Ushahidi wa video hii ni wazi Yanga ilinyimwa goli hapo jana

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,450
2,646
Jana Yanga haikustahili kuishia hatua ya robo, ile goli ni halali kabisa na ushahidi wa video ni huu hapa. Mpira ulivuka mstari wa goal line kwa zaidi ya asilimia 100 kisha uka rebound tena.
 
Attachments

  • NHhrcqrRQy_Q3mkB.mp4
    305.6 KB
Jamani mkubali kushindwa na maisha yaendelee how sure are you kuwa ingefungwa hilo goli mamelode wasingewafunga na nyie zaidi ya moja? Yani ingekua hivii..hilo goli lingeingiaa mngevimba kichwa mngejiachia yangeweza kurudi magoli hata 5 kwa zile kosa kosa zao..
 
Jana Yanga haikustahili kuishia hatua ya robo, ile goli ni halali kabisa na ushahidi wa video ni huu hapa. Mpira ulivuka mstari wa goal line kwa zaidi ya asilimia 100 kisha uka rebound tena.
Kinachoshangaza ni kwamba baada ya utata huu; CAF Haijatoa VAR views za angle mbalimbali kwa spidi tofauti ili kuhakikishia umma kuwa uamuzi ulikuwa ni halali au vipi: yaani ile clip fupi waliyotoa ndiyo final. Lakini niliangalia BeIn TV ikiliangalia bao hilo kutokea angles tofauti na kutamatisha kuwa lilikuwa golo halali.
 
Kosa walilolifanya Yanga ni kuendelea kucheza. Walitakiwa kugomea mchezo mpaka refarii aende kwenye VAR.

Wangekuwa Waarabu wangemzonga refa mpaka angeenda kwenye VAR na hata wangekuwa tayari kulimwa kadi.
 
mtasema yote leo.
 
Hili linahitaji semina kubwa sana kwa timu za Tanzania katika hili swala la kumlazimisha mwamuzi kwenda kujiridhisha. Unajua kabisa ile inaweza kuwa ndio mechi ya mwisho katika msimu huu kwanini wachezaji kadhaa wasimzonge refa mpaka aende kuangalia na yeye hata akikupa kadi sawa ila mechi isichezwe hadi akaangalie. Hapo ndipo waarabu wanatupitia kujiona sisi ni wanyonge. Wachezaji pia walizingua hapo
 
Tangu Jana azam tv waliporudia baada ya. Ki kufumua ile shoot tulishangilia tukijua Mpira unawekwa Kati lakini hii ndiyo afrika siwezi kushangaa , haki unanyimwa asubuhi na mapema .
 
Jamani mkubali kushindwa na maisha yaendelee how sure are you kuwa ingefungwa hilo goli mamelode wasingewafunga na nyie zaidi ya moja? Yani ingekua hivii..hilo goli lingeingiaa mngevimba kichwa mngejiachia yangeweza kurudi magoli hata 5 kwa zile kosa kosa zao..
Ilipaswa kuwa goli ndio maana ikatokea. Soo hata kama mamelodi walikuwa wafunge wangefunga tu hata baada ya goli la yanga kukataliwa
 
Kosa walilolifanya Yanga ni kuendelea kucheza. Walitakiwa kugomea mchezo mpaka refarii aende kwenye VAR.

Wangekuwa Waarabu wangemzonga refa mpaka angeenda kwenye VAR na hata wangekuwa tayari kulimwa kadi.
Timu yangu yanga tunaamini sana kwenye fair play sometimes inatuponza nilishangaa hata tulivyofika south tukapanda basi tuliloandaliwa na mwwnyeji hivi kwa figisu za soka la afrika unaweza kweli kukubali usafiri uliopewa na mwenyeji wako.!
 
Tangu Jana azam tv waliporudia baada ya. Ki kufumua ile shoot tulishangilia tukijua Mpira unawekwa Kati lakini hii ndiyo afrika siwezi kushangaa , haki unanyimwa asubuhi na mapema .
Ilivyorudiwa mara moja tu nililuka kwenye kiti kama kichaa nilijua mpira unapelekwa kati baada ya refa kukataa niliishiwa nguvu ghafla nilitulia chini kama dakika 20 hivi nikiwa dizaini kama sijielewi elewi vile
 
Back
Top Bottom