Usemi "Habari Ndiyo Hiyo" unatokea wapi?

Kitia

JF-Expert Member
Dec 2, 2006
418
74
Kwa muda kiasi sasa nimekuwa nikisikia msemo wa 'Habari ndiyo hiyo'. Je huu ni msemo ambao upo sasa katika jamii ya Tanzania? Na kama ni hivyo chanzo chake ni nini? Natanguliza shukrani.
 
Kwa muda kiasi sasa nimekuwa nikisikia msemo wa 'Habari ndiyo hiyo'. Je huu ni msemo ambao upo sasa katika jamii ya Tanzania? Na kama ni hivyo chanzo chake ni nini? Natanguliza shukrani.
Kwenye Bongo Flavour music
 
Na leo Naibu Spika baada ya kumjibu Zitto Kabwe akamalizia na "Habari ndo hiyo!"
 
Habari ndiyo hiyo inaweza kusisitiza zaidi habari kuliko kui endorse.

Kwamba huu ndio ujumbe, lakini mimi kuutoa ujumbe simanishi kwamba ujumbe huu ni wangu au nakubaliana nao. Ni kama disclaimer fulani ninavyoelewa mie.
 
Asanteni sana wote kwa maelezo hayo. Baada ya SaidSabke kuniambia ni wimbo wa Bongo Flava, nikaenda YouTube na nikaweza kuuangalia. Ni wimbo mzuri. Asanteni sana, maana kwa wengine ambao hatupo nyumbani, misemo mingi inatupita. Wakati uliopita kulikuwa na forum ya Tanzanet ambapo kulikuwa kunawekwa misemo mipya. Hii ilitufanya wengi tuwe 'uptodate' na mabadiliko ya lugha.
 
na leo naibu spika baada ya kumjibu zitto kabwe akamalizia na "habari ndo hiyo!"

ukweli ni kwamba aliyesema "habari ndio hiyo" bungeni wakati naibu spika anamjibu zitto sio yeye naibu spika. Sauti ilitoka sehemu ya waheshimiwa wabunge - lakini ilikuwa ya mbunge mwanamama, ikaonekana kama naibu spika ndio kasema "habari ndio hiyo".

Macinkus
 
Haya maneno yalianzia kwenye Bongo Flavour na specifically kwa Mwana FA a.k.a Binamu, ni sawa na maneno kama WIZI MTUPU from Komedi Orijino etc
 
Haya.

Mimi nina msemo wangu wa kuuliza.

Msemo wa "Ndivyo Sivyo" una maana gani haswa? Je ni sawa kusema "Sivyo Ndivyo" katika hali ya kumaanisha kinyume na "Ndivyo Sivyo?"
 
Back
Top Bottom