Willy NGOMA
JF-Expert Member
- Feb 25, 2016
- 4,416
- 5,978
Hizi hapa sababu tano kwanini TELEGRAM ni bora kuliko WHATSAPP.
Tunatumia WhatsApp kwa sababu ya mazoea tu ya mtaani, lakini kiufundi, Telegram ipo miaka mia mbele. WhatsApp ni kama usafiri wa umma, lakini Telegram ni mnyama mwingine kabisa.
Mambo yako hivi kifupi doti kwa doti: 👇
1. Cloud Storage: Telegram haijazi Memory ya simu yako hata MB moja; kila kitu kinalindwa kwenye seva zao. Ukibadilisha au kupoteza simu leo, unakuta chat na picha za miaka mitano iliyopita zipo palepale bila kuhitaji dharura ya ku-backup.
2. Kutuma Ma-File ya Makubwa: WhatsApp inaleta pozi ukituma faili kubwa na inakata ubora wa picha. Telegram inakubali kutuma file moja la hadi GB 2 bure! Unaweza kutuma movie nzima ya HD au software kubwa bila kupunguza ubora hata nusu.
3. Ulinzi wa Namba yako: Kwenye WhatsApp, ili uchat na mtu lazima amiliki namba yako ya simu. Telegram unaweza kuficha namba yako isionekane na kiumbe yeyote, kisha ukatumia Username tu kuwasiliana mtaani kwa usalama zaidi.
4. Ma-Group ya Jeshi na Bots: Group la Telegram linachukua hadi watu 200,000 kwa pamoja bila simu yako kukwama. Pia lina "Bots" (wasaidizi wa kidijitali) wanaoweza kukutafutia vitabu feki, kukupakulia nyimbo, au kusimamia magroup kimyakimya.
5. Kufanya Kazi Simu Ikiwa Imezima: Telegram ya kwenye kompyuta inajitegemea 100%. Hata kama simu yako kuu imezima chaji, imepotea, au haina internet, bado unaweza kuendelea kuchat na kufanya kazi kwenye PC yako kama kawaida.
Ukweli ni kwamba Mark Zuckerberg anasubiri Telegram wagundue kitu (kama Channels au kuficha meseji) kisha yeye anakinakili na kukileta WhatsApp kwa mbwembwe. Ukishaijua Telegram, kurudi WhatsApp ni kama kurudi nyuma kiteknolojia!
Kataa kifilimbi
Okoa bolo