USAJILI TELEGRAM TATIZO, NAOMBA MSAADA.

Chukua hayo maelezo
elezea sasa umefanikiwaje wengine wapite umo
 
Kizazi cha porn
Hakuna kingine unachoenda kuangalia telegram zaidi ya video za ngono
Usipotoshe bro. Mie na download software na movies ambazo kwa namna moja ama nyingine ningelazimika kuzinunua. Kwa mfano kuna software inaitwa FL Studio, kwa ajili ya music production, premius version subscription ni dola 400, wakati telegram naipata bure pamoja na plugins zake zote.
 
Umepitaje wenzio tunakwama kijana
Ingia PLAY STORE download app inaitwa PLUS MESSENGER kisha download na app inaitwa DeeProxy, baada ya hapo fungua app ya deeproxy ili uunganishe proxy kwenye app ya PLUS na TELEGRAM, kisha fungua PLUS fanya kujisajili, kuna namna hapo itakupeleka telegram, telegram jisajili.... Weka namba, email baada ya hapo watatuma codes na wasipotuma code kuna option ya call watakupigia.
 
Ingia PLAY STORE download app inaitwa PLUS MESSENGER kisha download na app inaitwa DeeProxy
Kuwa makini na hizo app za mod, unaweka namba yako na code ya kuingia kwenye app ambayo haijatoka kwa Telegram wenyewe. Ukishafanikiwa kusajili, hamia Telegram ya kawaida na uwashe Two-Step Verification (Settings > Privacy and Security), ili hata code ikivuja mtu asiweze kuingia kwenye akaunti yako.
 
Mnatishana sana wakuu, Mimi nmemkua mtumiaji wa mod ya Plus Messenger toka 2016 sijawahi pata tatizo, tena kabla hawajaweka feature ya dual accounts nlkua nazitumia zote 2 original na plus ila baada ya hiyo feature walipo ileta nmebaki na Plus tu.... Hamna mtu mwenye akili zake timamu wa kukudukua kama huna manufaa kwake labda wawe wale script kiddies wazee wa kujaribu jaribu mambo..
 
shukran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…