gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,323
- 3,378
Hivi ndugu yangu una ubongo kweli wewe?! au una tunda la ubuyu tu hapo kichwani?! Kina kushangaza nini hasa huyo jamaa kwenda kujichanganya na wananchi katika kipindi hiki?! Huu ndio muda wake, kipindi cha uchaguzi, watu wanafanya nini katika kipindi cha uchaguzi? Sio kunadi tu sera za chama isipokuwa na kuyasikiliza matatizo ya wananchi, si rahisi huyu jamaa kuyafanya anayoyafanya akichukua ofisi ila atleast ataingia kule akiwa na picha halisi ya nini kipo mtaani.
Tuache kuendekeza siasa za kipuuzi za kupondana na kukashifiana kila mara. Ifike pahala watanzania tutulize vichwa na kuanza critical judgment ya mambo ya msingi na tusiendeshwe na mihemko ya kisiasa.
Watanzania tunateseka sana! Maisha magumu, hatuhitaji ilani ya chama ili tuendelee (huu ni mtazamo wangu) maana for the last 53 years ilani ya chama imetusogeza mbele kuelekea maendeleo ni kama kilomita 1 hivi kwa safari ya kilomita 10000, naomba nitoe rai, tusipoteze muda mwingi kutafuta ya kukosoa tu kutoka kwa hawa wagombea, tuyatafute na mazuri pia. Aluchokifanya Lowassa ni kitu kizuri, si busara! Kuja na kuanza kumpaka tope! After all, huu ndio muda wake muafaka!
Mimi ni mtanzania ambaye niko huru ni vifungo vya kisiasa!
Yani mpaka unatia huruma,DNA imebaini jamaa anachembechembe za ufisadi kwenye damu,hata ujieleze vp mwalimu nyerere alishawahi sema hatuwezi kabidhi mbwa nchi