Ifahamu biashara ya spea za pikipiki (sehemu ya 6)

Ifahamu biashara ya spea za pikipiki (sehemu ya 6)

Jvei

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
42
Reaction score
67
Je, naweza kuanza biashara ya spea za pikipiki na bajaji kwa kufunga mzigo kutoka China moja kwa moja?

Jibu ni ndio. Unaweza kuanza biashara hii kwa kwenda China kufunga mzigo Kisha kuja kuuza.
Hata hivyo ni muhimu sana kabla ya kufunga safari kwenda China kujiridhisha na kufahamu mambo kadhaa.

Mambo yakufahamu kabla hujaenda kuchukua mzigo wa spea za pikipiki China

  • Kwanza Kabisa kama mfanyabiashara unapaswa kujua kama Kuna haja ya kwenda China.
Hii ni kwasabu asilimia zaidi ya 80 ya watengenezaji wa spea kutoka China na India wana wasambazi/Agents/Suppliers wao hapa hapa Tanzania. Hivyo unaweza jutumia garama kubwa kwenda kuchukua mzigo kumbe umeuacha nyumbani owa bei zile zile.
Mfano ni makapuni kama Bajaji, Yog, Ocelot, Sinory, Hard paudehe, YYW, CC, Tvs, n.k
Yote haya wana watu wao ambao hufanya B2B na wanaweza kukuuzia kwa bei nzuri kabisa Kisha wewe ukafungua duka la Jumla/rejareja.

  • Pili, Zifahamu kampuni zinazofanya vizuri sokoni. Kabla ya kwenda China unapaswa kuzifahamu kampuni zinazofanya vizuri kwenye soko lako. Hii itakusaidia sana kwenda kufunga mzigo ambao utakuwa unauzika sokoni. Hivyo hutalaza pesa!

  • Tatu, unapaswa kuwa na uzoefu wa ubora na njia nzuri ya kudhibiti ubora wa spea unazotaka kwenda kununua.
Hata China Kuna Vishoka na madalali, tena wapo makini sana. Unaweza kudhani unanunua kwa mzalishaji wa kampuni unayoijua kumbe sio. Hivyo utashangaa unachukua mzigo mkubwa lakini ukija ubora na nembo havifanani.

  • Nne, Unapaswa Kujua Bei ya Kiwandani dhidi ya Bei ya Suppliers waliopo Tanzania.
Kabla ya kukimbilia China fanya tafiti kwenye soko, zifahamu bei za spea kutoka kwa Suppliers na zile za manufacturers. Kama Kuna utofauti mkubwa ndipo uone haja ya kwenda kufunga mzigo nje.

  • Tano, Uzoefu wa soko.
Biashara sio location tu na mtaji, pia unahitaji watu wazoefu kukuongoza na kukupatia maarifa ya namna ya kufanya hadi pale nawewe utakapokuwa mzoefu (ndio maana sisi tupo).

  • Sita na mwisho kwa leo, Mtaji.
Ukitaka kwenda China lazima uwe na mtaji wa kutosha, kwani wana Mimimum order amabayo maranyingi kama huwezi kununua kwa ukubwa huo wanakuagiza urudi kwa agent wao. Hivyo unapofikiri kwenda China kufunga mzigo, fikiri pia kuwa si kazi rahisi itakuhitaji kuwa na mtaji wa kutosha.

Je, Kwa mfanya biashara wa spea za pikipiki Kuna faida yoyote ya kwenda China kuchukua Mzigo?

⚙Faida zipo nyingi sana, ukipata uzoefu wa soko na mtaji wa kutosha ni vizuri kwenda kuchukulia mzigo kiwandani.
Hata hivyo wafanyabiashara wengi hapa ndani wenye mitaji mpaka milioni 150 nazaidi hawaendi China. Bali hufanya Bulk stock kwa Suppliers, ambapo hununua Carton Nyingi za bidhaa wakati mwingine hata kwa pre order na hii hufanya wauziwe bei sawa na ile ya kiwandani.


  • Faida za kwenda China (ikiwa una uwezo) Ni pamoja na:

1. Bei nafuu zaidi – ukienda mwenyewe unaweza kupata bei za jumla (factory price) ambazo ni chini kuliko bei unazopewa na mawakala.


2. Ubora (Quality Control) – unaona bidhaa kwa macho, unaelewana na kiwanda moja kwa moja ili kuepuka kupata bidhaa feki.


3. Mkopo wa mzigo (Credit) – baadhi ya viwanda/agents wakikuamini wanaweza kukupa mizigo halafu ukalipa baadae.


4. Uaminifu – unajenga mahusiano na suppliers, ambayo ni muhimu sana kwenye spare parts.


5. Kufahamu aina mpya za bidhaa – unakutana na bidhaa ambazo bado hazijaingia Tanzania.


  • Hasara / Changamoto za kwenda China

1. Gharama kubwa – Tiketi, malazi, chakula, usafiri, kutembelea viwanda; gharama zinaweza kufika TZS 3m – 6m au zaidi.


2. Ujuzi wa lugha – Wachina wengi hawaongei Kiingereza, lazima uwe na agent.


3. Uhitaji wa mtaji mkubwa – Kupata bidhaa nzuri kwa bei ya kiwanda mara nyingi unahitaji kununua carton nyingi au container ndogo.


4. Hatari ya kudanganywa – Ukienda bila agent mzuri, unaweza kuuziwa bidhaa duni.
 
Back
Top Bottom