Ushauri: JKT kwa Mujibu wa sheria ifutwe, badala yake vijana wapelekwe VETA miezi 3 au 6

VTC ni muhimu sana. Wazo la kwamba VTC ni kwa walioshindwa kupata fursa kwingine, ni wazo linalotakiwa kuondolewa.

JKT ibaki. Ila iwe kwa ajili ya kuandaa jeshi la akiba. Kuruti wakifika tu, wapewe mafunzo ya awali. Kisha, wahamie kwenye tahasusi -- kurusha midege ya kijeshi na ya kivita; kuendesha vifaru; kufyatua mizinga; kuendesha manowari, nk.
 
lol, jeshi la akiba kwani tunajiandaa kupigana na nani mbona tunaishi kwa amani na majirani zetu,
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri Serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea Serikali ya viwanda.

Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.

Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Veta iko pale kwa kwa malengo tofauti na JKT pia ina malengo tofauti. Kwa hiyo kuifuta mojasiyo jibu. JKT kwa kifupi ni jeshi ikiwa na malengo ya kijeshi. JKT inatoa mafunzo ya kijeshi, uraia, na ulinzi wa nchi. VETA inatoa mafunzo ya ulinzi ikilenga ajira..kujiajiri au kuajiriwa.
 
lol, jeshi la akiba kwani tunajiandaa kupigana na nani mbona tunaishi kwa amani na majirani zetu,
Unataka ukivamiwa ndiyo uanze kujitayarisha. Kuwa na amani na majirani leo, haina maana mambo hayatakuwa tofauti kesho. Nani alijuwa tutapigana na Uganda enzi hizo!
 
Siungi mkono kufutwa kwa JKT bali naunga mkono kuimarisha JKT kwa kuifanya iwe sehemu yakutoa mafunzo ya stadi za kazi za muda mfupi kama baadhi ya mafunzo yatolewayo VETA.
 
Wazo zuri sana ila serikali haiwezi kukubaliana nalo maana wanapata free labourers for 3 to 6 months ambao malipo yao ni kula na kulala tu , kumbuka miradi mingi ya ujenzi ya serikali wamepewa JKT.
 
Wazo zuri sana ila serikali haiwezi kukubaliana nalo maana wanapata free labourers for 3 to 6 months ambao malipo yao ni kula na kulala tu , kumbuka miradi mingi ya ujenzi ya serikali wamepewa JKT.
Wapelekwe vijana wa kujitolea tu sasa, waongeze namba.
 
Habari zenu wanajukwaa?

Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri Serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea Serikali ya viwanda.

Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.

Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.

Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.

Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.

Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.
Jkt pia kuna veta, ukijiunga kwa kujitolea utaelewa
 
Mimi nashauri tujikite kwenye kanuni zilizoanzisha VETA na JKT vina malengo yanayofanana? Mimi nadhani vyote viwili viwepo kwani malengo yake ni tofauti, Pia kwa mujibu wa Sera ya elimu ya Tanzania Ni kwamba kijana amalizapo kidato Cha nne hupewa Uhuru wa kuchagua Kama anapenda kwenda Ufundi( Dar Tech, Mbeya Tech na Arusha Tech majina ya zamani) na Kidato Cha tano, ambapo VETA walikuwa wakichukua darasa la saba, ambapo huyu lasaba akifika (Grade I kwa zamani) aliepata sifa ya kuendelea ktk vyuo hivyo hapo juu, Sasa kwa Sasa naona hata VETA nae anachukua darasa la 12( form four) ambapo mtoto akifeli darasa la saba anajikuta Hana pakwenda zaidi ya kujishikiza kwa mafundi binafsi. Tukiweza kucheza vizuri na darasa la saba na kidato Cha nne wachague wanapenda kusoma Nini, Kisha hizi Taasisi ziwe zinashawishi na kufafanua ili watoto waone waende wapi Mara baada ya kumaliza masomo yao.
Aidha wale wanaopenda Mambo ya Ulinzi/ Usalama ndio waende huko JKT, Nina uhakika tungesonga mbele Sana.
 
mpaka leo sjui hata nlienda kufuata nin, kutesana na kudhalilishana kuumizana kutukanana na wadada hutongozwa sana kule.haina faida ifutwe
 
Mimi binafsi naona wasisitishe mafunzo ya JKT Bali wafunagamanishe mafunzo ya JKT na mafunzo VETA yaende sambaba, kwa, maana kwamba wafundishwe ukakamavu pamoja na Ufundi .
 
Back
Top Bottom