kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Wabunge na polisi wanapinga kila kitu Cha wapinzani na kuunga mkono kila kitu Cha Serikali. Inawezekana kweli wapinzani wana kasoro zao, lakini wanasaidia nchi kwenye checks and balances hasa kwa vitu vinavyokwenda umiza hata mama zao vijijini.
Tanzania hakuna kitu kizuri kuliko wengine zaidi ya utulivu kwa watu wetu. Tumewekeza zaidi kuhakikisha kuwa nchi Ina utulivu bila kujali kuwa watu wana Amani au la.
Polisi atamkong'ota mtu anaesema tunataka katiba mpya na kumuacha mtu aliyekula fedha za kupeleka maji kwa mama zao vijijini.
Mbunge anasahau kuwa ana mama, shangazi, binamu na wapwa ambao hawatanufaika na fedha za ubunge wake bali sera zitakazomsaidia kuwapatia mahitaji yao wao mwenyewe kwa nguvu na juhudi zao.
Ona sasa tunapoenda sheli kujaza mafuta hakuna tofauti Kati ya aliyeimba hiyenahiyena na peooooples, watoto wa polisi wanasoma pia shule hizihizi. Kila mtu analinda ajira isiyotoa majibu kwake, familia na ndugu zake vijijini.
Mpaka siku kila mtu atakapojitambua itakuwa too late. Tutakuwa tumeachwa nyuma na mataifa yote kwenye kila kitu na kila Jambo.