Usaliti wa Dkt. Slaa ni upi?

Usaliti wa Dkt. Slaa ni upi?

Nyani Ngabu Mimi binafsi nina tatizo kubwa sana na Dkt. Slaa. Nakubaliana kwamba CHADEMA walifanya kosa kubwa la kimkakati, kwa maslahi ya muda mfupi, kumpokea na kumpa kifimbo cha kugombea Urais, Edward Lowasa. ijapokuwa pia naweza kuelewa hoja yao, kwamba kwa kuwa na Lowasa kungekuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda urais.

Lakini tukubaliane kwamba lilikuwa kosa kubwa. sasa lakini Dkt. Slaa alifanya nini? kujiondoa CHADEMA inaeleweka, kama response ya mtu makini asiyekubaliana na kilichofanyika. Lakini kilichofuatia, kwenda live kwenye TV na kutumia hoja mbalimbali kuiponda CHADEMA, tena kwa kusaidiwa na CCM, hapo ndiyo simuelewi kabisa Dkt. Slaa.

Inaonekana zoezi lote liliandaliwa na CCM. yeye alikubali kutumika kama chombo cha kuiangamiza CHADEMA. Inaonekana Dkt. Slaa alikasirika, aliumizwa binafsi, na alikusudia kulipa kisasi. aliamua kuiharibu CHADEMA tena kwa nguvu zote, Shock and Awe. Kwa gharama za CCM, na kwa faida ya CCM. Inakuwaje, kosa moja la CHADEMA limfanye ajiunge na chama alichopambana nacho kwa miaka nenda rudi? kwa hiyo kwa kosa hilo la CHADEMA, CCM imekuwa safi?

Na kwa kweli, kwa kuangalia ile TV presence yake pale Clouds TV, unaweza kuona kwamba amebaba madhambi yote ya CCM. hana cha kukemea kwa nguvu katika CCM isipokuwa katika Upinzani. alifanya kile kinachoitwa "a tactical defence of CCM" alijificha nyuma ya "uchambuzi" , "umakini" lakini kwa uhalisia, alikuwa ni kama kada yoyote wa CCM.

Kuna swali aliulizwa, kuhusu maoni yake kwa shambulio la Tundu Lissu, na hoja kwamba hajatoa pole. Alijibu kwamba kuna mashambulio mengi tu yanafanyika kila mahali, So what? Lakini ni kama mtu anapata taarifa za rafiki yake kupata majanga, halafu hatoi pole. akiulizwa anajibu kwamba wengi tu wanapata majanga, so what. haiwagi hivyo. Slaa na Tundu Lissu wamepigana na kupambana side by side kwa miaka nenda rudi. wamejenga uhusiano mkubwa sana kama udugu vile. makamanda vitani sasa kwa mtu makini kama Slaa, ilikuwa ni jambo jema kuonesha ushirikiano na CHADEMA katika hali hiyo ngumu. kwamba hata kama walitofautiana huko nyuma, lakini bado nia yake ni kuona mapambano ya kudai haki yanaendelea vema, tena siyo Tanzania tu, bali Afrika Mashariki, Afrika na popote duniani.

Ningetarajia hayo kwa mtu wa calibre ya Slaa. lakini mwenyewe amejishusha chini sana. anastahili kuitwa MSALITI. hajaisaliti CHADEMA tu, bali amesaliti mapambano ya kudai haki toka kwa serikali kandamizi. amekuwa mshiriki wa serikali mojawapo katika kukandamiza haki za raia. hiyo ni changeover kubwa sana, eti kwa kisingizio cha CHADEMA kubadili gia angani! Actually, yeye pia amebadili gia angani. kutoka mtetezi wa wanyonge, hadi kuwa comrade in arms na serikali kandamizi. na yeye ndiye aliyefanya mabadiliko makubwa zaidi kuliko hata CHADEMA
 
Msingi uliojengwa kwa muda mrefu kwa gharama ya damu ya slaa na mkewe ulisalitiwa kwa siku moja tu kwa tamaa ya pesa ama kweli mbowe chadema ni yuda eskarioti!
 
d06777c9-4a07-4ef9-9ce1-bdc6202508b9-jpeg.672363
Kwa hivyo kamanda we ulitaka lowasa alivyokaribishwa kamati kuu cdm hapohapo dr slaa akimbie?!
busara nikumsikiliza huyo mamvi anasera gani, na ndio hapo slaa akawauliza wenzie "je huyu mamvi ni asset au liability" swali ambalo halikujibiwa na bado linaishi hadi leo!!
 
