Natafuta kazi yoyote itakayonisaidia kukusanya pesa ya kurudi masomoni

buswagg

JF-Expert Member
Oct 21, 2023
418
726
Habari wakuu. Niko mbele yenu nina shida naomba msaada wenu, sababu najua humu mpo watu aina mbalimbali na wenye kufahamu zaidi mambo mengi.

Mimi ni binti, miaka 24 sasa, nilibahatika kusoma hadi chuo, japo sikumaliza kuna changamoto ilinipata ghafla ikabidi nisikamilishe masomo kwanza.

Sasa jambo langu leo ni hili, nahitaji nipate ajira yoyote ambayo itakua available ili niweze kujisaidia mwenyewe, yes mzazi yupo japo kwa sasa anachangamoto kubwa anadeal nayo hivo imemuelemea, na mimi nahitaji niendelee na elimu hata kidogo kidogo nikiwa nafanya kazi huku najisomesha

Naomba msaada wenu, naweza kufanya kazi yoyote halali. Nimewahi kufanya kazi kama cashier mahali furani, sales, nimewahi kuwa mtu wa customer service katika restaurant, pia nimewahi fanya baadhi ya self local businesses, hivo nina uzoefu kiasi katika ajira.

Ila nafasi yoyote nafanya, iwe kuuza duka, supermarket, kusimamia biashara kwa uaminifu na uchapakazi mkubwa, hata nikipata kazi za nyumbani either za kwenda na kurudi, kuhudumia familia, na kila kitu naweza, ilimradi niwe napewa nafasi ya kuudhuria vipindi chuo.

Najua sio rahisi, lakini mimi ni mpambanaji, naelewa nilichofata kazini hivo tafanya kazi kwa bidii sana. Shukrani kwenu na nahitaji msaada wenu, ushauri nk. Bado najitafuta na Mungu asaidie. Kama umeguswa na ombi langu niulize lolote unalotaka kufahamu nami tatoa ufafanuzi. Please wakuu, nawahitaji, jambo lolote unalohitaji mtu tafadhari nijulishe tuzungumze. Mungu awabariki.
 
Umefika chuo kweli wewe? Mbona uandishi wako wa hovyo. Elimu ya siku hizi hakuna kitu. Pamoja na mapungufu unahitaji usaidiwe. Wana JF tumsaidieni kijana
 
Taja nini hasa kilikufanya usimalize chuo maana tunaeza tukakupa ajira then ukaacha kama ulivyoacha chuo
 
Pole Sana kama upo dsm njoo clouds Fm siku ya jumapili upate kukutana na Dr Issac Maro ,ukifika hapo utapata Ada ya shule na hela ya kujiendesha mwenyewe unaweza fanya Biashara

Njoo Katika njia Panda mkuu utasaidiwa
Habari wakuu. Niko mbele yenu nina shida naomba msaada wenu, sababu najua humu mpo watu aina mbalimbali na wenye kufahamu zaidi mambo mengi.

Mimi ni binti, miaka 24 sasa, nilibahatika kusoma hadi chuo, japo sikumaliza kuna changamoto ilinipata ghafla ikabidi nisikamilishe masomo kwanza.

Sasa jambo langu leo ni hili, nahitaji nipate ajira yoyote ambayo itakua available ili niweze kujisaidia mwenyewe, yes mzazi yupo japo kwa sasa anachangamoto kubwa anadeal nayo hivo imemuelemea, na mimi nahitaji niendelee na elimu hata kidogo kidogo nikiwa nafanya kazi huku najisomesha

Naomba msaada wenu, naweza kufanya kazi yoyote halali. Nimewahi kufanya kazi kama cashier mahali furani, sales, nimewahi kuwa mtu wa customer service katika restaurant, pia nimewahi fanya baadhi ya self local businesses, hivo nina uzoefu kiasi katika ajira.

Ila nafasi yoyote nafanya, iwe kuuza duka, supermarket, kusimamia biashara kwa uaminifu na uchapakazi mkubwa, hata nikipata kazi za nyumbani either za kwenda na kurudi, kuhudumia familia, na kila kitu naweza, ilimradi niwe napewa nafasi ya kuudhuria vipindi chuo.

Najua sio rahisi, lakini mimi ni mpambanaji, naelewa nilichofata kazini hivo tafanya kazi kwa bidii sana. Shukrani kwenu na nahitaji msaada wenu, ushauri nk. Bado najitafuta na Mungu asaidie. Kama umeguswa na ombi langu niulize lolote unalotaka kufahamu nami tatoa ufafanuzi. Please wakuu, nawahitaji, jambo lolote unalohitaji mtu tafadhari nijulishe tuzungumze. Mungu awabariki.
 
Pole Sana kama upo dsm njoo clouds Fm siku ya jumapili upate kukutana na Dr Issac Maro ,ukifika hapo utapata Ada ya shule na hela ya kujiendesha mwenyewe unaweza fanya Biashara

Njoo Katika njia Panda mkuu utasaidiwa
sawa sawa, shukrani sana mkuu
 
Back
Top Bottom