Ushauri katika utata huu

Ushauri katika utata huu

Sharing ni nzuri sana, ila kama wewe kwa binafsi yako utakosa amani kwa watu wanaokufahamu kujua ukubwa au tatizo lako, ni muhimu sana kuchunga privacy yako, vinginevyo itakusumbua psychologicaly na kukunyong'onyeza.

Tafuta wawili watatu uwashirikishe, naamini utapata pa kuanzia kama itakupendeza. nakupendekezea huyu mmojawapo [gfsonwin]. LoL

Asante kwa ushauri mkuu!!!!
 
Charminglady kwani mi wanijua? We kama vipi nimwagie PM ntakusaidia kwa kadri ntakavyoweza. Kama itakuridhia lakini. Kiroho safi
 
Kama unaogopa kuomba USHAURI kwasababu ya kujulikana na member's hapa jamvini,
mimi naona kama ni vizuri ungetumia jina la mtu mwingine either kwa kusema ni rafikiyo au mtu mwingine yoyote ila unaelezea ikiwa na maudhui yale yale ambayo yamekupata. Hiyo nadhani itakusaidia kupata mawazo ya watu wengi.
 
Kama unaogopa kuomba USHAURI kwasababu ya kujulikana na member's hapa jamvini,
mimi naona kama ni vizuri ungetumia jina la mtu mwingine either kwa kusema ni rafikiyo au mtu mwingine yoyote ila unaelezea ikiwa na maudhui yale yale ambayo yamekupata. Hiyo nadhani itakusaidia kupata mawazo ya watu wengi hivyo kuyachambua mawazo ya watu kwa kina.

Mkuu sio rahisi kama unavyofikiria... For example: Boss ananitaka kimapenzi kwa nguvu na ananifanyia vituko kila mara hata mbele ya wafanyakazi mwenzangu. Wakati huo huo boss pamoja na hao wafanyakazi ni member humu na tunafahamiana unadhani issue kama hiyo naweza kuibadili vipi wakati nataka nifunguke kwa kina ili nipate ushauri...????
 
Last edited by a moderator:
I knw it feels bad, then the best option ni kuPM mshauri anayeweza kudeal nalo jambo hilo.
 
Kwanza shikamoo dada mkubwa..Pili nakubaliana na ushauri wako.. ila kumbuka kuwa kuna issue ambazo ulishawahi kusema kwa njia moja ama nyingine hukuwahi kuzipitia.

Na zile ambazo umekuwa ukifunguka hapa jukwaani ni za kawaida sana ambazo hata.mimi naweza kufunguka.

Hapo mwishoni naona ndiyo pana faa zaidi kuwa niMPM USHAURI kisha yeye ndie anaweza kuileta jukwaan....
marahaba mdogo wangu.
ila kweli nafikiri ni wakati mzuri sana wa sasa kumtumia mama/baba USHAURI hasa kama tatizo lako hupendi liekwe hapa jamvini.

hapa ishu ni kujua kama huyu USHAURI atakuwa available muda wote. na pia confidentiality kwake ikoje. lakini sidhan kwamba kwenye hivi vipengele hata kuwa competent as washauri wengi ni watu wenye uzoefu wao kitaalamu kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli mkuu... Mficha maradhi kifo humuumbua ila si kila tatizo kila mtu alifahamu. Kuna wakati mtu anaweza kupost tatizo lake mwingine anamcrash hata kumtukana. sio jambo jema kutukanwa kama mtoto na watu wanakufahamu... Kuna wakati hata nahitaji ushauri wa kina kuhusu kazi na wafanyakazi wenzangu hata boss ni member humu, unadhani ni busara wao kuhafamu may be nataka kuacha kazi, au nimefanya kosa flani kazini lakini sijajulikana ila natafuta mbinu ya kurekebisha.. Au mchumba wangu yupo humu na ninahitaji ushauri juu yake, unadhani nitaweza kuomba ushauri???
Natambua kuwa kuna mambo ya kuweka humu na kuomba ushauri lakini ambayo yanagusa maisha yako ya kila siku na haijalishi kama Boss wako yupo humu au mwenza,kikubwa cha kuangalia ni kwa namna gani unataka ushauri juu ya jambo unalotaka ushauri,kama utataka ushauri wa kumuangamiza Boss wako au kumcheat si rahisi kwako kuliweka hapa maana watakufahamu ila kama unataka ushauri wa ufanye nini kuboresha mazingira yako ya kazi au changamoto unazopitia kazini,inawezekana kabisa kuomba ushauri hapa maana inawezekana Boss wako hajui kinachoendelea ofisini na utakuwa umemsaidia vivo hivyo kwa mwenza wako kama ana tabia mbaya na huipendi utakuwa umemsaidia kubadilika kama ataona post yako humu ingawa inawezekana ni vigumu kwako kumwambia face to face.
Kuna watu wachache sana ambao wana uwezo kumwambia Boss wake ananuka viatu,wengi ni waoga wa kuanika matatizo kitu ambacho huwa hakisaidii kulitatua.
 