Nimekuwa nikisoma soma humu tokea 2015 kutoka kwa baadhi ya watu kuwa eti aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho mwaka 2010, Dkt. Wilbroad Slaa ni msaliti.

Eti ni msaliti kwa sababu aliamua kuachana na siasa baada ya CHADEMA kuamua kubadili gia angani. Pia, baada ya kuachana na siasa akakataa pia kumuunga mkono mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa.

Sioni kabisa usaliti wa Dkt. Slaa hapo. Ninachokiona ni mtu mwenye msimamo na uadilifu na anayeongozwa na kanuni.

Hivi kweli kabisa mtu na akili yako timamu, kati ya Slaa na CHADEMA, unaweza kumwona Slaa ndiye msaliti?

Kama kuna msaliti basi msaliti huyo ni CHADEMA na si Dkt. Slaa.

CHADEMA walisaliti karibu kila kitu walichokipigania wakiongozwa na Dkt. Slaa. Ni CHADEMA ndiyo waliobadilika. CHADEMA ndiyo wasaliti.

Nyie wote mnaodiriki kumuita Dkt. Slaa kuwa ni msaliti ni vifuu tundu msiojielewa kabisa.
Ccm Hamuwezi mrudisha Dr Slaa ulingoni .mumtumie kuangusha chadema .huu muhogo sumu ulishakuwa rejected
 
Kwanini hii list mmeinyofoa kwenye website yenu toka EL alivyotinga Chadema? Mnajisaliti wenyewe alafu mnasingizia wengine. Kwanini hii list haipo na mkateua mtuhumiwa wenu agombee urais?
Je, hilo (la kuondolewa list) linaondoa hoja kwamba waliotajwa ni mafisadi?
Yes, CHADEMA walifanya big blunder kuji-associate na mtu waliyemtuhumu ni fisadi.
Lakini, hilo haliondoi hoja kwamba hao jamaa ni mafisadi.

Hoja inayonifanya nimwone 'mungu' wako ni mtu asiye na misimamo. Kaondoka CHADEMA kwa kuwa anasema nafsi yake haikutaka kukaa na mtu aliyemtuhumu ni fisadi. Ajabu leo anakaa meza moja na mtu aliyemtuhumu yeye na chama chake ni majizi na mafisadi. Anaenda mbali na hata kukubali kupokea 'cheo' kutoka kwa mtu aliyemtuhumu ni fisadi. Sasa watu wakisema Slaa alikimbia CHADEMA baada ya kukosa nafasi ya kugombea urais, utakataa kweli? Kumbuka Slaa huyuhuyu alikipa chama sharti la kulipwa mshahara wa ubunge alipoombwa kuwa KM fulltime!!
 
Slaa kichwa hataki ufisadi kwa dhati hayumbishwi aliposema lowasa fisadi alimaanisha lowasa alipokuja cdm ilikuwa lazima aondoke hawezi kukaa na fisadi hana usaliti kwa sasa anarudi ccm kwakuwa fisadi kaondoka ccm yeye anaweza kaa ccm sasa ni safi kwake sio kwa wengine wote
Kwenye list of shame na maboresho yake Slaa alitaja wana CCM wengine wakiwemo Kikwete, Mkapa, Magufuli n.k. Sasa hawa watu si bado wapo CCM? Hoja yako haina kichwa wala miguu! Au unamaanisha ni sawa kwa Slaa kukaa na mafisadi CCM, ila siyo sawa kukaa na fisadi CHADEMA?
 
a. Naamini vile vile Dr. Slaa hajatusaliti hata kidogo kwa lolote. Halazimishwi kuunga mkono kile anachoamini sio sahihi. n.

Kumezuka jitihada za kupotosha juu ya kilichotokea. Ila tunashukuru uwepo wa kumbukumbu za kivideo na maandishi. Kama hiyo video inavyoonyesha, Slaa mwenyewe alikiri kushiriki maongezi ya kujadili ujio wa Lowassa CHADEMA. Slaa alienda mbele na kusema alitoa masharti ya Lowassa kufanya kabla ya yeye kukubali ujio wake. Mtu aliye principled, hata nafasi ya kumjadili mtu aliyemtuhumu kuwa ni fisadi asingeipata.

