bongo-live
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 1,731
- 2,293
Mimi ni mbabaz wa miaka 39, sijaoa lakini naishi na mwanamke ambaye naweza kusema kuwa ni kama mke wangu kwani nilishamtolea mahari, tumeishi pamoja kwa miaka kumi bila ndoa, sikuona umuhimu wa kufunga naye ndoa kwani yeye ni mama wa nyumbani, nilijua kama nikifunga naye ndoa ikatokea tunatengana basi tunaweza kugawana mali hivyo nikawa nafanya mambo yangu kimya kimya.
Kila mara alikuwa akilalamika kufunga ndoa mimi nampiga chenga, lakini siku za karibuni amekuwa haulizii tena mambo ya ndoa, alikaa kimya kwa miezi sita mpaka na mimi nikaanza kuwa na wasiwasi. Nilianza kuchunguza kwani nilihisi kuwa ana mwanaume mwingine, huwezi amini nimegundua kuwa mke wangu ana mwanaume mwingine, tena mtu mzima ambaye alishaoa na kufiwa na mke wake pamoja na mtoto mmoja, alikuwa hajaoa muda mrefu baada ya kufiwa na mke wake.
Baada ya kuona hivyo niliongea na mke wangu akaniambia kuwa hakuna kitu kama hicho, nilimuambia suala la kuoana nikamuambia kuwa sasa hivi mimi niko tayari lakini yeye ndiyo akawa mtu wakunipiga chenga mara nyumbani hawajajiandaa, nyumbani hivi na nyumbani vile. Mimi niliamua tu kwenda mwenyewe lakini cha ajabu nimefika huko wakwe zangu wamekataa mimi nisimuoe binti yao, eti wanasema nimemchezea muda mrefu hivyo wamenirudishia mahari yangu ingawa mimi nimekataa kuzipokea.
Nimemuuliza mke wangu anajifanya hajui kitu, ananiambia lakini kama wazazi wameamua yeye si wa kuwapinga. Nimefuatilia kumbe kashampeleka yule mwanaume kwao na kajitambulisha na kutoa mahari.
Nilipombana na kumpiga kidogo aliondoka, niliamua kumtishia na kumuambia kama anaondoka na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine basi aniachie wanangu akanijibu hakuja kwangu na mtoto hivyo ni sawa tu nikibaki nao kwani ni wa kwangu hata kama nikiamua kuwanyanyasa ni mimi, ananitumia meseji ananiambia tena ni afadhali kwani ingemuwia shida kuanza ndoa mpya na watoto. Tuna watoto watatu na mke wangu kaondoka na kuniachia nao, sijui hata nifanyeje