Usanii mpya wajitokeza Tanzania

Usanii mpya wajitokeza Tanzania

Yule aliyekuwa anafanya maigizo ya kupiga matofali na kujenga nyumba hamkumuona eeh!!!
Ratiba ya lowasa;
Trh 24/08/15-kupanda daladala kukutana na wananchi
Trh 25/08/15-kupata chai kwa mama ntilie walioko mtaani
Trh 26/08/15-kwenda Tandale kubeba magunia.
Trh 27/08/15-kukutana na wachimbaji wa kunduchi na kufyatua Matofali
Trh 28/08/15-kwenda karume kuuza mitumba
Trh29/08/15-kufanya usafi kwa kusafisha mitalo na bararbara zilizopo
dsm
Tar 30/08 KULALA MWANANYAMALA WARD YA WAJAWAZITO.
31.8 Segerea kulala na wafungwa ajifunze shida zao
 
kiujumla siasa ni usanii,hakuna mwenye afadhali wanataka kutushawishi kwa uongo tuwape kura na hizi ahadi zao wapelekwe mahakamani waape kabisa wakishindwa kuzitekeleza anyongwe na yeye mana atakua ameshaua wengi sana kwa uongo wake.
 
Tata upo Sawa, shida ya wa tz hatuna hoja za mstakabali wa maisha ya mtz na kizazi kijacho.
 
Tunasema ni usanii kwa sababu tujiulize,amekuwa kiongozi kwa muda zaidi ya miaka 20 alikuwa wapi siku zote kutembelea hao walalahoi anaodai, au wakati akiwa waziri mkuu shida hizo hazikuwepo,kama Mtanzania mzalendo unapaswa kutafakri hilo na si kufurahia hayo maigizo.

Kama mtanzania mzalendo unapaswa kutafakari chama tawala kimekuwa madarakani zaidi ya miaka 50 kimekuwa wapi siku zote kuona hizo shida na sio kuja kutuhaidi mambo mapya sasaivi
 
you have made my day brother, nimecheka mpaka!! Title umeipatia vzr mno, na content pia

Ndg yangu kati ya Usanii wa CCM na Lowassa upi unastahili tunzo na nishati? Usanii wa Kupandisha TWIGA kwenye ndege??? usanii wa kupitisha meno ya tembo uwanja wa ndege??? haya ilitupasa kuyashangaa watanzania sio Mh lowassa kuwatembelea wanachi wake kujua matatizo!! sasa hufikirii akiwa Raisi ni lini atayajua matatizo ya wananchi wake ayatatue akiwa president kama sio sasa????

tuache ushabiki maandazi na siasa za maji taka! ni kweli ccm inamuogopa LOWASSA akienda msibani StOP.akienda kutembelea wananchi STOP mnataka aende wapi???
 
jamani tukubali au tukatae huu ni mwaka wa wa edward lowassa,mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
 
Eti Lowasa leo anakunywa chai iliyounga sukarı ya PK kweye kikombe kilichofubaa.Adaa hz ni balaa!Huyu jamaa kapania Urais s kdogo.
 
Hata kuhonga makundi ya raia kuja kwake kuigiza kwamba wanamkubali ni sawasawa?
Mifano kibao point 0!

km unachokiongea ni sahihi weka picha ili tuamini maana maccm yanabebwa kwenye mafuso km kokoto
 
umeandika vizuri sana, nakiri umenishawishi kumpigia kura magufuli 25.10.2015, anafaa sio msanii, huyo mwingine aajiriwe kaole

Huwa nafurahia sana pale mtu anapofanya mambo yanayofanya aitumie taaluma yake kwani ni kuonesha wazi kwamba hukwenda kusoma bure bure tu. Bila hivyo, ukisoma tu na kuweka makaratasi yako nyumbani hamna mtu yeyote atayeweza hata kuja kuotea umebobea kwenye tasnia gani hasa.
Huyu bwana mkubwa alichofanya ni kutumia taaluma yake ya maigizo na kuipeleka mtaani. Labda kwa sababu siku yake ya kuzaliwa ilikuwa inakaribia hivyo akaona ni bora kuwaalika wale alowaita "malofa" wenzake eti. Haya si matusi jamani! Yaani mnatukanwa na kukebehiwa mbele ya macho yenu mchana kweupe na mnamuangalia tu huyu babu! Mbona alishajulikana tangu muda mrefu kuwa ni mwizi aliyekubuhu na mwana sanaa wa hali ya juu katika kujipatia madili na kuwapa kwa upendeleo wa tenda za serikali marafiki zake au watu wenye kampuni ambazo yeye binafsi ana maslahi nazo? Na bado ana uthubutu wa kuja kukaa na sisi makabwela wa uswahilini, akiomba tumpigie kura ETI apewe rungu kamili ili yeye na genge lake la maharamia wachote vizuri kwa uhuru wanaoutaka.
 
Ha ha eti tarehe 26 atakuwa tandale kubeba magunia. Kwi kwi kwi
 
Tatizo we ni mgeni wa siasa, duniani kote ndo siasa zilivyo, wakati wa kampeni ndo wakati wa wansiasa kuwabeba watoto wadogo, kunywa bia na raia mtaani n.k kwa hiyo usione ni jambo geni
 
Mimi nadhani MSANII huyu angaaenza na wamasaki wenzie kabla ya kuja kwa wananchi wa kawaida

Mtanzania wa Leo asiye lofa sidhani Kama anaweza kudanganyika kwa bei kirahisi hivi.

Tangu nizaliwe sijawahi kumuona Mh Lowassa amekuja mbagala Au gogo la mboto ila Leo kaja , mwenye picha YAKE aiweke hapa .

Tangu nizaliwe sijawahi kumuona Mh Lowassa akiwa katika Gari ambayo sio tinted Leo katembea na daladala . mpeni na jembe akalime pia basi .

Tangu nizaliwe sijawahi kumuona Mh Lowassa akipiga stories na watu wa kawaida , Leo urafiki huu wa miezi miwili unatoka wapi?

Kulikoni Leo? Kulikoni mtu mfalume aache kasiri lake Masaki aje mbagala ? Kulikoni mtu anaye tembelea v8, karibia nusu ya mda tinao mjua sisi leo atembelee dalala Kama sio maigizo na kuwadharau watembea kwa usafiri huu?
Kulikoni mtu tunaye mjua katika msafara wake ni wa ma vx na V8 Leo ajitese hivi?
Kulikoni hasa?

MTU amekuwa Waziri , tena Waziri wa offisi ya mazingira na kupambana Na umasikini chini ya makamu wa Rais hakuwahi kufika nadhani aliwahi kuwa anapaona kwenye TV , kulikoni Leo ndo awe jamaa yetu ghafla hivi? Amekuwa Waziri mkuu , Waziri wa MAJI aliwahi kuja? Kulikoni?

Mimi nadhani nadhani ana wadharau Sana tena Sana muulizeni alikuwa wapi?

Kuna watu nawaona wana lia lia eti kwa nini tunamjadili Mh Lowassa , jamani hapa anaye tafutwa ni Rais wa nchi yetu sote , hivyo ni haki na wajibu wa kila rai kiwajadili viongozi hawa na kwa wakati huu ni ajenda.

Wageni wa siasa mtuwie radhi kwa hili , nenda duniani kote nje ya ajenda ya ilani wagombea ni ajenda pia
Ninacho weza kusema ukisikia wanao lia lia asijadiliwe mgombea wao Au ni wageni katika siasa Au mgombea wao ana Makonda konda hawataki wananchi wayajua kwa mgongo huo .

Safari hii Tanzania imepata msanii Na Dr wa physician Na chemistry kufika October tutaona Mengi Sana
Eti wa naenda kutafuta simpathy ya kuwa wameitw lofa .

Ukiwa RAIA unaye jitambua na ukadanganywa na pipi Kama hizi ili utoe kura wewe ni lofa tu hata wazunguke dunia nzima ni lofa .

Maghufuli tuna lala nae kwenye madaraja, tunakesha nae kwenye Barabara wakati wa mvua Masikini, tunakula nae chakula cha mama ntilie .Hana haja ya kufanya mbwembwe Kama hizo , daladala amepanda Mara kibao ili kushutukiza watendaji kazini .

Alfu unasemaje Ni mkutano wa ghafla mna vipaza sauti navyo means Vya ghafla?

Nakumbuka wapinzani ndio walioanza kuona usanii wa msee wa kuwa watu wa naenda kumshawishi mnakuta viti na vipaza sauti tiyari?

Leo naona wameamua kujiunga sasa kutengeneza movie .

Sisi sio malofa kataa kudanganyika.

Maneno mengi ya nini mkuu? tukutane October 25, kwa sasa mambo ni mengi sana. haina haja ya kujifanya unajua sana, maana wenye kujua la kufanya na wenye maamuzi ni watz!
 
Jana pale s'wanga magufuri alisema ktk kampeni atatumia usafiri wa magari badala ya helkopta ili kuona changamoto za wananchi.je,na huyu ni msanii?
 
Tunasema ni usanii kwa sababu tujiulize,amekuwa kiongozi kwa muda zaidi ya miaka 20 alikuwa wapi siku zote kutembelea hao walalahoi anaodai, au wakati akiwa waziri mkuu shida hizo hazikuwepo,kama Mtanzania mzalendo unapaswa kutafakri hilo na si kufurahia hayo maigizo.

Mbona alivyokuwa waziri kawasuprise sana watu ile vaapu huyo Lowassa, sasa yeye mbunge wa Monduli ataenda vipi kushughulikia matatizo ya gongo la mboto dar. Tumia akili yako vizuri, kwa sasa anaenda kuhold nchi lazima vitu kama hivyo avifanye kwa mtu aliekomaa na anaelewa nini anatakiwa kuwafanyia wananchi wake. Uliza Jimboni kwake kafanya nn ndo urudi tena
 
1. Kujenga barabara sita kutoka Morogoro hadi Dar
2. Kila kijiji kitapewa milioni 50
3. Itaundwa Mahakama ya mafisadi (si utawafunga ccm wote pamoja na magufuli)
4. Atafufua viwanda vyote
5. Blaaa blaa blaaaaa

Sasa kama huu siyo usaniii ni Nini? Magufuli Alikua wapi miaka 20 aliyoku madarakani asiyefanye? ccm kwa miaka 54 wameshindwa kufanya sasa watawezaje kufanya kwa miaka 5? Si akajiunge na King Majuto !!!
 
Jana pale s'wanga magufuri alisema ktk kampeni atatumia usafiri wa magari badala ya helkopta ili kuona changamoto za wananchi.je,na huyu ni msanii?

Mkuu kwa afya ile ya EL kuchanja mbuga kwa gari si kwamba hataki ila atazua balaaa hawezi thubutu
 
Tatizo we ni mgeni wa siasa, duniani kote ndo siasa zilivyo, wakati wa kampeni ndo wakati wa wansiasa kuwabeba watoto wadogo, kunywa bia na raia mtaani n.k kwa hiyo usione ni jambo geni

Mkuu haya mambo anayo yafanya EL kuigiza uhalisia wa walalahoi wa mtz ni kiiini macho,kuna watz huku mashambani hawana vyoo na maisha yanasonga mbele,sasa huu uigizaji huu bavicha sio mnapiga mokofi kwenye kila!
 
Usituletee akili zako za kuganda hapa. Kinaochokuuma ni nini kama humpigii kura huyo jamaa... Acha ushabiki wako wa kipuuzi kama wewe ni ccm nenda na magufuli wako huko..... Soma hii uelewe "They wiil disqualify you for the little weaknesses you have and they will never glorify you for the great strength you have shown". Alichokifanya lowassa ni kitu cha msingi sana na kimevuta tension ya watanzania wengi. Angefanya magufuli ungeleta umbea wako? Kama kweli wewe ni mchambuaji wa kweli mbona hujazungumzia usanii aliofanya samia suluhu juzi kwenya msafara? Eti wananchi hasa akina mama walizuia msafara wakitaka aongee japo neno ili msafara uendeleee.....
 
Back
Top Bottom