Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,127
- 138,150
Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Klarensi Usakazi (86), mkazi wa Kitongoji cha Mbisi, Tarafa ya Chipanga, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, aliyeamua mtalaka wa mtoto wake ‘mkamwana’ aitwaye Mary (20) baada ya wazazi wake kudai kutokuwa na uwezo wa kurudisha mahari.
Hata hivyo, Mary anakuwa mke wa nane kwa Usakazi, wakiwamo wengine watatu wa familia moja ‘pacha’, ambao anadai kufurahishwa na tabia ya ukoo wao hadi kufikia uamuzi wa kuwaoa.
Usakazi mwenye ukwasi wa mifugo karibu kila eneo la Tarafa ya Chipanga alimuoa Mary Chaina (20) kupitia ndoa halali ya kimila iliyofanyika Januari 25, 2024, baada ya kuolewa na Fredrick ambaye ni mtoto wake.
“Ni kweli alikuwa mke wa mtoto wangu Fed (Fredrick), lakini waliishi mwaka mmoja na wakaanza kusumbuana. Mimi nikaona bora nimuoe ili kijana akatafute mke mwingine anayempenda na alifanya hivyo. Nikalipa mahari,” amesema.