Ushauri: Kuliko ndege kuendelea kukaa Airport, bora zikodishwe

Hadi sasa shirika letu la ndege ATCL lina zaidi ya ndege 10, baadhi ya ndege hizo hazina kazi yeyote ya kufanya kulingana na mahitaji ya sasa zaidi ya kupaki uwanja wa ndege JKNIA.

Inavyoonekana shirika halikuwa limejipanga kupokea ndege nyingi kiasi hiki kwa wakati mmoja, na kwa sasa shirika haliko tayari wala halina uwezo wa ku 'operate' ndege zaidi ya kumi, ninavyoona uwezo wake ni wa kuendesha shirika lenye ndege moja au mbili tu tena za ndani.

Nashauri, wakati ATCL ikijipanga ki mikakati ya kuliendesha shirika kwa ufanisi, ikiwemo kupata management bora, kupata kibali cha kuruka nje, IATA, kufanya utafiti wa 'routes' zenye faida, ku train marubani wake, air hostess, kujenga karakana ya kufanyia service nk, bora baadhi ya ndege tuzikodishe hadi hapo tutakapokuwa tayari kuliko kuendelea kukaa uwanjani zikipigwa jua, mvua na vumbi, na kuzichosha kwa safari fupi ya Mwanza.

Nashauri, Dreamliner Boeing 787, ikodishwe, Airbus zote mbili zikodishwe na Bombardier moja ikodishwe, shirika libaki na angalau bombardier mbili kwa ajili ya safari za ndani.

ATCL hawatakuwa wa kwanza kukodisha ndege zao, mashirika makubwa kama Ethiopia Airlines, South African Airlines hukodi na kukodisha ndege kulingana na mahitaji ya soko la wakati huo.
Kwani Da Mange na Lissu na Umoja was Ulaya wanasemaje?
 
Miezi si mingi? Hasara yake unaijua, ndege siyo daladala kuwa unaweza ukaipaki uwani kusave mafuta ya siku hiyo, kadri ndege inavyopaki ndiyo hasara inavyoongezeka.
Walioziagiza hizi ndege wanayafahamu masuala ya sekta ya anga kuliko mimi na wewe.
 
We jamaa unajifanya unaongea Kwa fact huna lolote muongo tu,Kama ni biashara delicate mbona kuna nchi zina operate na zingine zinafanana na Tanzania,unataka kusema zimepaki Kwa kuwa kina uratibu unafanyika ili zianze ku operate Kwa ufanisi,uongo ambao hata mtoto wa chekechea hawezi ukubali,shrika la ndege si lilikuwepo na kuna ndege zilikuwepo ina maana tayari Lina experience sasa we unakuja na uongo wako wa kitoto kujifanya eti biashara ya ndege ni delicate sijui huwezi land ndege usiku blah blah nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hizi ndege tumenunua kwa cash hatujazikodisha wala kuziazima. Ni mali yetu hizo gharama za kuwa zimekaa bila ya kutumika, sijui mnazitoa wapi. Hizi ndege sio mkopo, usiwadanganye watu kwamba eti kuna gharama zinapokuwa zipo grounded. Tuliza mzuka waache watu wafanye kazi zao.
 
Ndiyo maana tuliwaambia hii biashara siyo ya kukimbilia kununua kama unanunua fuso la kusafirisha viazi mviringo kutoka Mbeya, bila ya mipango yeyote, huwezi kununua ndege karibu kumi ndipo uanze kufikiria kutafuta kibali na routes.
Route zipo, tatizo wabongo tunapenda kurahisisha kila jambo. Huwezi kwenda China au Japan pasipo kupanga muda na viwanja vya kule, huwezi ukaenda Australia pasipo kuweka sawa masuala ya wewe utatua lini na saa ngapi kule, kuna mijadala lazima iwe inaendelea kati ya ATCL na mashirika ya kule. Yapo mambo mengi ndio maana tunasema tuwape muda hawa waliopewa dhamana.

Hizi siasa zetu za huyu CCM na huyu CHADEMA tusiziingize kwenye masuala ya kitaalam, yabaki huku huku kwenye issue za kina pole pole na lissu sio kwenye utaalam.
 
Mkuu hizi ndege tumenunua kwa cash hatujazikodisha wala kuziazima. Ni mali yetu hizo gharama za kuwa zimekaa bila ya kutumika, sijui mnazitoa wapi. Hizi ndege sio mkopo, usiwadanganye watu kwamba eti kuna gharama zinapokuwa zipo grounded. Tuliza mzuka waache watu wafanye kazi zao.
Nchi zisizojua kufanya biashara,ndio Yale Yale ya mkulima uchwara,haya mahindi nimelima mwenyewe hta nikiuza debe shilingi 200 sina hasara,yaani Hana running costs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Route zipo, tatizo wabongo tunapenda kurahisisha kila jambo. Huwezi kwenda China au Japan pasipo kupanga muda na viwanja vya kule, huwezi ukaenda Australia pasipo kuweka sawa masuala ya wewe utatua lini na saa ngapi kule, kuna mijadala lazima iwe inaendelea kati ya ATCL na mashirika ya kule. Yapo mambo mengi ndio maana tunasema tuwape muda hawa waliopewa dhamana.

Hizi siasa zetu za huyu CCM na huyu CHADEMA tusiziingize kwenye masuala ya kitaalam, yabaki huku huku kwenye issue za kina pole pole na lissu sio kwenye utaalam.
Hayo yote leo ndio mnaanza kupanga?
 
Tulihitaji Management nzuri yenye weledi kabla ya kukimbilia kununua ndege, naambiwa inaweza kufika June kabla hazijaanza safari za nje, hatuoni ndege kukaa miezi sita ni hasara, dreamliner inaweza kufikisha mwaka bila kupata route ya nje.
ATCL ni sawa na mwanafunzi wa darasa la saba english medium kapewa mtihani wa form six chemistry..
Sidhani kama walikuwa tayari kupokea idadi kubwa ya ndege kwa haraka.
Director atakuwa katika tension sana kuhakikisha route zinakaa sawa,kitu kinachoitwa "Competition in Aviation Sector" kisikie tu huko DW,VOA,CNN,BBC..usiombe ukione kwenye kampuni ya kwenu(Nyumbani).
Pia Serikali ingeaanza kutoa mafunzo maalum mapema kwa watu watakofanya kazi katika mradi SGR ili isije kuwa na makelele.
 
Hayo yote leo ndio mnaanza kupanga?
Hakuna perfection kwenye maisha ya mwanadamu. Ni rahis kukosoa lakini ukipewa nafasi ukaboronga kuliko unayemkosoa leo.

Donald Trump alipanga kuwa akiingia madarakani atajenga ukuta, mpaka leo anahangaishana na bunge kuhusu fedha ya ujenzi.

Hakuna kitu kinachofanywa na mwanadamu kikawa na ukamilifu wa asilimia mia moja, upungufu wa hapa na pale ndio sifa ya mwanadamu.
 
Hata suala la korosho tuliwashauri hivi hivi mkasema tuwaachie wenye dhamana angalia walivyo vurunda.
Mkuu huko kwenye korosho kuna watu wamelipwa mabilioni ya shilingi, tatizo lenu huo ushauri huwa unabeba sura ya kisiasa na wakati mwingine unakuwa ni ushauri wa kinafiki.
 
Mtoto wa maskini wa kweli bongo hii uwezo wa kusomea urubani hana. Huyo mtoto amejaa tele kule kijijini hana elimu maarifa ya kilimo cha kisasa na wala hana mtaji
Ajitahidi hata Magufuli ni mtoto wa mkulima lakini leo ni Rais wetu Tanzania. Samaki na kilimo kinalipa.
 
Ajitahidi hata Magufuli ni mtoto wa mkulima lakini leo ni Rais wetu Tanzania. Samaki na kilimo kinalipa.
Faiza unapoteza muda wako ndege wapewe Fastjet mchezo uishe achana na prorojo biashara ya anga sio kama biashara za guta kubeba matenga ya nyanya sokoni kama Tanesco imeshindwa kujiendesha inadaiwa madeni kibao mtaweza bishara ya anga?
 
Acha kasumba za kishamba. Kuna watu wana shule zao na wanafanya kazi ya maana tu. Tatizo la sisi wabongo ni kujichukulia poa tu, kujiona kama hatuwezi kufanya lolote!.
 
Back
Top Bottom