Hili nalo geni..huyu USHAURI ndio nani??ni ngumu kuwin trust yake kirahisi humu jamvini labda mpka tumzoee kwanza kama ambavyo imekuwa kwa baadhi ya member kama@ashadii .

hilo nalo neno. lakini uzi wake wa jana ulinionyesha kwamba ni mtu ambaye ana utaalam wa haya mambo ya ushauri. na ukweli so long as simjui but ananishawishi kwa maelezo yake basi sion tabu kum-pm when needs arises.

mara zote nimejifunza kuwa na +mind towards others.
 
hapa naona akili ya mama/baba USHAURI iliwaza mbali sana sana. hili ni tatizo kwa mtu mwenye aibu ingawa kwa mtu free kama mm sio ishu kabisaa ingawa jamvini nusu yao wananijua na nimewah kuonana nao ila nikipata gumu huwa nalirusha live. na hata majuzi tu nimetoka kuomba ushauri hapa licha ya kwamba niliyoyaeleza wengine walibahatika nikiwa kwenye hali hiyo.

ushauri wangu kwako m-pm USHAURI atakusaidia na kama ni wa kitabibu pia anaweza kukusaidia.

Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa......................nusu ya wanajamvi wanakufahamu!!
mm hata mmoja simfahamu............zaidi ya IDs zao!!
Umempa ushauri mzuri huyo dada...............hope atazingatia!!!!
Lazima afahamu kuwa ''human wants are never satisfied" akijaribu kuishi kwa pressure ya sisi binadamu duuuuu tutamzika akiwa hai.................akipatwa na la kupatwa asiogope kulimwaga.................watu kibao wanatembea na matatizo lukuki ila tu wanapretend wapo fiti.......................so let her try to be her because she is her by nature, and we are us by nature just general life confrontations changed us!!
 
Habari zenyu binafsi wanajamvi…… Natumaini mko pouwa!!!!!!

Kutokana na kufahamiana mpaka kukutana na baadhi ya memberwa JF, nimekuwa nikipata shida katika kuomba ushauri wa baadhi ya mambo. Mfano1: Nina tatizo la kiafya na ninataka kuomba ushauri, nashindwa kufanya hivyokwa sababu unakuta flani ananifahamu kiuhalisia. Atajua kwamba nasumbuliwa natatizo Fulani la kiafya kitu ambacho sitopenda mtu mwingine afahamu zaidi yamshauri (Daktari).

Mfano 2: NInaweza kuwa na tatizo katika mahusiano yangu auhata kifamialia na ninahitaji ushauri , nashindwa kuomba ushauri kwani kila anayenifahamu kiuhalisia atajuakuwa nina tatizo katika mahusiano yangu au familia yangu.

Wadau, nifanyeje ili nisijulikane wakati Mods wanapingaissue ya kuwa na multiple IDs???????

(Nahisi pia kuna watu watakuwa na tatizo kama langu)

Wabheja sana!!!!! :A S angel:

Pole sana!!

Kweli kabisa nionavyo mimi privacy ni swala nyeti sana katika maisha ya binadamu yeyote yule. Haijalishi ni mtu mnafahamiana vp hata kama ni ndugu, mke, mme, a dearly friend, etc lakn privacy is always on track and you must keep in track kwa gharama yeyote ile. Hii ni kwa sababu kwa mtazamo wangu binafsi naona kama binadamu aweza kuwa ndio kiumbe chenye unafiki wa hali ya juu labda kuliko kiumbe kingine chochote kile hapa duniani.............. i mean trusting a human being is just a game of risk!!!!

Ushauri wangu kwako:
1. waweza kupost issue ya kuomba ushauri as if a friend of yours, ndugu, jamaa anaomba umshauri na wewe ukaja kwa members wa jf kuomba jinsi ya kumshauri..........ila sasa hv sijui km wataamini kuwa ni kweli si wewe
2. find another ID then develop taratiiiiiibu huku ukibadilisha style ya uandishi wako ili itofautiane na ile yako wanayoijua

3. tafuta mtu angalau unajua anaweza kukusaidia kuiwakilisha jamvini............huyo mtu awe na sifa kuu mbili a.asiwe na mtandao mpana wa marafiki na b. awe mtu mwenye silka ya kutunza siri za watu
4. just swallow pains and stand with your own legs..................the last sin i advice you to commit!!

Pole i can feel what you wish jamvi to feel!!
Thanks!!
 
Kila mwanadamu hukutwa na magumu na wakati mwingine huitaji ushauri na mtazamo kutoka kwa watu wengine.
Binafsi huwa naamini tatizo, kadhia au tukio lolote litokeapo huwa linashirikisha watu/mtu na mazingira.
Vile vile huwa naiamini sana serikali ya kichwa changu kuliko ya mtu yoyote yule(nadhani kila mtu anapaswa kuwa hivyo), maamuzi ya mwisho yafikiwayo katika ufahamu wangu kwa kiasi kikubwa yanapaswa yawe yamefanywa na mimi (Haijalishi nimepokea lundo la ushauri kiasi gani).
Hivyo basi pale unapoona kichwa chako kimeshindwa kutoa utatuzi, basi jaribu kuwajongelea watu wa karibu(wachache) wenye ujuzi wa mazingira ya tatizo lako (Try to narrow the possible ways of solving your problem, rather than JF'ing).
 
hilo nalo neno. lakini uzi wake wa jana ulinionyesha kwamba ni mtu ambaye ana utaalam wa haya mambo ya ushauri. na ukweli so long as simjui but ananishawishi kwa maelezo yake basi sion tabu kum-pm when needs arises.

mara zote nimejifunza kuwa na +mind towards others.
Ni vizuri kuwa na positive mind kwa watu..Lakn ni vizuri kuwa carefull sio na ndugu yako tu unamjua lakn zaidi sana kwenye huu ulimwengu wa keyboard.Mara nyingi unapoomba ushauri unaweza kujikuta unatoa very senstive information kukuhusu wewe au wale wakuzungukao..Hii ni hatari hasa kumuelezea mtu hata sura humjui au jina.Mie sishauri watu kuomba ushauri wa sensitive issues kwa watu wasiowajua..Ingekuwa ni bora sana kama mtu ana nia ya dhati kusaidia watu basi awe na Verified user name..Itasaidia sana kuwapa watu amani.
Hapa jf ni kama zile nyavu za kuvulia..zikitupwa zinakusanya kila kitu..Na kuna wengine hapa ni ma professional liars au matapeli na wanajua kuji disguise..Ni ngumu kumjua mtu mpaka ulizwe..Ndio maana kuna ongezeko la kulizwa watu kule love connect sababu ndio kama hizi watu wanajificha uhalisia...
Sina tatizo na huyo USHAURI lakn ni angalizo tu katika dunia hii ya leo ya kizazi cha nyoka.
 
Last edited by a moderator:
marahaba mdogo wangu.
ila kweli nafikiri ni wakati mzuri sana wa sasa kumtumia mama/baba USHAURI hasa kama tatizo lako hupendi liekwe hapa jamvini.

hapa ishu ni kujua kama huyu USHAURI atakuwa available muda wote. na pia confidentiality kwake ikoje. lakini sidhan kwamba kwenye hivi vipengele hata kuwa competent as washauri wengi ni watu wenye uzoefu wao kitaalamu kabisa

Hapo kwenye red ndipo penye utata!!! Kingine tutafahamuje yeye ni nani?? Huenda akaw anatuchora tu kumbe anatufahamu.....
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye red ndipo penye utata!!! Kingine tutafahamuje yeye ni nani?? Huenda akaw anatuchora tu kumbe anatufahamu.....

what matters to me ni kwamba so long as ananijua basi atanishauri na siku zote mshauri lazima ajue client wake, na kwakua unaanya online cancelling sitoangalia ananijua ama la ila ananishauri?? na kwakua simjui ni wazi kwamba sitoumia kwamba fulan analijua tatizo langu ila ninauhakika tatizo langu liko sirini.

huu ni mtazamo wangu tu ngoja tuone kama huyu mama/baba USHAURI anasemaje hapa.
 
Last edited by a moderator:
Habari zenyu binafsi wanajamvi…… Natumaini mko pouwa!!!!!!

Kutokana na kufahamiana mpaka kukutana na baadhi ya memberwa JF, nimekuwa nikipata shida katika kuomba ushauri wa baadhi ya mambo. Mfano1: Nina tatizo la kiafya na ninataka kuomba ushauri, nashindwa kufanya hivyokwa sababu unakuta flani ananifahamu kiuhalisia. Atajua kwamba nasumbuliwa natatizo Fulani la kiafya kitu ambacho sitopenda mtu mwingine afahamu zaidi yamshauri (Daktari).

Mfano 2: NInaweza kuwa na tatizo katika mahusiano yangu auhata kifamialia na ninahitaji ushauri , nashindwa kuomba ushauri kwani kila anayenifahamu kiuhalisia atajuakuwa nina tatizo katika mahusiano yangu au familia yangu.

Wadau, nifanyeje ili nisijulikane wakati Mods wanapingaissue ya kuwa na multiple IDs???????

(Nahisi pia kuna watu watakuwa na tatizo kama langu)

Wabheja sana!!!!! :A S angel:

Ndio Maana few know me..and i am not posting my staff anymore....:A S-heart-2:
 
Back
Top Bottom