Wana JF,
Tanzania 1 ametamka neno lisilotamkika ambalo naamini lina mkono mkubwa tu katika masoo yote. Wahenga walisema "mafahali wawili hakai zizi moja". Hilo ni kweli, lakini hata kama kuna zaidi ya fahali moja, basi mmoja wao ndio atakuwa Fahali Mkuu.
Binafsi naona kuwa kiinimacho kinachoendelea kila siku ni danganya toto ya kuficha ukweli mkubwa. Usiri ni jambo ambalo limemtawala Fahali Mkubwa na huwa ni mwerevu na katili kupindukia pale inapobidi kulinda usiri. Wakati mwingine usiri huo haufichwi kwani mazingaombwe yake yanakufanya usione kitu kilicho hadharani.
Kitu kikubwa cha kujua kuhusu Fahali Mkubwa ni kwamba, size does not matter. Kama mafahali wadogo wamenona na kuwa na nguvu mbalimbali (nguvu za mwili, pembe ndefu, mbio,etc)bado atakuwa anamheshimu na kumsikiliza Fahali Mkuu. Wakati mwingine Fahali Mkuu anaweza kuruhusu mafahali wengine "waendeshe boma" huku yeye akiwa pembeni lakini wote wanajua nani zaidi.
Unaweza kujiuliza kwa nini nazungumzia mambo ya mafahali na Fahali Mkuu. Kwa jinsi mambo yanavyoendelea, ninapata nadharia kuwa ufisadi wote unaoendelea ni kazi ya mafahali chini ya Fahali wao Mkuu. Mtandao wa mafisadi ni mkubwa sana na wakutisha. Fisadi mmoja, JP, anasemekana ameshawahi kuua (yeye binafsi) watu kadhaa waliopita kwenye anga zake. Katika boma hili la ufisadi, kumtosa kafahali kamoja ili kulinda mafahali wengine hususan Fahali Mkuu ni jambo dogo sana. Chukua mfano wa gavana mtenguliwa, Ballali. Ninahisi alikuwa katika kundi la mafahali bila kujijua kuwa anatumiwa. Aliletwa na BWM ambaye nafikiri ni fahali ingawa si mkuu. Lakini gavana mtenguliwa kwa sasa anatambua jinsi alivyochezewa na mafahali wengine (wamo hata kwenye TISS ya usalama...hawa wako kila kona, mahakamani, polisi, you name it)na sasa anacheza karata. Siamini kweli gavana mtenguliwa anakaa chini akifurahia shutuma za ufisadi zinazoletwa kwake kila kukicha na kukaa bila kujitetea. Pia kitendo cha kujiuzulu kwake kukanwa na Ikulu kumempa picha mpya. Naamini huyu bwana anataka kuwa makini ili kwamba akijitetea, ajitee kwa kutoa ukweli wote na watu wote wasikie. Pia, anataka ajiandae kwa kile kinachoweza kumpata pale atakapotoboa siri. Mafahali hawapendi siri zao zitoke kama nilivyosema awali na watafanya chochote wawezacho chini ya anga kuzitunza siri hizo.
Basi, na sisi tufanyeje? Tuendelee kuufichua ufisadi na hawa mafahali watapunguza makali kidogo. Cha msingi tusiogope kujitoa mhanga. Namuonea huruma gavana mtenguliwa kwani ametegwa na ni vigumu kujinasua. Kwa upande mwingine mafahali wataendelea kuwa matawi ya juu huko mitaa ya kati ya Ocean na Moringe wakitanua na Road Runners zao.