Usaliti unauma

Usaliti unauma

Poole kamanda pengine kawa kwenye kikosi maalum cha usalama akaona kwakuwa anakupenda sana hataweza kufanya kaz kwa usiri unaotakiwa akafanya uamuzi mgumu. Kwa pande zote mbili
 
Mimi nimedumu 7 years kwenye mahusiano lakn mwaka huu ameniacha,simu hapokei wala sms hajibu,nilimgharamia kama wew na sasa ni mwalimu kaniacha,ila sina stress mana nimewapanga balaa
1.Kuna nurse 2
2.Kuna mwalimu 1
3.Mfanyabiashara 1
Jumla 4
Ni dhambi kubwa sana kuwa na mwanamke mmoja hapa duniani
Heheheh aisee, hao wengine wanakuwa kama shock absober?
 
Pole sana rafiki,mwenyewe nilishakumbana na kadhia kama yako,tofauti ni kuwa ilikuwa twende naye wote JKT,lakini mie majina hayakuwa vizuri,hivyo akapata yy nafasi mie nikakosa,mie nikaamua kuendelea na masomo ya juu zaidi.
Mwaka wa mwisho kumaliza chuo ,naye ndio anapata kazi JWTZ,hapo akaanza kunichenjia.
Mie nikasema ,no sweaty,nikaamua pia kumuumiza kisaikolojia..Nikamwambia kuwa nilikuwa sikutaki ndio maana nikakusakizia uende jeshini ili niwe huru kula bata na nimpendaye,maana nilikuwa sikupendi,ila nilikuwa natafuta njia ya kukupiga chini. Alinipigia, nikamchana,sasa ivi analazimisha angalau tupige shoo tu,mie sitaki tena.
Hehehe aisee
 
Nijuavyo wote huwa wanatolewa uraia na kuwa tofauti na aria wa kawaida sasa ni wanawake wachache sana wanaoweza kubaki na ile spirit na kike na kujikubali kama mke wengi huwa wanaharibiwa na mazingira ya kazi zao usikute mngeendelea angekuja akuache baadae sana labda kwa kuona hamuendani kitabia
Hii ni mara ya pili nasikia hii kitu ya kuondolewa uraia, Hii ikoje mkuu?
 
Hii ni mara ya pili nasikia hii kitu ya kuondolewa uraia, Hii ikoje mkuu?
Umewahi sikia kuhusu 6 weeks bila kulala unadhani huwa wanafanya nini huko??kula nyama miaka 2 ya jkt unafikiri dhumuni lake nini??
 
Umewahi sikia kuhusu 6 weeks bila kulala unadhani huwa wanafanya nini huko??kula nyama miaka 2 ya jkt unafikiri dhumuni lake nini??
Duuh aisee ndo kinachofanyika kumbe, ndo maana asilimia kubwa hawana utu wanaishia kutusaliti.
 
Yaan kuna mambo mengine mpaka kuchangia unapata ukakasi! Yaan mke mtarajiwa unamfanyia mpango ajiunge na jeshi alafu useme akili zinakutosha! Labda kwa kuwa hujawahi ishi jeshini? Yaan huyo anapelekwa rest house mara mbili tu tayar ashakusahau. Nimpongeze kwa kujitahidi hata hivo
 
Kuna Dada yangu ni mrembo kishenzi anaolewa soon kila siku ananambia kaka yangu usithubutu kumwamini mwanamke sisi ni noma
 
Poole kamanda pengine kawa kwenye kikosi maalum cha usalama akaona kwakuwa anakupenda sana hataweza kufanya kaz kwa usiri unaotakiwa akafanya uamuzi mgumu. Kwa pande zote mbili
Ahsante aisee ila inanifundisha kitu hii
 
Mwaka 2010 niliingia katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja mwanafunzi wa kidato cha 5.
Tulidumu kwa muda mrefu sana kwani alikua akisoma jitegemee sec school nilikua nikimuudumia vitu mbali mbali vya shuluni mfano pesa ya matumizi na kadharika japo Ada ya shule alikua akilipiwa na wanafamilia yake ususani ndugu zake.
Mpaka alipomaliza kidato cha sita tulikua bado wapenzi na nilikua nikimjali kwa kila hali na kumsaidia shida zake kadri ya uwezo wangu.
Mwaka 2012 akajiunga na chuo cha hualimu kwa ngazi ya sekondary ikambidi akakae huko huko Hosteli lakini bado nilikua karibu nae kwa mawasiriano kwani alienda kusomea mkoani mbeya.
Sikusita kumsaidia japo yupo mbali nilikua nikimsaidia mambo mbali mbali ikiwemo pesa ya matumizi na hata nguo pia na n.k.
Mpaka alipo maliza mafunzo yake ya Diploma mwaka 2014 akubaatika kupata ajira ya moja kwa moja hivyo aliludi kukaa nyumbani kwanza kusubili ajira hapo tulikua karibu saanaa na kupanga mipango mingi ya kimaisha sasa na baadae pamoja na tulikubaliana kuja kufunga ndoa.
Mwaka 2016 akabaatika kupata nafasi ya kujiunga na JKT kwa kujitolea na yote hilikua ni kwa juudi zangu kwani nilitafuta mtu wa kumuunganishia si unajua siku hizi ili kupata nafasi JKT ni lazima uwe na mtu wa kukushika mkono hasa wewe wa elimu ya juu.
Akafanikiwa kumaliza mafunzo ya jkt na kupangiwa kambi kwa ajili ya kujitolea kusubili Ajira kwa kuwa ana elimu ya juu akuchelewa kuchukuliwa na JWTZ na kwenda kupitia Kozi ya JWTZ baadae ya kuludi uko na kuapishwa kuwa mwanajeshi rasmi alianza kubadilika kwa upande wangu nilishindwa kuelewa kabisha ni mwaka huu 2018.
Alikua mtu wa tofauti sana simu zangu hapokei kwa wakati msg ajibu yaani niliumia sana.
Nikamuomba tuonane tuongee kwa kina nini tatizo Alichonijibu sikutegemea.
Nilijibiwa hivi....FANYA YAKO NA MIMI NIFANYE YANGU NASHUKURU KWA UKARIMU WAKO NA KUWA MWEMA KWANGU KWA KIPINDI CHOTE AHSANTE.
Niliumia sana sikuelewa ni kwa nini ameamua kunifanyia hivi au labda nimemkosea lakini cha ajabu aliniblock kila koni
Facebook
Whatsapp
Sms
Call
Yaani sikutegemea inauma sana
Nawaombeni wanawake kuweni na huruma pia mkumbuke hutu alio kufanyia mtu.
Ukiona mwanamke anakusikiliza ujue anatatizo tatizo hilo likiondoka hatakusikiliza tena...
 
Pole sana mkuu, kuna sehemu kwenye biblia wameandika "nyumba na magari hurithiwa kutoka kwa wazazi, ila mke mwema hutoka kwa bwana" pia kuna sehemu nyingine wakataja sifa za huyo mke mwema "mke mwema ni nani aliyemwona......" unaweza fuatilia zaidi. Kwa hiyo mke mwema ni kama tunu, au zawadi ambayo unaipata toka kwa Mungu. Probably, vinginevyo ni kucheza kamari, kuna wengine wanasema unakuwa nao zaidi ya mmoja kama jamaa alivyo comment hapo ili usiumie sana endapo mmoja atakusaliti. Tatizo linakuja, huenda aliyeondoka ndo ulikuwa unampenda zaidi ya wote. Kwa hiyo utaona shida inabaki palepale.
 
Back
Top Bottom