Wakubwa wote heshima zenu kwanza.
Na poleni na majukumu ya kila siku .
Nimesikitishwa na karibia asilimia 78% ya majibu na ushauri uliotolewa na wajumbe wachangiaji kwa upande mmoja, lakini pia kwa upande wa pili imenithibitishia mambo mawili :
1. Watanzania wengi hawajui haki zao ktk AJIRA zao.
2.Watanzania wengi wananyonywa na kuonewa ktk ajira zao.
USHAURI KWA MHANGA WA TATIZO :
1. Unachofanyiwa sio stahili yako na ujue unaonewa sana ,hivyo hata kama unaendelea na hiyo kazi ujue ya kwamba muda wa kazi una viwango na vingi vimefata International Standard , me nimefaya serikalini na sasa niko private lakini muda wa kazi ni masaa yasiyozidi 9 kwa siku , labda iku moja moja za emergences ambazo hata mwenyewe unaona inabidi tu .
2. Nakushauri toa TZS 6000/= nunua kitabu cha EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT,2004 (ELRA,2004). Ni sheria ya kazi na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 , Na kimsingi waajiri wote wanalazimika kufuata sheria hii . Kwahiyo utapata muda wa kazi unaotakiwa kufanya,masaa ya ziada na siku za kazi ni ngapi kwa wiki na mambo mengine yote ya msingi kuhusu haki zako .
3. Na ujue una haki ya kumshitaki Mwajiri wako kwa kukiuka sheria ya kazi hiyo niliyoitaja na hawezi kukufukuza kazi
NB: MIMI SIO MWANASHERIA KWANI TUMEZOEA MAMBO YA SHERIA NA HAKI ZA MTU AJUE MWANASHERIA TU , UJUMBE WANGU KILA MFANYAKAZI ANATAKIWA KUJUA HAKI ZAKE ZA KISHERIA NA KIMSINGI .
USIKU MWEMA KWA WOTE MLIOSOMA UJUMBE HUU .
AHSANTENI NAOMBA KUWASILISHA.