Mkuu tindo ni kweli. Amesema kweli tupu. Wewe ni miongoni mwa watu ambao mpo objective na constructive. Dr Slaa wa leo sio yule wa 2015.Mimi kwangu nina mitazamo tofauti ni wengine kuhusu Dr. Slaa. Usipokuwa makini unaweza kumchukulia Slaa kama msaliti. Sikufurahishwa na Slaa alipoondoka cdm, tena kuondoka kwake akakutumia kama sehemu ya kuiumuza cdm kwa faida ya ccm. Ila hata ningekuwa mimi ningechukua maamuzi ambayo yangewashangaza wengi. Slaa alijiandaa kugombea urais cdm, na kweli alistahili hata kama asingeshinda lakini cdm ingebaki na msimamo wake. Lakini ninachomlaumu Slaa mpaka leo, hivi akija mtu kwenye chama chako kwakuwa humpendi ndio unaondoka. Kwangu naamini Slaa aliondoka cdm kwa kuzira baada ya kukosa nafasi aliyokuwa ameshajiandaa kuitumikia, ila kwakuwa cdm nao walifanya kosa kumpokea Lowassa ambaye alikuwa na kashfa, hapo ikawa rahisi Slaa kuhalalisha huko kuzira kwake. Hivyo mpaka sasa kwangu imebaki 50/50 kwamba Slaa aliondoka kwa kukosa nafasi ya kugombea urais, ama aliondoka kwa kutokutaka kubaki kwenye chama ambacho kimempa Lowassa nafasi adhimu ya kugombea urais wakati walimtuhumu kwamba ni fisadi. Yote mawali kwangu inaweza kuwa ni sababu ya Slaa kuondoka cdm.
Kama Slaa ni msaliti ama la, hilo linategemea na utashi wa kila mtu kulingana na uelewa wake na sababu nyingine mbalimbali. Kilichonifanya nianze kumuona Slaa hana maana ni ile sentesi yake ya jana kuhusu Lissu. Kwa kweli Lissu hakumfanyia Slaa sawa wakati kajitoa cdm kwa zile lugha alizokuwa anamtolea, lakini Slaa kama padre mstaafau alipaswa kusahau baadhi ya mambo na kuacha kutoa lugha zitakazoonyesha kwamba yaliyomkuta Lissu ni mambo ya kawaida. Ukiachia mapungufu hayo niliyoyaona kwa Slaa sioni kama ni adui sana wa cdm kulinganisha na mambo mengine yanayoendelea ndani ya cdm kwa sasa.
Jiulize amepewa masharti gani hata asitoe pole ya mdomo tu kwa madhila yaliyomkuta Lissu.
Je tuamini sasa kuwa na yeye ana visasi?!