Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara hiyo ni nzuri, ila inategemea na eneo uliopo, ila usisahau kila biashara inachangamoto zake. Kwa mfano biashara hiyo ya kuchezesha video games.

Jambo la kwanza la kufkiria ni je eneo uliopo linaruhusu kuanzisha biashara hiyo. maana kuna baadhi ya maeneo wazazi hawapendelei kabisa kuwepo mabanda ya michezo hiyo, wao huamini inapotosha watoto wao.

Jambo la pili, uwe na muda wa kutosha wa kuweza kusimamia biashara hiyo maana ina hitaji si chini ya masaa 12 iwe nafanya kazi kwa siku.

Yapo mambo mengi, kama uzoefu wa kuitumia hizo ps, umeme, vifaa kama CD's, pad n.k
 
Habari wana JF,

Natumaini nyie ni wazima wa afya.,mimi ni kijana wa miaka 19,nimepata mtaji wa milion mbili kutoka kwa mama yangu,ninahitaji play station 2 kwa ajili ya kufanyia biashara kwani nataka kufungua sehemu ya watoto ya kuchezea games na frem ninayo, nipo moshi soweto na naomba kusaidiwa mwenye details zozote kuhusu mahali pa kuzipata na kwa bei nafuu anisaidie.

Nkaribisha ushauri pia namna ya kuifanya ili niweze kufaidika na hiyo biashara kwani naamini kuwa hapa ndipo pa kupata mawazo mazuri yatakayoweza kuniongoza vizuri, naomba kama utakuwa huna la kunisaidia basi we pita tu kama hujaona kuliko kunikashifu.

Napenda kuwasilisha mada na Asanteni sana wana JF.
 
Swali la msingi kwanza. Je, kuna wateja wa kutosha?

Baada ya hapo tutapambanua zaidi namna ya kuendesha biashara.
 
Killy25,

Kama wewe ndiye uliyeandika hii post basi nakupongeza sana. Kichwa chako kimetulia, ni nadra sana kijana wa umri wako kuandika lugha iliyonyooka na kwa ufasaha namna hii! Siku hizi hata kijana aliyemaliza shahada ya kwanza ukimwambia ajieleze ni kazi kwelikweli! Hakika wazazi wako wana malezi mema.

Kila la heri katika biashara zako. Tunarudi kwenye mada, hizo ps2 ni obviously unahitaji used, jaribu kupita kwenye maduka ya used electronics hapo Arusha, otherwise kama una mtu Dar aende kkoo akazunguke madukani kukuchekia. Wazo lingine ingia FB, kuna pages nyingi za deals, ukipost request yako watu wenye nazo wacomment na price zao, hapo utapata kwa bei ya ushindani, japo bado utahitaji mtu wa kuzikagua kama wauzaji wako nje ya Arusha (Mara nyingi ni Dar), leo peke yake mimi nimeona watu watatu wanauza PSII, wote wanauza chini ya 130K tena wanakupa na offer ya games kadhaa! Kila la heri.
 
Killy25,

Fremu unayo yako au kodi inatoka kwenye izo mil 2? location pia muhimu mfano huku Dar biashara iyo inalipa sana uswahilini sasa huko moshi inabidi uwe na uhakika na wateja alafu tumia flash disk kucheza game CD zinasumbua.
 
mkuu kwanini unashauri anunue PS 2 used na sio mpya?

Mimi nimeangalia budget yake, 2M kama ataamua kununua mpya sidhani kama budget itamtosha, ikizingatiwa kuwa atahitaji screens, gamepads imara, speakers, desks, chairs, na vitu vingine vidogovidogo anaweza kujikuta anaanza na mashine tatu tu. All in all, kama anaweza kuaford mpya its better.
 
Mimi nimeangalia budget yake, 2M kama ataamua kununua mpya sidhani kama budget itamtosha, ikizingatiwa kuwa atahitaji screens, gamepads imara, speakers, desks, chairs, na vitu vingine vidogovidogo anaweza kujikuta anaanza na mashine tatu tu. All in all, kama anaweza kuaford mpya its better.

Yes mkuu. Hongera. Nadhani una malengo mazuri. Ila kama alivyoshauri usipendelee CD.
 
Kama ukiweza unaweza ukaanzishia hyo biashara yako kibaraza cha nyumbani kwenu huku unakuza mtaji, au kama una ndugu yako ana duka au biashara yeyote mjini, omba nafasi hata pembeni ya biashara yake kupunguza gharama za kodi.
 
Jamani habari zenu wadau.

