Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Habari zenu wanajukwaa?
Ngoja nijikite kwenye lengo la uzi. Naishauri Serikali sasa wabadili mwelekeo katika kuelekea Serikali ya viwanda.
Vijana wanaomaliza kidato cha sita wapelekwe VETA kwa miezi 3 ili wakapate mafunzo ya awali (basic) ya ufundi mbalimbali.
Kwa kufanya hivi itasaidia kuwaandaa vijana wenye ujuzi mbalimbali mitaani. Kuna kozi nyingi tu ambazo kijana akizipata kwa miezi 3 anaweza kuamka na kujiajiri au hata kuajirika as general helper au fundi mwanafunzi.
Binafsi nimepitia JKT Mujibu wa sheria Ruvu na nilibahatika kupata ajira kupitia gamba la JKT ila wenzangu wengi wamemaliza digrii na hawana kazi mitaani.
Serikali inatumia kiasi kikubwa sana kumrecruit kijana mmoja wa jkt kwa miezi 3 au 6. Ile fedha ingetosha kumlipia ada VETA na akimaliza miezi 3 akapewa kamtaji.
Viongozi natumaini mtalitendea kazi suala hili.