Usahihi wa taarifa toka Nkasi

Usahihi wa taarifa toka Nkasi

Kwanza kabisa kuna tatizo kubwa sana huko kuliko huu uiitao ufafanuzi wako...

Pili, hakuna tatizo kabisa watu kushiriki na kuitekeleza mipango yao ya kujiletea maendeleo....

Lakini hili ni lazima lifanyike kwa utaratibu unaoeleweka na kukubalika na kila mmoja ama ingalau na wengi kabisa.... hapa nina maana ya ushirikishwaji wa wananchi huku kila upande ukiwa unajua majukumu na wajibu wake...

Nina maana kwamba, wananchi hao waliorushwa kichura kichura wajue na watekeleze wajibu wao...

Na wakati huo huo serikali nayo itekeleze jukumu na wajibu wake kikamilifu pasipo kutumia ubabe wa kidola kulazimisha mambo kufanyika ambalo ndilo lililofanyika huko...

SASA BASI:

Umesema vifaa vya ujenzi kama mbao, simenti, misumari nondo na vingine vilikuwepo....

Maswali:

1. Tuambie, nani amevileta hivyo vifaa ? Je, ni serikali ama ni michango ya wananchi wenyewe kwa kulazimishwa na mitulinga ?

2. Mgawanyo wa majukumu ulikuwaje ? Kwa maana wananchi wao wafanye nini na nini ilikuwa wajibu wa serikali kama nilivyoeleza hapo juu ?

3. Je, kulikuwa na mpango shirikishi ulioandaliwa na wananchi wote ama kwa wingi wao wakauridhia ya namna kila mmoja ambavyo angeweza kushiriki zoezi la ujenzi la zahanati ya kijiji ?

Kumbuka kuwa haiwezekani iwapo mafundi toka JKT walikuwepo pamoja na vifaa vyote vya ujenzi halafu wakati huohuo utake wananchi wote wa kijiji chote wawe kwenye site ya ujenzi kana kwamba hawana shughuli zao binafsi za kila siku za kujitafutia maendeleo yao binafsi na mlo wao !!

Kwa ufahamu wangu ni kuwa, kama mafundi walikuwepo pamoja na vifaa vyote, wananchi wangeweza kujigawa wenyewe kimakundi mfano kivitongoji kwa ajili ya kwenda kuwasaidia hao mafundi kusogeza tofali, kuchota maji nk huku wengine wakiendelea na shughuli zao kwa amani wakisubiri zamu yao !!

Hili likifanyika, wala huhitaji polisi wa JWTZ ama Mgambo kuwasimamia wananchi hawa bali wao wenyewe watafanya hivyo pamoja na kuchukuliana hatua wao kwa wao kwa ambao hawatajitokeza !!

Lakini kwa kuwa serikali ya Magufuli ni ubabe tu huku wakiwa hawana akili wala maarifa, mpaka wamalize miaka mitano basi, watakuwa wameipata fresh yao !!

Mwisho kwa maelezo yako tu hayo hapo juu, mtu mwenye akili timamu hata kama hakuwepo huko, akisoma atagundua mara moja kuwa hakukuwa na mpango shirikishi uliowajumuisha wananchi wote ktk kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa zahanati bali viongozi wa eneo husika kwa kuwa tu wanatafuta sifa binafsi na kwa kuwa hawakubaliki na kuaminiwa na wananchi wa eneo husika, wametumia nguvu nyingi kuliko elimu ya ushawishi kwa wananchi ili waone umuhimu wa kujitoa ktk jambo ambalo ni la manufaa kwao wenyewe na watoto wao...!!

Ni wazi kulikuwa na makosa mahali fulani (hasa kwa upande wa serikali/wasimamizi) aidha tuwe tunapenda ama hatupendi kuambiwa hili na ni kwa mantiki hii wananchi waliwakatalia na kuamua kuwalazimisha kwa nguvu za kikoloni !!

Kuwarusha rusha kichura wananchi hao ni ujinga na ni kosa la kipumbavu kwa wote walioshiriki kutenda....ipo siku viongozi wa namna hii, watakuja kuwa - push wananchi to the limit na hapo nao watajibu mapigo!!!
 
Naunga mkono hoja vijana wafanye kazi kwa lazima....kama hawataki wapigwe tu.
 
Tena wangewarusha zaidi ya hapo wanategemea maendeleo yaletwe na nani?? Vijana kunywa pombe tu tena muwaongeze na viboko kuruka kichura ni mazoezi tu hayo wala si adhabu.
Tena hawa ni miongoni mwa wanaoshadadia viroba virudi mtaani ili uzembe uongezeke
 
Sasa wewe mleta ufafanuzi hapa ndio umeharibu kabisa. Yaani una kiri kulikuwa na kulazimishwa na kuteswa kwenda kujenga hicho kituo, lakini ukaharibu kwa kuleta ushabiki wa kumtetea mkuu wa wilaya kishamba. Kwa mfano...

