Usahihi wa taarifa toka Nkasi

Usahihi wa taarifa toka Nkasi

Ikiwa wewe ambaye hata jiografia ya nchi yako huijui unasemaje mbunge hamuelewi. Yani ukisikia Nkasi unadhani Mbunge ni Ally Kessy pekee, kumbe Nkasi ni wilaya na ina majimbo Mawili, Nkasi Kusini (huko mleta uzi anakozungumzia) na Nkasi Kaskazini kwa Ally Kesy huyo unayemaanisha wewe.

Ku-conclude jambo usilolijua huoni kama kutojielewa pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe ume-conclude Ally kesy umetumia nini kujua kuwa ni huyo kammaanisha!? maana hajataja kuna! au huyo ndiyo mnajua kwamba kichwa yake imeingia Mafuta ya taa.
 
Mkuu wa w. Mtanda Ni mchapkazi mzur Sana tatizo wakat wa kampen hamuwaambii vijana ukwel kua mtakwenda kufanya kazi za songambele mkituchagua. Mnawadanganya
 
Wamejiunga na bando la halichachi la chama cha zamani!
 
Usiamini utetezi wa kujikanyakanyaga kama huu Mkuu. Siku hizi imekuwa staili ya utawala wanajeshi kutumika kwenye operesheni za ndani hasa za kutumia nguvu dhidi ya wananchi kwa kisingizio cha maendeleo. Servive men wanatokaje kambini kwa amri ya Mkuu wa wilaya? Na wakitoka wanakuwa peke yao au na wanajeshi (viongozi wao)? Halafu waliokaidi inatolewa adhabu ya kuruka kichura (adhabu ya kijeshi) dhidi ya raia. Ni punguani tu atakayeamini kichura siyo adhabu ni maelekezo ya kufanya Kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa hiyo inajikanganya kweli, kama kungekuwa na ushahidi wa picha ingekuwa rahisi hata jkt yenyewe kuchukua hatua dhidi ya waliohusika kwa sababu mkuu wa mkoa au wilaya wako kwenye utawala wa kiraia hivyo hawahusiki na mambo ya wanajeshi wala hao servicemen. Kama wananchi waliadhibiwa na servicemen basi malalamiko hayo yanapaswa kupelekwa jeshini. Kwenye shughuli za jeshi DC hana tofauti na hao wananchi maana cheo cha kisiasa hakitambuliki jeshini.
 
Kunywa Pombe gulioni ndio kutafuta pesa? Unaambiwa watu wamekubaliana kushiriki kutatua kero lakini wengine wanaenda kunywa Pombe kana kwamba hiyo hospitali ikikamilika wao hawataitumia wataendelea kupona kwa Pombe! Wacha warushwe kichura chura hata kukwepa ndege, bila watu kushurutishwa tusingekuwa na reli toka Dar hadi kwetu Kigoma.
Umeamua kuegemea upande wako kama kawaida. Hata husumbui akili kutafuta undani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa hiyo inajikanganya kweli, kama kungekuwa na ushahidi wa picha ingekuwa rahisi hata jkt yemyewe kuchukua hatua dhidi ya waliohusika kwa sababu mkuu wa mkoa au wilaya wako kwenye utawala wa kiraia hivyo hawahusiki na mambo ya wanajeshi wala hao servicemen. Kama wananchi waliadhibiwa na servicemen basi malalamiko hayo yanapaswa kupelekwa jeshini. Kwenye shughuli za jeshi DC hana tofauti na hao wananchi maana cheo cha kisiasa hakitambuliki jeshini.
Ushahidi si lazima kuwe na picha kwani wajibu tuhuma wanakiri kuwatumia servicemen. Na hapa walikuwa wanajibu Uzi uliosimamishwa ambao ndio ulioibua sakata hili lakini Mods wakausimamisha na kubakisha huu ulioanzishwa na watetezi. Uzi wa awali ulitoa taarifa ya nini kilichotokea huko mnadani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi tabia za kuwaambia wananchi wajitolee,wakati wanalipa kodi ili kwa niaba serikali ifanye hiyo kazi kwa kutumia wataalamu inaboa sana. Eti kujitolea,hizi zilikuwa zama za ujamaa huko. Kila mtu apambane kwa hali yake,Tulipe kodi serikali iunde miundombinu. Hakuna kuhamisha magoli.
 
Wakuu,

Kuna Uzi umepandishwa jukwaani ukiwa na taarifa kwamba Mkuu wa Wilaya ya Nkasi amewaamuru askari kuwaadhibu wananchi.

Ufafanuzi wa taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Jana, Wananchi, Mbunge na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg Said Mtanda walikubaliana kufanya kazi ya kujenga zahanati ya kijiji iliyokwama kwa takriban miaka 5 huku wananchi wakitembea umbali wa Km 20 kufuata huduma za afya.

Wakati huo huo kwenye kijiji cha Ntuchi (siku ya jana Jumamosi) kulikuwa na mnada ukiendelea hivyo baadhi ya vijana walitajwa kwenda kunywa pombe kinyume na makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja (Songambele).

Askari wa JKT ambao ni mafundi walikuja kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo kwakuwa zana zote ( Mbao, bati, misumari) kwa miaka miwili vimekuwa vikioza.

Vijana waliokuwa wamekwenda mnadani walifuatwa wakaletwa ili kushiriki zoezi hilo (songambele).

