Nyani Ngabu Mimi binafsi nina tatizo kubwa sana na Dkt. Slaa. Nakubaliana kwamba CHADEMA walifanya kosa kubwa la kimkakati, kwa maslahi ya muda mfupi, kumpokea na kumpa kifimbo cha kugombea Urais, Edward Lowasa. ijapokuwa pia naweza kuelewa hoja yao, kwamba kwa kuwa na Lowasa kungekuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda urais.
Lakini tukubaliane kwamba lilikuwa kosa kubwa. sasa lakini Dkt. Slaa alifanya nini? kujiondoa CHADEMA inaeleweka, kama response ya mtu makini asiyekubaliana na kilichofanyika. Lakini kilichofuatia, kwenda live kwenye TV na kutumia hoja mbalimbali kuiponda CHADEMA, tena kwa kusaidiwa na CCM, hapo ndiyo simuelewi kabisa Dkt. Slaa.
Inaonekana zoezi lote liliandaliwa na CCM. yeye alikubali kutumika kama chombo cha kuiangamiza CHADEMA. Inaonekana Dkt. Slaa alikasirika, aliumizwa binafsi, na alikusudia kulipa kisasi. aliamua kuiharibu CHADEMA tena kwa nguvu zote, Shock and Awe. Kwa gharama za CCM, na kwa faida ya CCM. Inakuwaje, kosa moja la CHADEMA limfanye ajiunge na chama alichopambana nacho kwa miaka nenda rudi? kwa hiyo kwa kosa hilo la CHADEMA, CCM imekuwa safi?
Na kwa kweli, kwa kuangalia ile TV presence yake pale Clouds TV, unaweza kuona kwamba amebaba madhambi yote ya CCM. hana cha kukemea kwa nguvu katika CCM isipokuwa katika Upinzani. alifanya kile kinachoitwa "a tactical defence of CCM" alijificha nyuma ya "uchambuzi" , "umakini" lakini kwa uhalisia, alikuwa ni kama kada yoyote wa CCM.
Kuna swali aliulizwa, kuhusu maoni yake kwa shambulio la Tundu Lissu, na hoja kwamba hajatoa pole. Alijibu kwamba kuna mashambulio mengi tu yanafanyika kila mahali, So what? Lakini ni kama mtu anapata taarifa za rafiki yake kupata majanga, halafu hatoi pole. akiulizwa anajibu kwamba wengi tu wanapata majanga, so what. haiwagi hivyo. Slaa na Tundu Lissu wamepigana na kupambana side by side kwa miaka nenda rudi. wamejenga uhusiano mkubwa sana kama udugu vile. makamanda vitani sasa kwa mtu makini kama Slaa, ilikuwa ni jambo jema kuonesha ushirikiano na CHADEMA katika hali hiyo ngumu. kwamba hata kama walitofautiana huko nyuma, lakini bado nia yake ni kuona mapambano ya kudai haki yanaendelea vema, tena siyo Tanzania tu, bali Afrika Mashariki, Afrika na popote duniani.
Ningetarajia hayo kwa mtu wa calibre ya Slaa. lakini mwenyewe amejishusha chini sana. anastahili kuitwa MSALITI. hajaisaliti CHADEMA tu, bali amesaliti mapambano ya kudai haki toka kwa serikali kandamizi. amekuwa mshiriki wa serikali mojawapo katika kukandamiza haki za raia. hiyo ni changeover kubwa sana, eti kwa kisingizio cha CHADEMA kubadili gia angani! Actually, yeye pia amebadili gia angani. kutoka mtetezi wa wanyonge, hadi kuwa comrade in arms na serikali kandamizi. na yeye ndiye aliyefanya mabadiliko makubwa zaidi kuliko hata CHADEMA