1/Yaani taarifa nzima imejichanganya. Mara vijana wamekwenda kunywa pombe, mara watu wamechukuliwa Gulioni, mara Askari (service men!), Mara hawajapigwa lakini wamerushwa vichura chura nk. Ni mchanganyiko kuliko usahihisho.

2/Mleta ufafanuzi hapa husemi wewe ni nani katika ufafanuzi huu. Wewe ni mkuu wa wilaya hiyo? Wewe ni msemaji wake? Wewe ni shuhuda? Wewe ni mleta mada tu lakini una source?

3/Taarifa hii ya ufafanuzi imetolewa na upande wa mkuu wa wilaya ambayo ndio inayodaiwa kutesa watu. Nini maana ya story kuwa balanced?

4/Kama shughuli ilikuwa ni ya kujitolea, kwanini watu wasakwe, warushwe rushwe kichura, wakimbizwe masokoni, Wahukumiwe kwa kwenda kilabuni?

5/Hivi ukaidi ni nini katika tukio hili? Kama suala ni kuombwa kujitolea, na mtu akakataa kujitolea ili aendelee na shughuli zake za kutafuta pesa, kuna kosa gani hapo?
Amesema wanajeshi hawakuwepo ina maana servicemen walikuwa wenyewe? kama wanajeshi walikuwepo basi ndio waliotoa order kwa servicemen kuwaadhibu wananchi na hiyo ni kashfa kwa upande wa jeshi kwa sababu jeshi haliko katika mfumo wa utawala wa kiraia na kama kulihitajika order basi ni kutoka kwa mkuu wa kikosi tu, sasa kama jkt waliombwa kujitolea halafu wakaanza kuwapiga wananchi ni kosa kwa taratibu za jeshi. Huyo mkuu wa wilaya alitakiwa na yeye arushwe kichura chura.
 
Kwanza kabisa kuna tatizo kubwa sana huko kuliko huu uiitao ufafanuzi wako...

Pili, hakuna tatizo kabisa watu kushiriki na kuitekeleza mipango yao ya kujiletea maendeleo....

Lakini hili ni lazima lifanyike kwa utaratibu unaoeleweka na kukubalika na kila mmoja ama ingalau na wengi kabisa.... hapa nina maana ya ushirikishwaji wa wananchi huku kila upande ukiwa unajua majukumu na wajibu wake...

Nina maana kwamba, wananchi hao waliorushwa kichura kichura wajue na watekeleze wajibu wao...

Na wakati huo huo serikali nayo itekeleze jukumu na wajibu wake kikamilifu pasipo kutumia ubabe wa kidola kulazimisha mambo kufanyika ambalo ndilo lililofanyika huko...

SASA BASI:

Umesema vifaa vya ujenzi kama mbao, simenti, misumari nondo na vingine vilikuwepo....

Maswali:

1. Tuambie, nani amevileta hivyo vifaa ? Je, ni serikali ama ni michango ya wananchi wenyewe kwa kulazimishwa na mitulinga ?

2. Mgawanyo wa majukumu ulikuwaje ? Kwa maana wananchi wao wafanye nini na nini ilikuwa wajibu wa serikali kama nilivyoeleza hapo juu ?

3. Je, kulikuwa na mpango shirikishi ulioandaliwa na wananchi wote ama kwa wingi wao wakauridhia ya namna kila mmoja ambavyo angeweza kushiriki zoezi la ujenzi la zahanati ya kijiji ?

Kumbuka kuwa haiwezekani iwapo mafundi toka JKT walikuwepo pamoja na vifaa vyote vya ujenzi halafu wakati huohuo utake wananchi wote wa kijiji chote wawe kwenye site ya ujenzi kana kwamba hawana shughuli zao binafsi za kila siku za kujitafutia maendeleo yao binafsi na mlo wao !!

Kwa ufahamu wangu ni kuwa, kama mafundi walikuwepo pamoja na vifaa vyote, wananchi wangeweza kujigawa wenyewe kimakundi mfano kivitongoji kwa ajili ya kwenda kuwasaidia hao mafundi kusogeza tofali, kuchota maji nk huku wengine wakiendelea na shughuli zao kwa amani wakisubiri zamu yao !!

Hili likifanyika, wala huhitaji polisi wa JWTZ ama Mgambo kuwasimamia wananchi hawa bali wao wenyewe watafanya hivyo pamoja na kuchukuliana hatua wao kwa wao kwa ambao hawatajitokeza !!

