Demu wangu amepata kazi Casino. Je, nimruhusu afanye kazi hiyo?

knows

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,403
2,006
Habarini, nina imani wote ni wazima Mungu anaendelea kutupigania.

Nina changamoto naomba ushauri wakuu.

Nina demu nipo nae kwa mahusiano lakini hii wiki sasa temekuwa tukipishana ishu nikwamba huyu dem kapa kazi kwenye CASINO moja kubwa tu hapa jijin Dar akaja kunieleza na kuniomba ruhusa nimruhusu akafanye kazi huko CASINO.

Lakini ukweli nilimkatalia kabisa na nikamwambia staki kusikia habari za kufanya kazi CASINO na ananijua nikishakataaga kitu nimekataa sasa yapita wiki kila siku akija home nikulia na kuniomba nimruhusu akafanye kazi huko na mimi staki.

Sasa imefika hatua analalamika kuwa namuonea tu kwa kumkatalia kufanya hiyo kazi kwakuwa wanatamlipa vizuri.

Sasa nimekuja kwenu wakuu mnishauri kwa mnavojua kazi na mambo yanayoendelea huko kwenye makasino; je na kazi zauko zilivo maana mengine siyajui ya huko nilegeze kamba nimruhusu kama anavolalamika au niendelee kukaza kamba na kusimamia msimamo wangu uleule kuwa siitaji.

Kwenu wakuu naimani mtanishauri vyema na ndomana nimekuja kuwawasilishia jambo hili Mingu awabariki
 
kama unatarajia aje kuwa mke wako usimruhusu...
kama unasogeza nae siku ili mradi umpelekee moto basi mruhusu...
mwanamke kufanya kazi sehem za starehe ni sawa na kupanda miwa karibu na shule...
Daah ndomana nakataa kabsa hilo jambo mkuu
 
Muulize mshahara sh ngapi then mlipe asiende kama kwa sasa hauko vizuri hata ukimzuia hutafanikiwa....NB kama ana chura tutafaidi ipasavyo.
daah nacheka lakini naogopa
 
Punguza uzinzi vuta jiko

Mtoto wa watu unamtumia hutaki akae kwako

Hutaki atafute kipato chake

Oa ili aishi kwenye misingi ya ndoa kama unampenda

Kama humpendi mwache akapambane na hali yake

Uhuru wa mtu ni mhimu
Sawa mkuu nimekuelewa nitafanya maamuzi ulio niambia
 
Casino sio pazuri hayo maeneo unatakiwa kujiuliza wahudumu wa kike ni wengi kuliko wa kiume kuleta ushawishi wa kingono

Sikia nakwambia Fanya uoe kama hutaki kumuoa mwache aende huko casino usije ukaja kumuacha akiwa Hana ajira
Sawa mkuu nimekupata vyema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom