Ushauri kuhusu Biashara ya Kuuza Computer: Laptop/dektop used

Niliuliza watu wawili watatu wanasema pc ni za ku order nakusubiri mzigo ukifika ndio ukachague..
Mzigo ukichukuliwa na kuwekwa dukani price yake inakuwa kubwa kusafirisha huku Dar kodi kubwa unaweza kupata faida
Kwa Zanziber sio! Kule kuna vitu vya bei rahisi sema tu mambo ya ushuru ndiyo yanabana sana kama vile sio nchi ya muungano bana.
 
Kwa Zanziber sio! Kule kuna vitu vya bei rahisi sema tu mambo ya ushuru ndiyo yanabana sana kama vile sio nchi ya muungano bana
Mkuu unashauri tukafanye survey tu zanzibar? Na kuchukua mzigo huko.

Mfano Laptop 1 ushuru wake unaweza kuwa kiasi gani?
 
Shida wakulungwa hawawezi kupa channel wabongo sijui tukoje asee
Mbongo anahisi akikupa mchongo au akishea mchongo hapa anahisi labda watanzania mil60 wote watafanaya biashara kama yake,

Na ukiangalia yeye mwenyewe hana uwezo wa kusupply kwa demand yote iliyopo.. lakjni bado atakubania...!!
Natamani tungekuwa tunashirikaiana kama wahondi wasomali na wakenya ... kwenye biashara na uchumi
 
Nilishawahi kufanya tafiti nikabaini computer nyingi hasa laptops zinapatikana alibaba na huwa zinauzwa kutokana na specs za pc husika. Mfano unaweza kupata piece 100 za used laptops kwa dola 200 na au vinginevyo kwa piece moja bei ya jumla. Ukiwa na mtaji mzuri ni vyema kwenda dubai moja kwa moja kisha ukachukue mzigo uje nao. Maana wengi hufuata mizigo hasa used smartphones na kadhalika.
Tatizo pia linakuja kumpata supplier wa uhakika huko alibaba... namna yakuzisafirisha pia kupunguza gharama ...

maana niliwahi kuongea na mhudumu silent ocean nilimuuliza akaniambia hawasafirishi vifaa vya electronic kama laptop !
 
Habari wakuu.

Ni wapi zinapatikana Computer used nzuri kwa bei ya jumla?

Nitapata kwa Tshs. Ngapi kwa pc 1 kutokana na specifications za computer husika? Yaani bei ya kila pc na specifications zake.

Kwa wanaofahamu ma Supplier wa China na Dubai watujuze pia.

Kwa mzigo wa kutoka nje gharama za usafirishaji kwa Meli /Ndege zikoje?

Asante.
View attachment 1761981

Mzee, mimi nilipo huku zinapatikana used nyingi sana kwa bei tofauti tofauti. Tatizo ni gharama za huku zinaweza zisiwe rafiki kwa bongo, pili ni usafiri, tatu ni kodi za uingizaji bidhaa hizo lakini la mwisho ila siyo kwa umuhimu ni sheria za uagizaji.

Je, sheria inaruhusu uagizaji wa bidhaa tajwa, kwa urahisi gani? Maana navyoelewa siku hizi serikali zetu zinaziba mianya ya kuifanya Afrika kuwa jalala hivyo ni muhimu kuyafanyia utafiti hayo mambo kwanza
 
Uko wapi? Na gharama ziko vipi huko?
 
Back
Top Bottom