiyo document usitoe maoni yoyote kwa kupitia taarifa pekee za vyombo vya habari.
Hatari zaidi ni kuwasikiliza watu ambao hawalijui Kanisa, hawajui mafundisho ya Kanisa na wengine wamejaa chuki hata kabla ya taarifa kama hizi.
Uhai wa Kanisa upo mikononi mwa Kristo na yeye mwenyewe alishatuhakikishia Kanisa halitoshindwa. Let's watch and pray [emoji120]