Lakini kwa kuwa serikali ya Magufuli ni ubabe tu huku wakiwa hawana akili wala maarifa, mpaka wamalize miaka mitano basi, watakuwa wameipata fresh yao !!

Mwisho kwa maelezo yako tu hayo hapo juu, mtu mwenye akili timamu hata kama hakuwepo huko, akisoma atagundua mara moja kuwa hakukuwa na mpango shirikishi uliowajumuisha wananchi wote ktk kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa zahanati bali viongozi wa eneo husika kwa kuwa tu wanatafuta sifa binafsi na kwa kuwa hawakubaliki na kuaminiwa na wananchi wa eneo husika, wametumia nguvu nyingi kuliko elimu ya ushawishi kwa wananchi ili waone umuhimu wa kujitoa ktk jambo ambalo ni la manufaa kwao wenyewe na watoto wao...!!

Ni wazi kulikuwa na makosa mahali fulani (hasa kwa upande wa serikali/wasimamizi) aidha tuwe tunapenda ama hatupendi kuambiwa hili na ni kwa mantiki hii wananchi waliwakatalia na kuamua kuwalazimisha kwa nguvu za kikoloni !!

Kuwarusha rusha kichura wananchi hao ni ujinga na ni kosa la kipumbavu kwa wote walioshiriki kutenda....ipo siku viongozi wa namna hii, watakuja kuwa - push wananchi to the limit na hapo nao watajibu mapigo!!!
Mkuu wa wilaya hana mamlaka hata ya kuwaamrisha servicemen, swali ni nani aliyetoa amri ya kuwaadhibu wananchi?
 
Wakuu,

Kuna Uzi umepandishwa jukwaani ukiwa na taarifa kwamba Mkuu wa Wilaya ya Nkasi amewaamuru askari kuwaadhibu wananchi.

Ufafanuzi wa taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Jana, Wananchi, Mbunge na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg Said Mtanda walikubaliana kufanya kazi ya kujenga zahanati ya kijiji iliyokwama kwa takriban miaka 5 huku wananchi wakitembea umbali wa Km 20 kufuata huduma za afya.

Wakati huo huo kwenye kijiji cha Ntuchi (siku ya jana Jumamosi) kulikuwa na mnada ukiendelea hivyo baadhi ya vijana walitajwa kwenda kunywa pombe kinyume na makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja (Songambele).

Askari wa JKT ambao ni mafundi walikuja kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo kwakuwa zana zote ( Mbao, bati, misumari) kwa miaka miwili vimekuwa vikioza.

Vijana waliokuwa wamekwenda mnadani walifuatwa wakaletwa ili kushiriki zoezi hilo (songambele).

Askari waliwaleta wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na waliokaidi walirushwa kichura chura!

Wananchi kwa pamoja wamefurahi kwakuwa kazi iliyopangwa imefanyika.

Mpaka kufikia muda huu ( Leo jumapili 13, August) wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kuendelea kushiriki zoezi hill.

Hakuna wanajeshi waliokuja kushiriki Bali ni service men waliojitokeza kujenga zahati kwa kushirikiana na wananchi.

Pia askari hao hao (service men) walishiriki shughuli za maendeleo katika kijiji cha Kasu.

Mtoa taarifa aliyejitanabaisha kama mwanahabari anapaswa kufuata misingi na weledi wa taaluma ya habari.

Ofisi ya mkuu wa wilaya Nkasi imesikitishwa na taarifa zilizotolewa mtandaoni za upotoshwaji!

Yani wamewabembeleza wange wafinya kidogo,
Wakinywa pombe wake zao watembee km 20 kuji fungua.
Mkuu wengine wanatakiwa kuchapwa.
 
Mkuu wa wilaya hana mamlaka hata ya kuwaamrisha servicemen, swali ni nani aliyetoa amri ya kuwaadhibu wananchi?
Usiamini utetezi wa kujikanyakanyaga kama huu Mkuu. Siku hizi imekuwa staili ya utawala wanajeshi kutumika kwenye operesheni za ndani hasa za kutumia nguvu dhidi ya wananchi kwa kisingizio cha maendeleo. Servive men wanatokaje kambini kwa amri ya Mkuu wa wilaya? Na wakitoka wanakuwa peke yao au na wanajeshi (viongozi wao)? Halafu waliokaidi inatolewa adhabu ya kuruka kichura (adhabu ya kijeshi) dhidi ya raia. Ni punguani tu atakayeamini kichura siyo adhabu ni maelekezo ya kufanya Kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Kuna Uzi umepandishwa jukwaani ukiwa na taarifa kwamba Mkuu wa Wilaya ya Nkasi amewaamuru askari kuwaadhibu wananchi.

Ufafanuzi wa taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Jana, Wananchi, Mbunge na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg Said Mtanda walikubaliana kufanya kazi ya kujenga zahanati ya kijiji iliyokwama kwa takriban miaka 5 huku wananchi wakitembea umbali wa Km 20 kufuata huduma za afya.

Wakati huo huo kwenye kijiji cha Ntuchi (siku ya jana Jumamosi) kulikuwa na mnada ukiendelea hivyo baadhi ya vijana walitajwa kwenda kunywa pombe kinyume na makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja (Songambele).

Askari wa JKT ambao ni mafundi walikuja kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo kwakuwa zana zote ( Mbao, bati, misumari) kwa miaka miwili vimekuwa vikioza.

Vijana waliokuwa wamekwenda mnadani walifuatwa wakaletwa ili kushiriki zoezi hilo (songambele).

Askari waliwaleta wananchi ili kufanikisha zoezi hilo na waliokaidi walirushwa kichura chura!

Wananchi kwa pamoja wamefurahi kwakuwa kazi iliyopangwa imefanyika.

Mpaka kufikia muda huu ( Leo jumapili 13, August) wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kuendelea kushiriki zoezi hill.

Hakuna wanajeshi waliokuja kushiriki Bali ni service men waliojitokeza kujenga zahati kwa kushirikiana na wananchi.

Pia askari hao hao (service men) walishiriki shughuli za maendeleo katika kijiji cha Kasu.

Mtoa taarifa aliyejitanabaisha kama mwanahabari anapaswa kufuata misingi na weledi wa taaluma ya habari.

Ofisi ya mkuu wa wilaya Nkasi imesikitishwa na taarifa zilizotolewa mtandaoni za upotoshwaji!
wacha upumbafu wa kuhalisha kisichofaa

mshazoea mateso had mnaona kawaida. sjui mtajiongeza lini!!!

watanzania wana uhaba wa mafanikio kiasi kwamba serkali ikijenga barabara watu wanaona ngekewa wakat ni wajibu wa serkal *by prof kitila mkumbo!!

sasa ni Kipi kinachowanya watu washangilie raia kupigwa?

try me
 
Huyu Said Mtanda ni bure kabisa, ccm ni adui wa haki na maendeleo, zaidi ya nusu karne ya uhuru wetu lakini wananchi wanaishi bila Huduma za afya za kuridhisha afadhali hata kipindi cha mkoloni Huduma za afya zilikuwa bure na za uhakika
 
Sasa wewe mleta ufafanuzi hapa ndio umeharibu kabisa. Yaani una kiri kulikuwa na kulazimishwa na kuteswa kwenda kujenga hicho kituo, lakini ukaharibu kwa kuleta ushabiki wa kumtetea mkuu wa wilaya kishamba. Kwa mfano...

1/Yaani taarifa nzima imejichanganya. Mara vijana wamekwenda kunywa pombe, mara watu wamechukuliwa Gulioni, mara Askari (service men!), Mara hawajapigwa lakini wamerushwa vichura chura nk. Ni mchanganyiko kuliko usahihisho.

2/Mleta ufafanuzi hapa husemi wewe ni nani katika ufafanuzi huu. Wewe ni mkuu wa wilaya hiyo? Wewe ni msemaji wake? Wewe ni shuhuda? Wewe ni mleta mada tu lakini una source?

3/Taarifa hii ya ufafanuzi imetolewa na upande wa mkuu wa wilaya ambayo ndio inayodaiwa kutesa watu. Nini maana ya story kuwa balanced?

4/Kama shughuli ilikuwa ni ya kujitolea, kwanini watu wasakwe, warushwe rushwe kichura, wakimbizwe masokoni, Wahukumiwe kwa kwenda kilabuni?

5/Hivi ukaidi ni nini katika tukio hili? Kama suala ni kuombwa kujitolea, na mtu akakataa kujitolea ili aendelee na shughuli zake za kutafuta pesa, kuna kosa gani hapo?
Ahsante sana mkuu kwa comment yako hii
 
Kunywa Pombe gulioni ndio kutafuta pesa? Unaambiwa watu wamekubaliana kushiriki kutatua kero lakini wengine wanaenda kunywa Pombe kana kwamba hiyo hospitali ikikamilika wao hawataitumia wataendelea kupona kwa Pombe! Wacha warushwe kichura chura hata kukwepa ndege, bila watu kushurutishwa tusingekuwa na reli toka Dar hadi kwetu Kigoma.
 
Back
Top Bottom