Usaliti unauma

Usaliti unauma

Kuna kitu kwa upande wako hujasimulia hasa responds zako alipokua hapokei cm
 
Huyo wa kwako amechelewa kubadilika tena nampongeza kidogo.

Mabinti wa siku hizi akihama tu wilaya achilia mbali mkoa, anakuwa sio wako tena
Dah mwenyew she wangu alihama mkoa akaend jiji chafu dsm cjuh nilipgw kibuti kimoja hatar xana nikasema apa wanaum wa dar washafany yao
 
Jifunze ya kuwa mwanamke akiamua kukubadilikia au kulipiza kisasi hata shetani hukaa pembeni ili ajifunze kitu , katika maisha yako tambua ukimsomesha mwanamke ni kama unatoa sadaka usije ukategemea sana kile unachotarajia au mlichopanga. Katika wahanga 65% ya waliowahi kuwa na mahusiano kuanzia utotoni sio wale waliowaoa / kuolewa nao ukubwani japo waliahidiana. hebu fanya utafiti mwingine kama idadi ya asilimia imeongezeka au imeendelea kubaki vile vile
 
Mwaka 2010 niliingia katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja mwanafunzi wa kidato cha 5.
Tulidumu kwa muda mrefu sana kwani alikua akisoma jitegemee sec school nilikua nikimuudumia vitu mbali mbali vya shuluni mfano pesa ya matumizi na kadharika japo Ada ya shule alikua akilipiwa na wanafamilia yake ususani ndugu zake.
Mpaka alipomaliza kidato cha sita tulikua bado wapenzi na nilikua nikimjali kwa kila hali na kumsaidia shida zake kadri ya uwezo wangu.
Mwaka 2012 akajiunga na chuo cha hualimu kwa ngazi ya sekondary ikambidi akakae huko huko Hosteli lakini bado nilikua karibu nae kwa mawasiriano kwani alienda kusomea mkoani mbeya.
Sikusita kumsaidia japo yupo mbali nilikua nikimsaidia mambo mbali mbali ikiwemo pesa ya matumizi na hata nguo pia na n.k.
Mpaka alipo maliza mafunzo yake ya Diploma mwaka 2014 akubaatika kupata ajira ya moja kwa moja hivyo aliludi kukaa nyumbani kwanza kusubili ajira hapo tulikua karibu saanaa na kupanga mipango mingi ya kimaisha sasa na baadae pamoja na tulikubaliana kuja kufunga ndoa.
Mwaka 2016 akabaatika kupata nafasi ya kujiunga na JKT kwa kujitolea na yote hilikua ni kwa juudi zangu kwani nilitafuta mtu wa kumuunganishia si unajua siku hizi ili kupata nafasi JKT ni lazima uwe na mtu wa kukushika mkono hasa wewe wa elimu ya juu.
Akafanikiwa kumaliza mafunzo ya jkt na kupangiwa kambi kwa ajili ya kujitolea kusubili Ajira kwa kuwa ana elimu ya juu akuchelewa kuchukuliwa na JWTZ na kwenda kupitia Kozi ya JWTZ baadae ya kuludi uko na kuapishwa kuwa mwanajeshi rasmi alianza kubadilika kwa upande wangu nilishindwa kuelewa kabisha ni mwaka huu 2018.
Alikua mtu wa tofauti sana simu zangu hapokei kwa wakati msg ajibu yaani niliumia sana.
Nikamuomba tuonane tuongee kwa kina nini tatizo Alichonijibu sikutegemea.
Nilijibiwa hivi....FANYA YAKO NA MIMI NIFANYE YANGU NASHUKURU KWA UKARIMU WAKO NA KUWA MWEMA KWANGU KWA KIPINDI CHOTE AHSANTE.
Niliumia sana sikuelewa ni kwa nini ameamua kunifanyia hivi au labda nimemkosea lakini cha ajabu aliniblock kila koni
Facebook
Whatsapp
Sms
Call
Yaani sikutegemea inauma sana
Nawaombeni wanawake kuweni na huruma pia mkumbuke hutu alio kufanyia mtu.

Mkuu pole sana. Lakini ushauri wangu ni kwamba hebu fanya mpango na wewe ukafungue vitabu kwa kwenda shule Mkuu. Ni muhimu sana. Nenda kasome mkuu.
 
Polee utakuja kumpata mwingine hadi ujiulize mbona ulichelewa kumfahamu. Saivi tulia tu
 
Pole sana ndugu makosa uliyafanya mwenyewe kuruhusu kwenda JKT na Jeshi. Hayo maeneo ni bora uwaachie wenye kwa wenyewe.
 
Ni kwa kuandika haraka haraka tu mkuu

Uwe unapitia kabla ya ku post mkuu. Umahiri wa lugha ni moja kati ya kigezo cha kutambua uelewa wa mtu. Pole sana kwa yaliyo kusibu. Kukua ni hatua. If people can walk away from you... let them walk bro.
 
Uwe unapitia kabla ya ku post mkuu. Umahiri wa lugha ni moja kati ya kigezo cha kutambua uelewa wa mtu. Pole sana kwa yaliyo kusibu. Kukua ni hatua. If people can walk away from you... let them walk bro.
I will never repeat any mistakes
 
Back
Top Bottom