Usaliti wake mkubwa ni yeye kukubali kutumika na CCM katika wakati ambao mapambano yalikuwa yamepamba moto. Kwa kuheshimu harakati zake, angeweza kuondoka chamani, kusubiri uchaguzi uishe na kisha kusema aliyoyasema. Ila yeye kukubali kutumiwa na CCM (kulipiwa gharama za press, kukutana na Mwakyembe n.k.) wakati kama ule, ndiyo sababu ya yeye kuitwa msaliti. Alisaliti harakati alizoshiriki kuzianzisha.
 
Slaa ndiye aliyempeleka Lowasa Chadema ........ ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuongea naye na kumkaribisha kwa masharti!!

Kama Slaa angekataa toka mwanzo kuongea na Lowasa kupitia yule Mshenga, huenda yote haya yasingetokea!!
Ujio wa EL ungekuwa na manufaa kama procedures za mapokezi alizoshauri katibu mkuu zingefanyiwa kazi. Kwanini tunakataa ukweli huu bila hata soni? Hata mimi EL kuja CDM kimkakati bila kumkaribisha hadi chumbani ningeunga mkono ....angalia sasa mnavyokukuruka nae ...
 
Kwahiyo tatizo lilikuwa procedures za ujio ama ni ufisadi wa Lowassa?
 
Hata mi nimekuwa nikojiuliza hilo swali lako. Mi niliwaambia Slaa alikuwa sahihi na kwamba wafuasi wa Chadema walikuwa wakiongozwa na mihemuko zaidi ya logic kutokana na joto la uchaguzi. Nikiwaambia munahitaji mufa kumuelewa Slaa alichowaambia. Ni kwasasa wengi wameliona hilo kulingana na mambo yanavyoenda ndani ya Chadema.

Niliwashangaa watu sana na kuwauliza kwanini hawakumuona Mbowe kama msaliti. Mi.kwa mtizamo wangu niliwaambia mbaya wenu ni Mbowe na siyo Slaa kama mnavyofikiri. Siku zinaenda, na mpaka tufike 2020 ndo wengi watamuelewa Slaa.
 
Ningekubaliana na hoja yako kama Slaa toka day 1 angemkataa Lowassa. Lakini kitendo cha kukubali kumsikiliza, kumjadili na kumpa masharti fulani, kime-nullify hoja yako.
 
Slaa hajabadilika.

Alimkataa Lowassa wakati Lowassa yupo CCM na akamkataa alipoenda CHADEMA.

Huyo ni mtu mwenye msimamo. Mtu mwenye kanuni.

Sioni kabisa usaliti wake.

Vipi msimamo wake wakumtia ndani Magufuli baada yakuuza nyumba za serikali kiholorera na kuhonga vimads upo palepale au ame swap na ubalozi waakiba mkuu??
 
Mimi binafsi namkubali sana Dr slaa, ni gwiji mbobezi kwenye siasa. mwenye msimamo na kuamini anachokiamini, amekipigania sana chama cha chadema. anajua kupangua hoja na kujenga hoja zenye mantiki na ushindani. ni mtu mwenye mtizamo wa mbali na maono.
 
Kweli, ndiyo maana sasa amekubali 'kuhongwa' ubalozi na mtu aliyemtuhumu kuwa ni fisadi, mtu aliye Mwenyekiti wa chama ambacho Slaa alisema kimejaa mafisadi na majizi, kama Kikwete, Mkapa, Magufuli n.k.
 
Kwahiyo tatizo lilikuwa procedures za ujio ama ni ufisadi wa Lowassa?
Tatizo ni ufisadi ndio maana katibu akashauri utaratibu utakaoacha chama salama ....uzi mmeweka wenyewe clip ya Serena ...ipo very clear na Katibu amesema alijiuzuru ndani ya kikao baada ya kuona taratibu zinakiukwa ...kwa utaratibu wa wengi wape au kukataa kuwa sehemu ya maamuzi ndio maana akajiondoa ....very simple facts
 
Mimi kwangu nina mitazamo tofauti ni wengine kuhusu Dr. Slaa. Usipokuwa makini unaweza kumchukulia Slaa kama msaliti. Sikufurahishwa na Slaa alipoondoka cdm, tena kuondoka kwake akakutumia kama sehemu ya kuiumuza cdm kwa faida ya ccm. Ila hata ningekuwa mimi ningechukua maamuzi ambayo yangewashangaza wengi. Slaa alijiandaa kugombea urais cdm, na kweli alistahili hata kama asingeshinda lakini cdm ingebaki na msimamo wake. Lakini ninachomlaumu Slaa mpaka leo, hivi akija mtu kwenye chama chako kwakuwa humpendi ndio unaondoka. Kwangu naamini Slaa aliondoka cdm kwa kuzira baada ya kukosa nafasi aliyokuwa ameshajiandaa kuitumikia, ila kwakuwa cdm nao walifanya kosa kumpokea Lowassa ambaye alikuwa na kashfa, hapo ikawa rahisi Slaa kuhalalisha huko kuzira kwake. Hivyo mpaka sasa kwangu imebaki 50/50 kwamba Slaa aliondoka kwa kukosa nafasi ya kugombea urais, ama aliondoka kwa kutokutaka kubaki kwenye chama ambacho kimempa Lowassa nafasi adhimu ya kugombea urais wakati walimtuhumu kwamba ni fisadi. Yote mawali kwangu inaweza kuwa ni sababu ya Slaa kuondoka cdm.

