Ushahidi: Waandikishaji waandika majina hewa ili kujaza akidi waonekane waliondikishwa ni wengi kumbe bao la mkono, yadaiwa ni agizo toka mzizi mkuu

Kuna baadhi ya wadau humu wanabisha! Ila kwa namna hilo zoezi linavyoendeshwa, hakika uwezekano wa kujaza majina hewa na kuyasaini, ni rahisi sana! Eti nasikia unamtajia wakala jina lako, halafu anakuandika, na mwisho anakupa sehemu ya kusaini!

Sasa kwa hali hiyo, si anaweza tu kuandika majina mengi hayo yaliyo kwenye huo ushahidi! na mwisho wa siku kusaini kwa niaba? Nilishangaa sana kusikia eti Dar es Salaam wameandikisha watu kwa zaidi ya 75%! Kirahisi tu ndani ya siku 2! Hakika siasa inaiharibu nchi yetu.
 
Uongo siku zote mwisho wake ni mbaya. Leo utafanikiwa kusema uongo lakini kesho utashikwa tu. Siku za mwizi ni arobaini. Kuna siku mwizi atakamatwa tu na kuwekwa ndani. Mwizi ni kati ya mfungwa mtarajiwa. Basi ukiwa mwizi, jiandae kwenda gerezani siku moja.
 
Cyber crime...law itumike kama kuna uzushi katika hili.i!!! Na kama ni kweli wahusika washughulikiwe kwa sheria zilizopo za utumishi wa umma na usimamizi wa uchaguzi.
====
Tunataka matokeo halali, hata kama kuna mbinu za kuchafua matokeo hayo.

Kwa taarifa yako matokeo halali ndio mwisho wa ccm. Sio kwamba ccm hawataki kushinda kihalali bali hawana uwezo wa kushinda. Sasa pata picha huu ni mwaka wa nne wanafanya siasa wao tu na maendeleo wanasema wameleta, na hujuma za wazi dhidi ya wapinzani wao, lakini umma ndio huo hautaki kushiriki uchaguzi, kwa sababu kama hizo. Hapo hujiulizi tu?
 
Hivi iliwachukua muda gani kufanikisha hiki mnachokifanya kwenye majukwaa ya kijamii?

Ni semina ya muda gani na mnaifanya kwa maslahi ya nani hasa?
 
Mkuu wakati mwingine unajishushia heshima yako kwa kupenda kutunga uongo!

Kama nakuona unavyotahayari kwa hiyo aibu. Vumilia tu maana ukishakataliwa umekataliwa tu hata utumie mabavu. Nashauri mtu yoyote anayejitambua asishiriki huo upuuzi unaoitwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom