Ushauri; Kazi inaelekea kunishinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri; Kazi inaelekea kunishinda

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by gwankaja, Nov 1, 2011.

 1. gwankaja

  gwankaja JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 1,951
  Likes Received: 1,587
  Trophy Points: 280
  Wakuu mimi ni mgeni katika masuala ya ajira. Nimegraduate mwaka huu pale UDSM, na nimepata kazi wiki mbili zilizopita katika kampun moja pale Posta. Hawa jamaa wanataka nifike kazin saa moja asubuh na niondoke saa 12. Kulingana na eneo ninaloishi nalazimika kuamka saa 11 na kurudi nyumban saa 2 mpaka 3 usiku<MBEZI>. Pia wanafungua ofis mpaka jumapili, kinachosikitisha hakuna hata overtime pamoja kutoa mshahara kiduchu. Hivi wengine ndivyo mnavyofanya kazi hivi? Naomba ushaur katika hili.
   
 2. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  chezea mshahara husichezee kazi !

  hapo unapimwa.
  Kama unaona ni kero acha kazi ndipo utakapogundua kuwa hao wako sawa.
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hahaa haa!!! Hii kali mzee komaa nao tuu upate cha kuandika kwenye CV yako, chukulia kwamba bado upo shule. Mimi nipo kwenye hatua za awali za kujiajiri lakini still nafanya kazi za kuajiliwa kwasababu bado siko kwenye mazingira mazuri ya ku-take risk kwa 100% ila naamini maisha mazuri wanaishi watu walio jiajiri
   
 4. T

  Tabby JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,894
  Likes Received: 5,521
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu.

  Sikubaliani na mjumbe anayesema unapimwa. Unapimwa kufanya nini? Kutembea usiku, kazi bila mapumziko, malipo kiduchu ili kukupa msongo wa mawazo? Hiyo ni kampuni ya aina yake. Mimi nakushauri uendelee kutafuta kazi. Hapo watakuharibu ukiwa bado mchanga katika duru za ajira matokeo yake uchukie kazi na kuanza udanganyifu kama sehemu zingine za kazi tunazosikia. Hawajui kwamba wanavyokufanya wanakupunguzia uwezo wako wa kuzalisha na kujituma? Mimi sijaona. Tafuta kazi kwingine ila usiache kabla hujapata. Uwe makini na kazi. Usirumbane nao wala kukosa uadilifu. Mungu atakupa kazi nyingine kwa mwajiri atakethamini utu wako, elimu yako na uwepo wako katika ofisi yake.
   
 5. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkiambiwa wavivu mnasema mmetukanwa mnadharauliwa. hivi wewe kuamka saaa 11 asbui unaona ni tatizo? kurudi saa 2 usk unaona ni tatizo?? halafu hata kazi hujui bado ndo unajifunza, lakini unaanza na mtazamo hasi, ukirudi nyumbani saa kumi na nusu jioni unaweza kutuambia utakuwa unafanya nini???, au unaweza kutuambia kikubwa unachofanya weekend ambacho gharama yake ni wewe kukimbia kazi?.

  iache hiyo kazi, itakufundisha kazi
   
 6. g

  gambagumu JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 698
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  kaka tupo pamoja hata mimi niko katika situation kama yako ila mimi nshapiga two year..kwa sasa fanya ila kaka naamini kazi si utumwa..itabidi tutafute chaka zingine au tujaribu ujasiriamali..tuzidi kuomba Mungu.
   
 7. Kimolah

  Kimolah JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  una bahati wewe! Just fresh from school unaingia kwenye payroll, au kazi umepata kimagumashi na 'Kamlete'?! Kama ni private sector huna haja kulalamika if you can't dance the beat, ingekuwa serikalini ungeamka saa 1 job saa 3 na ungetoka saa 9 bila wasiwasi, I suggest kama ni 'kamlete' fanya mchakato upate serikalini (ambapo digits mwisho wa mwezi utajuuuta)
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Wafanyakazi wote ndio ratiba ipo hivyo au?
   
 9. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Vumulia ili upate experience then unaweza kuangalia sehemu zingine. Kuamka saa 11 na kurudi saa 2 au 3 ni jambo la kawaida kabisa. Ajira yangu ya kwanza ilikuwa kwenye one of the big four professional firms hapo Dar na hayo masaa unayoyataja yalikuwa ni kawaida kabisa. Tengeneza CV ndugu yangu then baadae utaona faida yake.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kazi std ni masaa 8 kwa siku x 5 days per week, hii hufanya kuwa jumla kuwa masaa 40 kwa wiki. Ukitakiwa ufanye overtime ni maximum 10 hours per week, hivo jumla maximum ni masaa 50 kwa wiki. Nje ya hapo ni unyonyaji na utumwa.
   
 11. O

  Optimistic Soul JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kawaida kabisa acha uvivu dogo, maisha ya kuajiriwa ndo ivo kama kuolewa vile lazima ulale uchi, kamua mzigo hadi jamaa wakome huku unaangalia nje, unachomoka kimtindo unaenda kupiga interview sehem then unarudi, mpaka kieleweke, usiache bila kupata kazi sehem nyingine unless una kitu cha kufanya, na kama ni wahindi ndo ufanye mishe mishe fasta watakufyonza hadi wakumalize. welcome to the world
   
 12. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,325
  Trophy Points: 280
  Acha kazi uone machungu ya kitaa.
   
 13. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mkuu kumbuka,
  Ukiwa na kazi ni rahisi kupata kazi,kama ilivyovigumu kupata kazi ukiwa huna kazi ! hivyo huyu jamaa akomae mpaka hapo baadaye kila kitu uanza na 0 ,wewe unatoka chuo unataka uanze kazi mbayo utakuwa unafuatwa nyumbani na gari la kampuni,pole sana
   
 14. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kwa upande mmjoja hii inaweza kutafsiriwa kama uvivu lakini kwetu sisi wenye utalaam wa kuongoza raslimaliwatu naona kama mwajiri anakiuka kanuni. Post ya kijana inaonesha hajaridhika na mchango anaoutoa na kile anachokipata. Kuanzia saa 1-12 jioni ni masaa kumi na moja kazini. Kulingana na sheria ya kazi mtu huyu anafanya ziada ya masaa 3kila siku. Na kwa vile anafanya siku saba za wiki anafanya kazi karibia masaa 77. Mwajiri anapaswa kuboresha maslahi na kulipa overtime.

  Bila shaka mwajiri huyu ni muhindi hao ndo wanapenda kunyonya watu. Namshauri kijana apime upepo. Anaweza kutumia dhana ya "opportunity cost" kufanya maamuzi.
   
 15. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  You are very smart..mkuu.
   
 16. m

  makuti Member

  #16
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wakubwa wote heshima zenu kwanza.
  Na poleni na majukumu ya kila siku .

  Nimesikitishwa na karibia asilimia 78% ya majibu na ushauri uliotolewa na wajumbe wachangiaji kwa upande mmoja, lakini pia kwa upande wa pili imenithibitishia mambo mawili :

  1. Watanzania wengi hawajui haki zao ktk AJIRA zao.
  2.Watanzania wengi wananyonywa na kuonewa ktk ajira zao.

  USHAURI KWA MHANGA WA TATIZO :
  1. Unachofanyiwa sio stahili yako na ujue unaonewa sana ,hivyo hata kama unaendelea na hiyo kazi ujue ya kwamba muda wa kazi una viwango na vingi vimefata International Standard , me nimefaya serikalini na sasa niko private lakini muda wa kazi ni masaa yasiyozidi 9 kwa siku , labda iku moja moja za emergences ambazo hata mwenyewe unaona inabidi tu .

  2. Nakushauri toa TZS 6000/= nunua kitabu cha EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT,2004 (ELRA,2004). Ni sheria ya kazi na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 , Na kimsingi waajiri wote wanalazimika kufuata sheria hii . Kwahiyo utapata muda wa kazi unaotakiwa kufanya,masaa ya ziada na siku za kazi ni ngapi kwa wiki na mambo mengine yote ya msingi kuhusu haki zako .

  3. Na ujue una haki ya kumshitaki Mwajiri wako kwa kukiuka sheria ya kazi hiyo niliyoitaja na hawezi kukufukuza kazi

  NB: MIMI SIO MWANASHERIA KWANI TUMEZOEA MAMBO YA SHERIA NA HAKI ZA MTU AJUE MWANASHERIA TU , UJUMBE WANGU KILA MFANYAKAZI ANATAKIWA KUJUA HAKI ZAKE ZA KISHERIA NA KIMSINGI .

  USIKU MWEMA KWA WOTE MLIOSOMA UJUMBE HUU .

  AHSANTENI NAOMBA KUWASILISHA.
   
 17. gwankaja

  gwankaja JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 1,951
  Likes Received: 1,587
  Trophy Points: 280
  nimekuelewa mkuu
   
 18. gwankaja

  gwankaja JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 1,951
  Likes Received: 1,587
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru, nna softcopy yake na nitaanza kupitia taratibu.
   
 19. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Tuseme ungepewa kazi utakayofanya bure ungeikubali kwa kuwa wewe ni "nyoya" wa kazi?

   
 20. M

  Mario Gomez JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 471
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Kaka jitahidi kuzoea kuamka mapema haya ndiyo maisha ya bongo kama vipi utafute nyumba karibu na city centre kitu ambacho sidhani kama utaweza kumudu gharama za kodi ya nyumba,Mwendo mdundo,kazi ni mbele kwa mbele.
   
Loading...