Najaribu kutoa maujanja juu ya biashara amabayo nimeifanya kwa almost miaka mitatu mfululizo na nimepata mafanikio makubwa. Biashara ya kuchezesha GAMES inahitaji mambo yafuatayo:
  1. Eneo lenye watu wengi hasa kando ya barabara au makazi ya watu wengi..
  2. Frame yenye upana wenye hewa kiasi cha kutosha
  3. Console (hasa za playstation 3 au xbox 360) kuanzia 3 na zaidi na Televisheni 3
  4. Unahitaji pia kuwa maeneo ambayo yana mlinzi wa duka hilo au kama frame iko karibu na nyumbani haina haja ya mlinzi unaweza kuhamisha console kila jioni hasa mida ya kufunga saa mbili usiku...
  5. Mtaji wake ni kama mil 2.5 cash..
  6. Generator la mchina (in case ya mgao kama sasa hivi)
Console za playstation 3 au xbox 360 ni bora zaidi kwani wachezeshaji wengi wanatumia hizi za kizamani za ps2 ambazo zishapitwa na wakati..na kama ukiongezea na TV zako zikawa ni flat screen inches 21 (hata kama ni za Used) itakuwa bora zaidi kwani itaboresha ubora zaidi wa picha, yaani high definition, pia unahitaji mtu wa kusimamia mradi huo we ukija jioni wakamilisha mahesabu tu.

Mradi huu unalipa vipi? kwa kawaida sie huchezesha kwa mtindo wa saa na nusu saa..kwa saa ni 1000 na nusu saa ni 500...na kufungua game center ni kuanzia saa 5 asubuhi wakati watoto wamekwenda shule siku za shule na mpaka saa mbili usiku..na weekend ni saa 3 mpaka saa mbili usiku...ukiwa mahali pazuri na unafikisha mpaka 25,000 kwa siku na inategemea una games nzuri kiasi gani inaongezeka hadi 30,000 (huu ni uzoefu wangu)

Ukija kutoa gharama ya umeme+ gharama ya ulinzi na mengine unabakia na aproximately 750,000 kwa mwezi...assuming umeme haukatiki katiki.

Console moja ya ps3 inapatikana kwa laki 3 mpaka 3 na nusu zanzibar...na xbox 360 zenyewe ni laki 3 ukiagiza kupitia mtandao wa EBAY na hiyo ni pamoja na gharama ya TRA..

CD za games best way ni kuziagiza nje (used kutoka EBAY ambazo ni gharama ndogo sana ya elf 20 mpaka 25) huku bongo ni elf 70 mpaka laki na nusu madukani...mwenye kutaka kujua zaidi ani PM
 
Games pendwa sana na wacheza games ni mpira hasa PRO EVOLUTION SOCCER na FIFA..gran turismo, moto GP, tekken 6, virtual fighter, need for speed (the run, au most wanted), mortal combat, God of war, WWE, call of duty na RESIDENT EVIL. Zote hizi ukiagiza EBAY ambazo ziko katika (GOOD CONDITION) ni bei sawa na bure.
 
Ukipenda kuchezesha games kupitia computer..ina gharama kiasi. Kwani PC lazima iwe duocore 2 na kupanda. Processor yake at least iwe 2.2 ghz na zaidi Ram at least iwe 2 GB na kuendelea.

Pia unahitaji graphics card ya ku support games amabazo inaweza kuwa Mvidia au Radeon ila iwe kuanzaia Ram ya 512mb na zaidi, ila much better ni 1GB ram, kisha unahitaji kifaa cha kuunganisha pad za playstation 1&2&3 kwenda usb au uchezeshe kwa kutumia USB pads ambazo bahati mbaya nyingi sana ni mchina na hazidumu. Games za kompyuta haziuzwi bali we wahitaji kuweka bundle la kutosha na kuingia kwenye mitandao ya TORRENTS na kudownload na kuinstall, basi kinachibakia ni kupiga fedha.
 
Sawa mkuu, somo zuri. Mi ni mmoja kati ya wanaotaka kufanya hii biashara, nitakucheki nikiwa tayari.
 
Mkuu lensi za deki za ps zinaharibika sana vipi huwa unafanyaje cz kutengeneza ni gharama sana.
 
Mambo yote safi sasa. Open for business.

Wenye kunibana ni wengi, niko kwenye nyumba yenye wapangaji, umeme natumia mdogo sana lakini wapangaji ndio hasara kwangu, maana wanatumia bila kujali na wanalazimisha wote tuchange sawa.

Kila baada ya wiki natoa 10,000, umeme unatumika zaidi ya 100,000 kwa mwezi, mita ya luku ni moja. mwenye nyumba anataka kodi tu, na biashara yangu bila umeme haifanyiki, nimesema sana lakini nimeambulia patupu.

Nisipoweka hamna mtu anaweka, wote wanataka nihame. Niko na separate mita ya kusoma matumizi yangu lakini haizingatiwi.

Nje ya biashara ni mafundi gari, kwani ni uswahilini na hawa mafundi hata niseme vipi, wanatengeneza magari nje ya biashara na siku nzima ni kelele za kugonga gonga na matusi kawaida yao kutukanana.

Sasa hebu niambieni, huu ni uungwana? Nimekuja kujua fikra za wengi hapa ni finyu sana na hawataki kuona mtu anaendelea kibiashara.
 
Back
Top Bottom