Askari waliwaleta wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na waliokaidi walirushwa kichura chura!

Wananchi kwa pamoja wamefurahi kwakuwa kazi iliyopangwa imefanyika.

Mpaka kufikia muda huu ( Leo jumapili 13, August) wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kuendelea kushiriki zoezi hill.

Hakuna wanajeshi waliokuja kushiriki Bali ni service men waliojitokeza kujenga zahati kwa kushirikiana na wananchi.

Pia askari hao hao (service men) walishiriki shughuli za maendeleo katika kijiji cha Kasu.

Mtoa taarifa aliyejitanabaisha kama mwanahabari anapaswa kufuata misingi na weledi wa taaluma ya habari.

Ofisi ya mkuu wa wilaya Nkasi imesikitishwa na taarifa zilizotolewa mtandaoni za upotoshwaji!
Acha zarau nani kakwambia service men sio askari huyo ni askari tofauti inakuja kwenye ajira kwamba yeye hajaajiriwa..

Sasa nakuja kwenye mada yako umesema vizuri na umesahihisha lakni ninavolijua jeshi letu vijana walichezea doso LA kutosha labda ungetuwekea video ya kijana mmoja kati ya waliyofatw mnadani akanushe tungekuelewa


Kajipange na ofisi yako mmekurupuka

acha uongo
 
Serikali imeshindwa jukumu lake inaanza kufukuzana na raia wake. Sasa maana ya kulipa kodi ni nn? Tunaelekea Zimbabwe
 
"Askari waliwaleta wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na waliokaidi walirushwa kichura chura"! sasa mbona kama askari ndo waliowarusha kichurachura pia mtu aliyelewa anaweza kuruka kichurachura kweli?
 
Sasa wewe mleta ufafanuzi hapa ndio umeharibu kabisa. Yaani una kiri kulikuwa na kulazimishwa na kuteswa kwenda kujenga hicho kituo, lakini ukaharibu kwa kuleta ushabiki wa kumtetea mkuu wa wilaya kishamba. Kwa mfano...

1/Yaani taarifa nzima imejichanganya. Mara vijana wamekwenda kunywa pombe, mara watu wamechukuliwa Gulioni, mara Askari (service men!), Mara hawajapigwa lakini wamerushwa vichura chura nk. Ni mchanganyiko kuliko usahihisho.

2/Mleta ufafanuzi hapa husemi wewe ni nani katika ufafanuzi huu. Wewe ni mkuu wa wilaya hiyo? Wewe ni msemaji wake? Wewe ni shuhuda? Wewe ni mleta mada tu lakini una source?

3/Taarifa hii ya ufafanuzi imetolewa na upande wa mkuu wa wilaya ambayo ndio inayodaiwa kutesa watu. Nini maana ya story kuwa balanced?

4/Kama shughuli ilikuwa ni ya kujitolea, kwanini watu wasakwe, warushwe rushwe kichura, wakimbizwe masokoni, Wahukumiwe kwa kwenda kilabuni?

5/Hivi ukaidi ni nini katika tukio hili? Kama suala ni kuombwa kujitolea, na mtu akakataa kujitolea ili aendelee na shughuli zake za kutafuta pesa, kuna kosa gani hapo?
Nani aliyeteswa hapo mkuu?
Kurushwa kichurachura sio adhabu,ni zoezi hilo.
 
Huyo DC anatafuta umaarufu, ambao kwa wafipa utamtokea puani. Kwanza si alikua Mbunge huyu mfuasi wa Lowasa! Hajui amefichwa mahala. Kwanza alisababisha kupoteza jimbo kwa kutotumia akili na busara ktk kutenda na kuamua. Nimtahadharishe, boss wake hapendi watu wake washurutishwe na kuteswa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani aliyeteswa hapo mkuu?
Kurushwa kichurachura sio adhabu,ni zoezi hilo.
Akili za kushikiwa taabu kweli kweli. Yaani kwako mtu akitaka kufanya shughuli ya ujenzi anaanza na kuruka kichura.? Utetezi feki wa aliyekutuma anasema wananchi walikwenda kulewa, unawarushaje kichura walevi kisha uwape Kazi? Halafu kwa nini mnataka kuwafanya Wafipa ni watu Wa ovyo kiasi hicho? Mara muwaambie wanazaa kama panya, Mara ni walevi!! Kama mnaona hawafai kuongozwa na nyie watakatifu ombeni uhamisho muwaache hao walevi mkaongoze watakatifu wenzenu. Manakanusha na kutetea vitendo vya kidhalimu kwa vile tu vimetendwa na mtu mwenye cheo? Aibu gani hii??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena wangewarusha zaidi ya hapo wanategemea maendeleo yaletwe na nani?? Vijana kunywa pombe tu tena muwaongeze na viboko kuruka kichura ni mazoezi tu hayo wala si adhabu.
Akili ndogo huwez kuhukumu kwa kusikiliza upande mmoja ungeenda field ukasikilize wananchi wewe mwenyewe maana hadi sasa habari zinakanganya huki na huyo adrian kaja kufukia mashimo kamanilivyo kawaida ya watanzania.
 
Tatizo watanzania ushabiki mwingi sana, tena vijana wanajifanya wao ni wapinzani wanasahau maendeleo hayana chama. Ilitakiwa viboko sana hawa. MTOTO WA MWAFRIKA BILA KIBOKO HAELEWI KITU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom