USHAURI: Je, aache kazi aende BBT?

USHAURI: Je, aache kazi aende BBT?

Habari wakuu,

Nina mdogo wangu ana Bachelor ya Computer Engineering, sasa alipata kazi kwenye kampuni moja Posta huko kama mtu wa Sales/Customer Service, analipwa laki tatu kwa mwezi.

Juzi kapokea taarifa kwamba anahitajika Dodoma kesho kwa ajili ya mafunzo ya mambo ya kilimo ya BBT ya muda wa miezi mitatu.

Sasa naomba mnishauri, maana wiki 2 zilizopita nimetoka kumpatia Kodi ya chumba na kumnunulia mahitaji zaidi ya 1 million ili apange, na kashapanga alikuwa anasema kwangu mbali na kazini. Mimi naona bora aendelee na kazi hapahapa town lakini labda namkosesha fursa!

Naomba ushauri wenu wakuu.
Dah computer engineer anafanya sales!!? Nimesikitika sana!! Mshauri ajisajili ERB kama graduate l.

NB: aende BBT kuna future nzuri. Wakimaliza wanakabidhiwa eka 10 kwa ajili ya kilimo
 
Aiseh nimejitahidi nipate muda nikomment


Mkuu Epuka project zenye mikono ya kisiasa ni hatari. Level of Risk kwenye project zenye mikono ya kisiasa IPO juu Sana.

IPO siku anaweza kutokea waziri akasema hiyo project ifutwe ukabaki unashangaa.

Muache kijana akomae mjini atangeneze network Kwa kuanzia hapo alipo. Najua huo mshahara sio mkubwa Kwa Dar lakini Kwa Dar ukiwa na pakuanzia sio mbaya. Kupitia hapo naamini akiwa MTU WA kujiongeza atafika anapotaka kufika.


Ushauri wangu aachane na hizo project za kisiasa na ajikite kwenye hiyo ajia yake mpya.




Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Nimwkuelewa mkuu
 
Unaikumbuka kilimo kwanza ya yule Mheshimiwa wa sumbawanga ? Iko wapi ?

Tatizo akishaamua huwezi kumbadilisha.

Hata hivyo unamnunulia fanicha na kodi kwani yeye hiyo laki tatu anafanyia nini, uwe tu una busti pale anapokwama
300K kwa town inaishia kwenye chakula tu, ilibidi hadi mashuka ninunue
 
Habari wakuu,

Nina mdogo wangu ana Bachelor ya Computer Engineering, sasa alipata kazi kwenye kampuni moja Posta huko kama mtu wa Sales/Customer Service, analipwa laki tatu kwa mwezi.

Juzi kapokea taarifa kwamba anahitajika Dodoma kesho kwa ajili ya mafunzo ya mambo ya kilimo ya BBT ya muda wa miezi mitatu.

Sasa naomba mnishauri, maana wiki 2 zilizopita nimetoka kumpatia Kodi ya chumba na kumnunulia mahitaji zaidi ya 1 million ili apange, na kashapanga alikuwa anasema kwangu mbali na kazini. Mimi naona bora aendelee na kazi hapahapa town lakini labda namkosesha fursa!

Naomba ushauri wenu wakuu.
Aachane na mambo ya BBT ya kichamachama hayo, akomae na kazi mjini kuna siku patatiki sehemu nzuri.
 
Dah computer engineer anafanya sales!!? Nimesikitika sana!! Mshauri ajisajili ERB kama graduate l.

NB: aende BBT kuna future nzuri. Wakimaliza wanakabidhiwa eka 10 kwa ajili ya kilimo
Ishawai kufanyika hii project?
 
Back
Top Bottom