Kwa kuwa umeshaanza kutia shaka hiyo kazi haikufai, mwisho wa siku utafanya chini ya kiwango na mwajili wako atakasirika. Cha kufanya, USIACHE KAZI, kula sahani moja naye, huku ukifanya kazi kwa bidiii zote. Wakati unafanya kazi pia endelea kutafuta sehemu nyingine.
Kuna washauri wazuri wamekuambia usome sheria za kazi, fine, Lakini nahisi hazitakusaidia mbali na kukujenngea conflict na mwajili wako kisha atakutimua. Sheria za kazi zinafanya kazi lakini inabidi uwe makini kuzi apply. Kuwa mtaratibu, jenga mahusiano mazuri na mwajiri, apply unyenyekevu kisha chomekea hizo sheria na massaa ya kufanya kazi bila kuwa na jaziba wala hasira. Akiwa mkali kuwa mpole kabisa.
Kuna jamaa katoa maoni kuwa, inavyoonekana watanzania wengi hawajuwi haki zao kazini, na pia kuna wachangiaji kibao wamemmbeza jamaa mwenye master anayeamka usiku na kufanya kazi kwa masaa-mengi anayekuomba ukomae. Mi naona we komaa na kazi, hao wanaobeza kuwa watanzania hawajuwi haki zao kazini nawapa pole, kwa kuwa wana uhuru wa kutoa maoni, ni haki yao.
Ni sawa tu na shabikii anayeweza kusema "yule mchezaji si angekinga mguu tu na kufunga goli". UGUMU WA SEHEMU YA KAZI UNATOFAUTIANA. WEWE ULIYE nje ya nchi na kujidai unajuwa sheria za kazi na kuahidi ukija utasaidiwa watanzania wenzako, karibu, sana. Ni rahisi kukaa kwenye Keyboard na kuandika unavyojisikia. Hata hao waajiri wanazijuwa hizo sheria kazi wanachokifanya ni profit maximazation, UKIkomaa sana wanakupiga chini.
Ushauri wa pili ni kwamba, kuna kazi kibao ambazo wanafanya kazi muda mrefu zaidi ya hayo masaa yako, wala isikupe shida na kujiona kuwa hujuwi haki zako. Ukiwaza hivo utaumia sana na utaishia kupata msongo wa mawazo. Kwa kawaida ukiona kazi hailipi unapiga kazi kwa malengo, miezi kadhaa unakusanya mtaji unawekeza na wewe, kisha unapiga chini kazi huku ukitafuta nyingine wakati ukijuwa kuna sehemu inakupa mkate wa kila siku. Ukiacha kazi huku huna pa kukupatia mkate wakila siku UTAUMIA.
Jiulize kwa nini ROONEY wa man U anavuta 220pauni kwa wiki, huku WERBECK akivuta 50pauni kwa wiki, kwa nini yeye asidai akalingana na Rooney? Unataka kuniambia Welbeckck Hajuwi haki zake? Mkataba wako na makubaliano ndo msingi wa yote. Chapa mzigo siku ukipata panapokufaa ndo uondoke na si kuanza kulalamika lalamika. CHANGANYA NA ZA KWAKO PIA.