Ushauri: Kuliko ndege kuendelea kukaa Airport, bora zikodishwe

Hadi sasa shirika letu la ndege ATCL lina zaidi ya ndege 10, baadhi ya ndege hizo hazina kazi yeyote ya kufanya kulingana na mahitaji ya sasa zaidi ya kupaki uwanja wa ndege JKNIA.

Inavyoonekana shirika halikuwa limejipanga kupokea ndege nyingi kiasi hiki kwa wakati mmoja, na kwa sasa shirika haliko tayari wala halina uwezo wa ku 'operate' ndege zaidi ya kumi, ninavyoona uwezo wake ni wa kuendesha shirika lenye ndege moja au mbili tu tena za ndani.

Nashauri, wakati ATCL ikijipanga ki mikakati ya kuliendesha shirika kwa ufanisi, ikiwemo kupata management bora, kupata kibali cha kuruka nje, IATA, kufanya utafiti wa 'routes' zenye faida, ku train marubani wake, air hostess, kujenga karakana ya kufanyia service nk, bora baadhi ya ndege tuzikodishe hadi hapo tutakapokuwa tayari kuliko kuendelea kukaa uwanjani zikipigwa jua, mvua na vumbi, na kuzichosha kwa safari fupi ya Mwanza.

Nashauri, Dreamliner Boeing 787, ikodishwe, Airbus zote mbili zikodishwe na Bombardier moja ikodishwe, shirika libaki na angalau bombardier mbili kwa ajili ya safari za ndani.

ATCL hawatakuwa wa kwanza kukodisha ndege zao, mashirika makubwa kama Ethiopia Airlines, South African Airlines hukodi na kukodisha ndege kulingana na mahitaji ya soko la wakati huo.
Wacha tufanye maonyesho ya ndani kwanza tuongeze mapato

In God we Trust
 
Hata gari ikipaki muda mrefu injini hu knock sembuse ndege.

Note that, Ndege inahesabiwa masaa tangu itengenezwe yakiisha na muda wake wa kuwa hewani unakwisha.
Wacha kudanganya wewe, gari ipi uliyoiona ije "knock" kwa kuegeshwa muda mrefu?

Hivi unaelewa hata maana ya gari ku "knock"?
 
Wewe kweli punguani, utapata "routes" na kibali bila kuwa na ndege?

Halafu kwa fikra zenu za kimaeikini mnaona ndege kumi nyiiingi sana, kuna wenzenu wanaagiza ngapi...

Emirates airline ordered 70 Airbus jets at a value of $21.5 billion (Dh78.97bn) and reached an agreement with the plane manufacturer to receive 14 more A380s, whose production will stop by 2021.

Airbus to scrap A380 production by 2021 as Emirates orders 70 smaller jets
FaizaFoxy Emirates hakuna ccm kuna management watu wamesoma kazi hizo biashara ya anga haitaki propaganda hapa kwetu ccm waliofanya mchakato wa manunuzi ya ndege hizi ukiwachunguza utakuta wana PHD za propaganda na ndege wapi na wapi
 
Sisi hatuna hela za mafuta kama waarabu. Na wala hatuna uzoefu na hiyo biashara. Badala yake sisi tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo ,uvuvi na ufugaji na vijana wengi wasio na maarifa wala mitaji ya kufanya kilimo na ufugaji wa kisasa

Hiyo hela tungeielekeza huko. Huko tusingekosa wateja kama tunavyokosa wateja kwenye ndege mpaka zinapaki muda mrefu
 
Sasa unataka kusema tusifanye kwa kuwa CCM ndiyo inaongoza Tanzania?

Na huko ATCL wafanyakazi wote ni CCM?

Wewe ambae si CCM nnauhakika hata ki toy cha ndege huna nyumbani.
 
Sisi hatuna hela za mafuta kama waarabu. Na wala hatuna uzoefu na hiyo biashara. Badala yake sisi tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo ,uvuvi na ufugaji na vijana wengi wasio na maarifa wala mitaji ya kufanya kilimo na ufugaji wa kisasa

Hiyo hela tungeielekeza huko. Huko tusingekosa wateja kama tunavyokosa wateja kwenye ndege mpaka zinapaki muda mrefu
Kalime na kavue ulikatazwa? Wacha sisi tuwapatie ajira watoto wa wakulima na wavuvi waliopiga kitabu na kuwa marubani.
 
Kwani route ya India haijaanza? Nauliza wapanda madege tu wengine mabasi ni raha zetu na bajaji.
 
Kalime na kavue ulikatazwa? Wacha sisi tuwapatie ajira watoto wa wakulima na wavuvi waliopiga kitabu na kuwa marubani.

Ni ajira ngapi zimetengenezwa? Ni ajira ngapi zingetengenezwa kwenye option ya kuwekeza kwa vijana?

Biashara ya ndege ushindan wake ni balaa. Muda utasema yote. Nategemea tutakuwa watu wa ku-inject hela zaidi na zaidi kwenye hiyo biashara
 
Kalime na kavue ulikatazwa? Wacha sisi tuwapatie ajira watoto wa wakulima na wavuvi waliopiga kitabu na kuwa marubani.

Mtoto wa maskini wa kweli bongo hii uwezo wa kusomea urubani hana. Huyo mtoto amejaa tele kule kijijini hana elimu maarifa ya kilimo cha kisasa na wala hana mtaji
 
Nchi ya Ethiopia Wana shirika kubwa la Ndege kuliko yote Africa,Wana SGR,Wana Miundombinu mizuri sana ya Barabara Flyover, Reli (Metro)ukilinganisha na sisi na vitu tunavyotaka kuvifanya... Lakini mbona Wananchi wao tena vijana wanaikimbia Nchi? Wapo radhi wafungiwe kwenye Containers Ili wavuke kwenda South Africa. Maendeleo ni watu! sio vitu. PERIOD.
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom