Usaliti wa Dkt. Slaa ni upi?

Usaliti wa Dkt. Slaa ni upi?

Lowassa anakuja Chadema unampokea na kuwa pamoja naye na unaendelea kuwa mwana chadema.
Lowassa anapewa nafasi ya kugombea Urais unakataa na kuikataa chadema, TATIZO NI LOWASSA AU KITI CHA URAIS?

Ni Urais mama anautaka u-first lady halafu unayeyuka hivi hivi tu
 
Itawachukua muda mrefu sana hawa ndugu zetu kutambua hili na kukubali upekee wa mchango wa Dkt. Slaa katika kujenga upinzani. Sasa hivi wamekuwa kama kondoo wasio na mchungaji!

Upinzani ni misingi, kama leo hii upinzani hauna misingi basi tambua misingi iliyojengwa ni dhaifu ndio maana haikudumu.
Upinzani sio lazima uwe CDM au ukawa, hata ukiwa TADEA unaweza kuwa mpinzani tu na hiyo misingi unaweza kuijenga pia ukiwa huko na watu wanaokuamini watakufuata huko na hatimaye TADEA itakuwa na nguvu zaidi ya CCM au CDM.

Dr Slaa amesaliti harakati zake mwenyewe...
 
Kumbuka tu 2010 Chadema ilisimama peke yake, halafu 2015 viliungana vyama vingapi.?

Ukitaka kujua mchango wa Dr Slaa Nenda kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa 2014......hapo ndio utajua hata kura na mafanikio ya 2015 mizizi ni 2014.

Huyo Lowasa amekuja kwenye shamba ambalo tayari limeshalimwa.
Na mkulima wa shamba alikuwa Dr Slaa na CDM wanalijua ilo ila wameamua kufa na mzoga wao(Lowassa)
 
ni lazima ujiulize kwa kulinganisha asilimia... Dkt. Slaa kulinganisha na Kikwete alipata asilimia ngapi za kura kulinganisha na alizopata Lowassa kwa Magufuli?
Na akumbuke Dr Slaa lilikuwa jeshi la mtu mmoja lakini Lowassa alipewa nguvu na UKAWA.

Je Dr Slaa angekuwa na nguvu ya UKAWA?
 
Slaa kichwa hataki ufisadi kwa dhati hayumbishwi aliposema lowasa fisadi alimaanisha lowasa alipokuja cdm ilikuwa lazima aondoke hawezi kukaa na fisadi hana usaliti kwa sasa anarudi ccm kwakuwa fisadi kaondoka ccm yeye anaweza kaa ccm sasa ni safi kwake sio kwa wengine wote
 
kuondoa utata ,ungeweka video clip ili tujionee kinachoendelea. kwa picha hii nina wasiwasi huo mkono umekuwafotoshopudi si kwa mikunjokunjo ile.
picha ni real....kama sio real aje slaa humu aikatae sababu yumo humu
 
Yaani jamaa akili kubwa kweli kweli
d06777c9-4a07-4ef9-9ce1-bdc6202508b9-jpeg.672363
 
Nimekuwa nikisoma soma humu tokea 2015 kutoka kwa baadhi ya watu kuwa eti aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho mwaka 2010, Dkt. Wilbroad Slaa ni msaliti.

Eti ni msaliti kwa sababu aliamua kuachana na siasa baada ya CHADEMA kuamua kubadili gia angani. Pia, baada ya kuachana na siasa akakataa pia kumuunga mkono mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa.

Sioni kabisa usaliti wa Dkt. Slaa hapo. Ninachokiona ni mtu mwenye msimamo na uadilifu na anayeongozwa na kanuni.

Hivi kweli kabisa mtu na akili yako timamu, kati ya Slaa na CHADEMA, unaweza kumwona Slaa ndiye msaliti?

Kama kuna msaliti basi msaliti huyo ni CHADEMA na si Dkt. Slaa.

CHADEMA walisaliti karibu kila kitu walichokipigania wakiongozwa na Dkt. Slaa. Ni CHADEMA ndiyo waliobadilika. CHADEMA ndiyo wasaliti.

Nyie wote mnaodiriki kumuita Dkt. Slaa kuwa ni msaliti ni vifuu tundu msiojielewa kabisa.
Umetoka kwenye ban na huu utumbo...Jamaa umeshaachaga kupiga picha ukiwa umesimama juu ya meza?
 
Kama hii picha isingekuwepo Slaa angetudanganya mengi. Tunajua kuwa Slaa aliwekwa kati na Josephine Mushumbusi Delillah na alichezea kipigo usiku kucha hadi akalala kwenye kibanda. Kesho yake akafungiwa ndani ya geti na hakuna kutoka. Hapo ilibidi Slaa asalimu tu amri. Tuliokuwa tukienda kwake tuliujua ukweli baada ya mlinzi kuanika kila kitu!
 
Lakini ndiye aliyempeleka CDM,tafuta Video zake za alivyoifanya ile press conference ya kwanza pale Serena.Kumbula Lowassa na Dr.Slaa wote hawa walikuwa wanaunganishwa na Gwajima ambaye kwake Dr.Slaa alikuwa Baba wa Kiroho.

Na muda aliomtambulisha Gwajima kama Baba yake wa Kiroho nilimdharau pale pale,maana Dr.Slaa aliwahi kuwa Padre na anaelewa vyema Baba wa Kiroho ni nani ilinishangaza,na sitoshangaa hata akija kusema hakuongea hivyo pale Serena.Nilimsikia kwa masikio yangu na nikamuona kwa macho yangu,tuache unafiki Dr.SLaa aikane kwanza ile Press Conference ndipo nitamuelewa
Acha kabisa nguvu ya Josephine Mushumbusi Delillah
 
Itawachukua muda mrefu sana hawa ndugu zetu kutambua hili na kukubali upekee wa mchango wa Dkt. Slaa katika kujenga upinzani. Sasa hivi wamekuwa kama kondoo wasio na mchungaji!

Hili nakubaliana na wewe kwa Asilimia 100%

Hata ukiangalia CHADEMA iliaminika sana na wasomi wengi na viongozi wa kidola kwasababu ya Dr.W.Slaa.

Dr. Slaa kama mwanadamu anaweza akawa na hasira sana na CHADEMA hata mimi ningeumia sana sanaaa:

Yaani tuujenge upinzani kwa nguvu vile, tuhatarishe maisha lakini mwishowe wakafanya vitu nyuma ya Mgongo wake.

NB: Ukimsikiliza Dr.Slaa utagundua kwamba alikuwa hataki Uraisi, lakini kilichomuumiza sana ni kwanini wafanye vitu nyuma ya mgongo wake ?? Hata mimi kama mwanadamu ningeumia kabisa.

Zitto Kabwa alikuwa na nguvu kubwa sanaa ndani ya CHADEMA lakini alivyoondoka chama hakikuyumba sana, lakini ondoka ya huyu Mzee ilinifanya hata mimi niliyekuwa nawapenda sana CHADEMA kutowaamini tena.! (Kibaya wao hawataki kukubali haya makosa)
 
Slaa hajabadilika.

Alimkataa Lowassa wakati Lowassa yupo CCM na akamkataa alipoenda CHADEMA.

Huyo ni mtu mwenye msimamo. Mtu mwenye kanuni.

Sioni kabisa usaliti wake.
Slaa ndiye aliyempeleka Lowasa Chadema ........ ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuongea naye na kumkaribisha kwa masharti!!

Kama Slaa angekataa toka mwanzo kuongea na Lowasa kupitia yule Mshenga, huenda yote haya yasingetokea!!
 
Mbowe na Lowassa Nani msaliti?

Mbowe kawasaliti watanzania wapinzani waliokuwa wameujenga upinzani Kwa Hali na mali,

CCM mafail yote ya Lowassa wanayo na Lowassa ni mnyonge, kuna mengi hayasemi kuwahadaa watu,

Ila mbowe msaliti
Kuna maneno mawili siku hizi yanatumiwa vibaya, neno "usaliti" na neno "uzalendo". Inavyoonyesha utafikia wakati watoto watakaopata divisheni 0 au kushindwa mtihani wataitwa wasaliti na kuwa sio wazalendo. Waheshimiwa Wilbroad Slaa na Mbowe, hawawezi kuwa wasaliti kwa chama cha CHADEMA. Ninaamini pasina shaka kuwa Mhe. Mbowe alitupa karata vibaya hajatusaliti, tulishindwa mchezo lakini hakutuuza. Naamini vile vile Dr. Slaa hajatusaliti hata kidogo kwa lolote. Halazimishwi kuunga mkono kile anachoamini sio sahihi. Kwangu mimi ni uzalendo wake kwa taifa uliomfanya afyanye alichokifanya.

Wote wawili ni wazalendo kila mmoja kwa wakati wake na kwa mtazamo wake.
 
picha ni real....kama sio real aje slaa humu aikatae sababu yumo humu
Utetezi wako haujitoshelezi. Na akija akakanusha nina uhakika kwa asilimia zote hutakubaliana naye, kwani aliwauliza swali kuwa mtu fulani ni asset ama lialibility kwa chama, mkajibu kwa nguvu zote kuwa ni asset, naye akaona sasa hicho chama kinaanza kufanya mambo ya kubebe choo na kukileta sebuleni akaamua ku'sepa'!
 
Nimekuwa nikisoma soma humu tokea 2015 kutoka kwa baadhi ya watu kuwa eti aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho mwaka 2010, Dkt. Wilbroad Slaa ni msaliti.

Eti ni msaliti kwa sababu aliamua kuachana na siasa baada ya CHADEMA kuamua kubadili gia angani. Pia, baada ya kuachana na siasa akakataa pia kumuunga mkono mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa.

Sioni kabisa usaliti wa Dkt. Slaa hapo. Ninachokiona ni mtu mwenye msimamo na uadilifu na anayeongozwa na kanuni.

Hivi kweli kabisa mtu na akili yako timamu, kati ya Slaa na CHADEMA, unaweza kumwona Slaa ndiye msaliti?

Kama kuna msaliti basi msaliti huyo ni CHADEMA na si Dkt. Slaa.

CHADEMA walisaliti karibu kila kitu walichokipigania wakiongozwa na Dkt. Slaa. Ni CHADEMA ndiyo waliobadilika. CHADEMA ndiyo wasaliti.

Nyie wote mnaodiriki kumuita Dkt. Slaa kuwa ni msaliti ni vifuu tundu msiojielewa kabisa.
Asante sana kwa makala nzuri
 
Thanks brother for sharing this; sitashangaa mleta uzi akijifanya hi picha hajaiona.
Kwa mujibu wa Chadema mtu aliyefanikisha deal la kumleta Lowassa kwenye kundi lao ni huyu huyu Dr. Slaa, uthibitisho tunaupata kupitia maneno yake mwenyewe na Tundu Lissu.

Wakati wa kampeni, Dr alihojiwa na Television Fulani na miongoni mwa mambo aliyasema ni kwamba "tumeleta choo sebuleni" but akasema mshenga aliyesababisha Lowassa kuja Chadema ni Askofu Gwajima, Lissu alimjibu hivi;

Kama askofu Gwajima alikua mshenga, Dr amtaje mchumbiaji na akatwambia mchumbiaji alikua ni yeye Dr. Slaa na ndiye aliyemtafuta mshenga, maneno hayo ya Lissu Dr hajawahi kuyakana hata mara moja. Hope utakua umejua sasa kwanini Dr anaitwa msaliti
 
Slaa kichwa hataki ufisadi kwa dhati hayumbishwi aliposema lowasa fisadi alimaanisha lowasa alipokuja cdm ilikuwa lazima aondoke hawezi kukaa na fisadi hana usaliti kwa sasa anarudi ccm kwakuwa fisadi kaondoka ccm yeye anaweza kaa ccm sasa ni safi kwake sio kwa wengine wote

Moja kati ya mambo yanayo ifanya ccm ipendwe sana na Watanzania ni UJINGA, ujinga sio tusi bali ni either kutokujua kitu au kukijua kitu nusu nusu; kwani nani aliyefanikisha Lowassa kwenda Chadema/Ukawa!? Muulize vizuri Dr. Slaa atakwambia.

Leo anaweza kusema hayo anayo yasema kwasababu ya UJINGA wetu wa kupoteza kumbukumbu za mambo ya juzi tu; sipati picha miaka 10-20 ijayo jinsi gani picha hi itakavyo geuzwa na uongo kuhubiriwa sana kua kama ukweli. The bottom line is, Slaa ndiye aliyefanikisha Lowassa kwenda Chadema, Mbowe kama mwenyekiti ilikua lazima asimame na kutetea kile walicho kubaliana kwa pamoja.

Hivi sio Dr. Slaa aliyetaja majina ya mafisadi wakubwa kwa mara ya pili pale Tabora na jina la mhe aliliweka!? Sio huyu huyu Slaa!???? Halafu tena yeye huyu huyu anamsifia; kweli Watanzania aliye tuloga aliisha kufa na kaburi lake lilipelekwa na maji ya Elinino so hatuwezi hata kwenda kutambika!!
 
Back
Top Bottom