Msaada wa Kazi au Connection ya Kazi

crazyrider

Member
Jun 10, 2019
27
26
Habari wakuu,

Umri wangu ni miaka 28. Nimekuja kwenu kuomba ajira au mtu yoyote anayeweza kunisaidia kupata ajira au Connection.
  • Jinsia: Me
  • Elimu: Bachelor Degree of Banking and Finance.
  • Ninapoishi: Dodoma
  • Uzoefu wa kazi : Sina uzoefu mkubwa kwenye Carrier yangu zaidi ya kufanya Field mara mbili Bank flani.
  • Uzoefu wangu mkubwa nje ya Carrier yangu ni Kazi za Sheli ambayo nimewahi kufanya kazi kama Manager, Assistant Manager na Pump Attendant, kwa maana hiyo nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika issue za sheli au Petrol Station.
Naomba yeyote anayeweza kunipa ajira kwenye office yake/connection ya ajira anisaidie.
Ninaweza kufanya kazi kama vile;
  • Bank teller
  • Customer Service
  • Finance Officer
  • Loan Officer
Kwa upande wa sheli ninaweza kufanya kazi kama
  • Manager
  • Assistant Manager
  • Pump attendant pia
N.B Kwa kazi za sheli hakuna haja ya kufundishwa ninaweza kuripoti na kuanza kazi siku hiyo hiyo.

Sifa za ziada
  • Ninajua kutumia computer.
  • Ninafahamu kutumia Microsoft word, excel na PowerPoint.
  • Ninajua kutumia accouting software kama excel.
  • Uwezo wangu katika lugha ya kingereza ni mzuri, ninaongea (90%), kusikia na kuelewa (100%), kusoma na kuandika kwa ufasaha (100%).
  • Pia ni mchapakazi na ni muaminifu.
Yeyote anayeweza kunisaidia ajira au hata ushauri naomba aniambie nitamfuata inbox.
Au yeyote anaehitaji kuona CV yangu pia nitamtumia

Asanteni.
 
NDUGU YANGU, MIMI NINGEKUWA WEWE ningeomba sponsorship ya kuendelea na masomo USA ambako unaweza kusomeshwa kwa gharama zao na faida ya kubaki huko kwa muda sawa na ule ambao utakaa masomoni.

Bongo utakaa sana na ajira inayoendana na elimu yako huto pata, zidi kumuomba Mungu na ikikupendeza omba vyuo vya nje vingi kadri ya uwezavyo, hapa nchini kwetu swala la ajira limeshakuwa ugonjwa usio na tiba.

UBARIKIWE SANA NDUGU YANGU ukifanikiwa unikumbuke kwenye ufalme wako.
 
Jaribu na kupitia kule ajira portal,ajira nyingi za serikali zinapitia kule.
 
NDUGU YANGU....MIMI NINGEKUWA WEWE ningeomba sponsorship ya kuendelea na masomo USA ambako unaweza kusomeshwa kwa gharama zao na faida ya kubaki huko kwa muda sawa na ule ambao utakaa masomoni...bongo utakaa sana na ajira inayoendana na elimu yako huto pata...zidi kumuomba Mungu na ikikupendeza omba vyuo vya nje vingi kadri ya uwezavyo...hapa nchini kwetu swala la ajira limeshakuwa ugonjwa usio na tiba...UBARIKIWE SANA NDUGU YANGU ukifanikiwa unikumbuke kwenye ufalme wako
Nashukuru sana Mkuu hilo nitalishughulikia. Mungu akubariki pia Ndugu
 
Hili tangazo mbona nilishalisoma humu. Wewe ndio wale wa ku copy na ku paste huko vyuoni.
Mpaka hapo wewe sio mwaminifu wala mchapa kazi kama tangazo la kuomba kazi tu limekushinda kuandika.
 
Nenda Taesa pale utapata tempo serikalini then utapata ajira ya moja kwa moja after 6 months. All the best
 
MIMI NINGEKUWA WEWE ningeomba sponsorship ya kuendelea na masomo USA ambako unaweza kusomeshwa kwa gharama zao na faida ya kubaki huko kwa muda sawa na ule ambao utakaa masomoni
Hapa ungeweka hizo njia kuanzia pakuanzi hadi kumalizia kuhusu hili jambo ulilolisema na ungewasaidia vijana wengi si wakizazi hiki mpaka vijavyo. Tunaomba utuwekee hayo mawazo na huo mchakato ili na wengine waweze kufanya vile ulivyomwelekeza huyoo jamaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom