pole mwaya
charminglady, kweli inauma na inakera ukiwa na shida na uko down halafu kuna watu wanakuletea mizaha, kwamantiki hiyo inaonesha mtu unakuwa huru iwapo hujulikani upande wa pili means in real world ila kwa kuwa wewe ushajulikana na wengine na wengi wanaendelea kujuana basi litatue nje ya jf, piga moyo konde kama ni swala la ofisi kalizungumze na mama yako, baba, dada au kaka au rafiki yako anayefanya kazi kwingine.( Ndugu wa karibu ni bora zaidi).
Kama tatizo ni la ugonjwa basi usisite kwenda hospitali moja kwa moja bila kufanya ajizi hata kama umepata mimba ambayo si ya mumeo/mpenzio, au umepata gonjwa la zinaa wahi hospitali lipia tu kumuona daktari upate ushauri kwa usiri wa hali ya juu hata mumeo hatajua.
Pia kama tatizo ni la ntumbani/mtaani aidha umemfumania mumeo au wewe ndo umefumaniwa au ni jambo la aibu kwa baba au mama yako na uko desperate wa kukushauri hapa ni rafiki ambaye unamtrust kuliko marafiki wote anaweza kuwa mnafanya nae kazini au anafanya kazi pengine ila hatakiwi kuwa wa mtaani kwenu au ndugu.
Nimejaribu kutoa mifano ya jinsi kama imetokea hivo na unajulikana hapa jamvini nini ufanye, believe me kujulikana hapa hata ukimpm mtu itakusumbua akili bora uje uwasimulie watu baadae tatizo lishaexpire kama story anazoletaga kaka
Mtambuzi hii pia ni njia ya kutoa mambo yako ya siri ila yanakuwa ya zamani na unashare kama story tuu.
All the best mamii.
Pamoja sana, always Sakapal.