Kama Slaa ni msaliti ama la, hilo linategemea na utashi wa kila mtu kulingana na uelewa wake na sababu nyingine mbalimbali. Kilichonifanya nianze kumuona Slaa hana maana ni ile sentesi yake ya jana kuhusu Lissu. Kwa kweli Lissu hakumfanyia Slaa sawa wakati kajitoa cdm kwa zile lugha alizokuwa anamtolea, lakini Slaa kama padre mstaafau alipaswa kusahau baadhi ya mambo na kuacha kutoa lugha zitakazoonyesha kwamba yaliyomkuta Lissu ni mambo ya kawaida. Ukiachia mapungufu hayo niliyoyaona kwa Slaa sioni kama ni adui sana wa cdm kulinganisha na mambo mengine yanayoendelea ndani ya cdm kwa sasa.
Watu hawana shukrani.

Mimi najiuliza swali moja vipi dr. Slaa angebaki cdm akiwa katibu mkuu huku akikihujumu chama? Vipi angekubali kubaki huku akiuza siri na mikakati ya cdm kwa ccm?

Nadhani cdm wangeshukru tu dr kwa kukaa pembeni tu.
 
Tatizo ni ufisadi ndio maana katibu akashauri utaratibu utakaoacha chama salama ....uzi mmeweka wenyewe clip ya Serena ...ipo very clear na Katibu amesema alijiuzuru ndani ya kikao baada ya kuona taratibu zinakiukwa ...kwa utaratibu wa wengi wape au kukataa kuwa sehemu ya maamuzi ndio maana akajiondoa ....very simple facts
Kama tatizo lilikuwa ni ufisadi, je hizo taratibu zingefuatwa zingeondoa ufisadi wa Lowassa?
Kama Slaa yupo principled katika vita dhidi ya ufisadi: kwanini alikubali kutoa nafasi ya kumjadili mtu aliyeamini ni mchafu "choo"? Hadi akitoa masharti ya kukubali ujio wa Lowassa. Lakini swali ambalo nyiye fanatics wa Slaa hamjawahi kulijibu ni kwamba, taratibu zingefuatwa na Lowassa angezingatia masharti, je, ufisadi wake ungefutika?
 
Ujio wa EL ungekuwa na manufaa kama procedures za mapokezi alizoshauri katibu mkuu zingefanyiwa kazi. Kwanini tunakataa ukweli huu bila hata soni? Hata mimi EL kuja CDM kimkakati bila kumkaribisha hadi chumbani ningeunga mkono ....angalia sasa mnavyokukuruka nae ...
First of all mimi siyo CDM ..... ninacomment tu!!

Kwa mtazamo wangu, Lowasa, hakutakiwa kukaribishwa CDM kabisa, whether kwa masharti au bila masharti. The whole thing was miscalculated!!
 
Kama tatizo lilikuwa ni ufisadi, je hizo taratibu zingefuatwa zingeondoa ufisadi wa Lowassa?
Kama Slaa yupo principled katika vita dhidi ya ufisadi: kwanini alikubali kutoa nafasi ya kumjadili mtu aliyeamini ni mchafu "choo"? Hadi akitoa masharti ya kukubali ujio wa Lowassa. Lakini swali ambalo nyiye fanatics wa Slaa hamjawahi kulijibu ni kwamba, taratibu zingefuatwa na Lowassa angezingatia masharti, je, ufisadi wake ungefutika?
Shortly nyie ni propagandist mnajifanya hamuelewi. Sikiliza hiyo clip uliyoweka Dr Slaa kaeleza kila kitu. I believe unajua ukweli ....sihitaji kuelezea jambo tulilokwishajadili sana ...
 
Yuda alimuuza Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.
Hiyo ndiyo maana halisi ya usaliti.
 
Back
Top Bottom