Ushauri juu ya kozi ya Kodi (Taxation)

senzoside

Senior Member
Mar 13, 2012
183
31
Habari wadau,

Ningependa kufahamu mtu anayesoma kozi TAXATION anaweza kufanya kazi sehemu zipi?

Na kati ya kozi ya TAXATION na PROCUREMENT ni ikozi ipi yenye soko zaidi
 
TAXATION muajiri mkubwa ni TRA (Idara ya kodi - Serikali). Unaweza ukaajiriwa na taasisi kubwa binafsi (chache sana) kwa ajili ya maswala ya kodi.

PROCUREMENT ni Ugavi ( Storage + logistik) - Muajiri mkubwa ni serikali, hususan halmashauri.

Kimsingi kozi zote hizo mbili ni finyu hasa katika upande wa ajira. Mfano mdogo kama halmashauri wanahitajika wahasibu (acountant) 8, basi sehemu hiyo itahitaji watu wa procurement 2 mpaka 3. Mhasibu anaweza kufanya kazi ya mtu wa TAXATION.

Kama umepata zote ningekushauri kuchukua TAXATION. Vinginevyo ni mapenzi yako mwenyewe tu, kwani hazitofautiani sana kivile katika ajira.
 
Sawa mkuu nashukuru sana kwa respond yako
 
WANAFUNZI WATARAJIWA...someni kimkakati.
Kozi ya kodi ni ya ubobevu wa awali. Early specialization. Maana kodi inasomwa kwenye kozi nyingi kama somo. Uhasibu una kodi ya kutosha..nk.
Angalieni course content.

Procurement nayo ni nzuri ila kile kikolezo ndo cha kuangalia... procument and.... logistics? Supply? Supply chain management? Nk.
Narudia someni course content kwa makini.
 
Kodi sikushauri bora procurement....nilisoma Tax nina ajira ila changamoto zake ni ngumu mno maana hata huko Tra Mhasibu anafanya kazi za mtu wa kodi
 
WANAFUNZI WATARAJIWA...someni kimkakati.
Kozi ya kodi ni ya ubobevu wa awali. Early specialization. Maana kodi inasomwa kwenye kozi nyingi kama somo. Uhasibu una kodi ya kutosha..nk.
Angalieni course content.

Procurement nayo ni nzuri ila kile kikolezo ndo cha kuangalia... procument and.... logistics? Supply? Supply chain management? Nk.
Narudia someni course content kwa makini.
Procurement yenye kikolezo kipi ni nzuri zaidi?mkuu
 
Soma procure ipitaa kila sehemu ila kama ungependelea zaidi ungesoma account.
Procure kila sehemu department ipo
 
Back
Top Bottom