Usafiri wa Ungo !

Usafiri wa Ungo !

habari zenu,
natumaini weekend inaenda vyema hapo ulipo....leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari nikaona watu kadhaa wa familia moja wamedondoka na ungo sehemu flani hapa nchini kwetu Tanzania (thread yenye habari zaidi JF hii hapa)...maswali yakaanzia hapo kutoka kwa niliokuwa nao,naomba niwashirikishe ili kama kuna anayefahamu atujulishe.
1.is it scientifically proved kwamba ungo unapaa?....kwanini tusijaribu kufanya utafiti tuhakikishe hii mambo,maana wengine(mimi personally) naona hili swala la kupanda ungo ni mulugo.
2.je hizi ungo zinavyopaa,zina route yake?....kama kulivyo na anga la kimataifa,anga la ndege ndogo etc.
3.je radar inaweza ikaona hizi ungo?
4.ungo unafananaje----kwa mwenye picha tafadhali aweke
5.je zinatumia nishati gani?
6.zipo aina tofauti za ungo?ni ngapi?




wengine mtaanza kuponda hii thread,ila naamini itatusaidia wengine kupata uelewa kuhusu haya mambo yakoje yakoje,na kama ni kweli au stori tu......sisi ni waafrika,na mambo haya yapo kwetu,nitafurahi kujua kiundani kuhusu haya kwa JF.ni haayo tu kwa leo



CC: watu8 , Chimbuvu babaV Nicas Mtei Bujibuji Zinduna Filipo Mtambuzi Mbuzimzee The Boss Puppy @lara1 Preta Erickb52 charminglady Mwali Ndoa

Usafiri huu ni mzuri kweli, hawa wachawi wangekua atleast wanasaidia dunia katika usafiri, coz ingekuwa very cheap kwenda majuu :-D
 
Mmmmh!

Sasa hapo Polisi watawafungulia hawa jamaa jalada kwa kosa gani?
-Rubani kuendesha chombo cha anga bila leseni?
- Chombo cha anga kutua sehemu isioruhusiwa?
- Au wamevunja kifungu gani cha sheria hawa?

Niana shaka sana hawa jamaa walikuwa wamekula kitu cha A town; wakajiona ka wako mawinguni vile!
Chezea MARYJANE bila kula ni noumaa!!!
Kiukweli, hawa jamaa hawana kosa lolote kisheria, japo tunayo sheria ya uchawi ya mwaka 1922, 1928 na marekebisho yake ya mwaka 2002.
 

Attachments

hizi ni story tu, na hazipo Africa tu, hata ulaya zamani kutokana na hadithi kulikuwa na myth kwamba wanasafiri kwa kutumia ufagio, kama vile wasukuma na fisi na wakerewe na mamba..., its just a load of BS

Labda ufafanue. Hao walioonyeshwa kwenye TV wamelipwa?
 
Labda ufafanue. Hao walioonyeshwa kwenye TV wamelipwa?

Mkuu kuna kitu kinaitwa hallucinations.., (na kuna dawa kemikali) ukitumia unahallucinate mfano aina fulani ya uyoga.., sasa basi ukitumia haya madawa hata wewe unaweza kujiona unapaa au unelea au upo mbinguni.., kwahio inawezekana hawa watu wanaodhani wanapaa huwa wanatumia haya madawa wanadhani wanapaa kumbe wanatembea uchi sijawahi kuona mtu anasema kawaona wanapaa wote huwa wanaona wameanguka
 
Inaonesha huyu Zombie hakuona hiyo taarifa ya habari bali amewasikia majirani walioiona hiyo habari ndo akakimbilia ki-mchina kupost ----- hapa. Eti TV fulani, eti watu kadhaa wa familia moja, mara oh sehemu fulani ya Tz! Nyamb...f kwa nini usiulize walioiona hiyo taarifa? Watu wengine bwana mnatia hasira sana!
 
duh,kumbe wavumbuzi tunao humu humu nchini!!!hureeeeeee!!!naja kuwawekea dhamana.
 
Inaonesha huyu Zombie hakuona hiyo taarifa ya habari bali amewasikia majirani walioiona hiyo habari ndo akakimbilia ki-mchina kupost ----- hapa. Eti TV fulani, eti watu kadhaa wa familia moja, mara oh sehemu fulani ya Tz! Nyamb...f kwa nini usiulize walioiona hiyo taarifa? Watu wengine bwana mnatia hasira sana!


mwanga mkubwa we'............. naona umeguswa!😕
 
Watu mnashangaza kweli! Yaani mnashangaa kana kwamba hamjawahi kuisikia hii makitu. Awamu ya kwanza ya Che Nkapa Mh. Dr. Pius Ng'wandu, alikaribishwa na Dr. Matunge kwenda kuzindua usafiri wa Ungo kutoka Dar hadi Mbeya (sijui kwa nini Mbeya? Maana hata hawa wa Sngd walikuwa wanaenda huko). Hii ilishindikana kutokana na masharti yake. Hawa wa Sngd mwenzao aligeuka nyuma ndo wakaanguka, nilicheka sana yule mzoefu alivokuwa anaelezea, eti mwenzetu asiye na uzofu ndiye aliyetu-cost tukadondoka!
 
Sasa kama mambo ni hayo mbona pesa za walipa kodi zinaishia kwenye piga la dhaifu kila siku? Si wamtafutie huko kaungo kake kagodo hizo pesa ziwalipie watoto wetu shule na kuwatibu wazee wetu wanaofia huko mahospitalini kwa kukosa dawa?
 
Mkuu the Boss, its the other way round, tuko more developed kuliko wazungu!.

Hata mimi hao jamaa nimewaona, mwanzo nilidhani wasafiri wote wa ungo, huvalia birthday suit zao, kuna wanaweza kusafiri na nguo zao!. Pia nidhani husafiri one on one, kumbe wanaweza kusafiri watu watatu?.

Hao wanahitaji kufanyiwa research ili usafiri huo utumike kitaifa zaidi!.

Kwa msio fahamu, hiyo ni "works of super natural power" kwa kutumia power ziitwazo "PSI". Kila binadamu anazaliwa na hizi powers ila wengi zaidi zina fall out kadri wanavyokuwa. Sasa wengine ziko more dorminant kuliko wengine. Wale ambao ni more dorminant wakishajijua kwa vijijini huitwa waganga, wanga na wachawi, kwa mjini hujiita mitume, manabii na wachungaji au waponyaji kimiujiza!.

Powers hizi zina brances nyingi, miongoni mwake ni "telekinesis", "telepathy", "pre cognition", "pre amonition", " "levitations", "telepotation", "metal benders", "clayvoyance", "deja vu"etc, stc.

Kuna Myahudi "Uri Geller", yeye baada ya kuwa na uwezo wa kupinda vyuma, alianza kurajirika kwa kuonyesha mazingaombwe tuu ya kupinda vyuma hadi alialikwa royal wedding ya Prince Charles na Lady Di, na akavipinda seti ya vijiko vya dhahabu walivyo zawadiwa maharusi.

Kampuni fulani ya mafuta ikamfanyia reseach kufanya "oil dowsing", jamaa anapewa ramani, anapepesa tuu mkono juu ya ramani kujua eneo lenye mafuta!. Baada ya hapo anapandishwa helcopter to trace the real location, jamaa analocate mpaka exact position, jamaa wakijimba wanakuta mafuta. Tangu hapo sasa jamaa huyo ni tajiri mkubwa sana with shares kwenye makampuni makubwa ya mafuta!.

Kwa jinsi nilivyowaona wakihojiwa, wamesema kila kila kitu, ila usiku wa leo, huyo mwenye chombo cha usafiri, atawaibukia na kesho watakuwa wamesahau kila kitu ili wasimuonyeshe huyo mganga alipo. Kesho wataonekana kama mataahira fulani. Hii ni sayansi ya kiafrika, tukiiendeleza, unaweza kukuta hata kuyasafirisha mafuta au gesi kuja jiji, wala hakuhitaji bomba!.

Lets be open minded kukubali black magic ipo, lets put it to a good use!.
Pasco.

hapo kwenye red,bonge la pointi.......kwanini tusiwatafuta hawa tuwafanyie utafiti....nashauri iitwe TaSuWiRi(Tanzania Supernatural Witchcraft Research Institute)....makao makuu yawe hukohuko tabora,au nyanda za juu kusini...tunaweza tukawa mabilionea eti.
 
ninavideo ya jamaa wa kigoma walikamatwa mwanza, sijui namna y kuapload
 
wapi huko??
Tukio hili lilitokea huko Manyoni. Wahusika walikuwa wanatoka sehemu moja iitwayo Mkwese. Jamaa hao 3 walikuwa wanakwenda Mbeya, kuhudhuria mazishi ya mama yao mzazi. Sabubu kubwa iliyowafanya waanguke hapo Manyoni ni mmoja wao ambaye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupaa na ungo kugeuka nyuma wakati chombo kikiwa angani. Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 ya usiku wa kuamkia jana.
Habari hii ilirushwa kupitia kituo cha ITV.
 
Back
Top Bottom