BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,213
- 4,165
Ni kweli mkuu mambo mengi hatuyafahamu lakini hata kama sijaona siwezi kukubali kwamba maji yanaweza kupanda mlima vile vile siwezi kukubali kwamba kuna chombo cha kawaida tu kwa kutumia mizizi kina-defy gravity..
Ndio maana nikafanya uchunguzi mdogo tu, nikaona kwamba sio Bongo tu, hata huko kwa hao wazungu kuna watu walisadikika kwamba wanapaa kwa kutumia mifagio au magic carpets (na kumbe wengi ya hawa wachawi walikuwa katika kutumia madawa yao kuna dawa mtu ukitumia una-hallucinate.., kwahio hawa jamaa wakadhani wanapaa kumbe wala..)
Kwenye issue ya alleviation aliyoitoa Pasco, nikacheki pia nikamuonyesha kwamba that is a known trick na ukigoogle online unaweza na wewe ukajifunza (its just magic tricks).., kuhusu kupinda vyuma na kina Uri Geller pia nikamuonyesha kwamba its just magic tricks..
Tutakuwa tumewakosea sasa wazazi na ndugu zetu waliotupeleka shule kama tutaamini mambo tu kwa majibu mepesi ya (black magic) bila kujiuliza hii kitu inafanywaje.., kwahio mkuu kama mtu anapaa na ungo basi huo sio ungo bali labda ni balloon lenye gas kama helium au hydrogen ambayo ni nyepesi kuliko oxygen..
Sio kwamba tunabisha bure bali tunakaa kukubali mambo ambayo ni impossible mpaka pale tutakapo-prove otherwise..
"When your remove all the impossibles, whatever remains however improbable its the answer.." kwahio ukimuona magician anafanya kitu ambacho hakiwezekani fahamu kwamba ni illusion
...Mkuu Sun Wu, kimsingi ninakubaliana nawe.
Lakini, pamoja na kuwa elimu tunayo pata inatuaminisha kutoamini jambo hadi liwe limedhibitishwa Kisayansi(na Wazungu?), bado ninaamini pia kwamba sisi kama waafrika tunapaswa kuweka pia issue kama ya 'kuruka na ungo the benefit of doubt.
Tunapaswa kujiuliza;What if it is really Possible?
What if mababu wa mababu zetu walikuwa wamegundua 'Sayansi' ya Kiafrika ya kuuwezesha Ungo kuruka hewani lakini kutokana kutojua kwako kuandika, kusoma na kuweka kumbukumbu, 'sayansi' hiyo ikaishia kurithishwa kizazi na kizazi kwa mdomo tu na ikafika mahali wale waliokuwa wakiifahamu kweli wakatoweka?
Unasema kwamba huamini kitu bila kushuhudia mwenyewe kwa macho? Samahani, nachepukia kidini kidogo ili kuipa hoja yangu uzitona Samahani sana kwa wote watakaokwazika. Si nia yangu kuwakwaza maana mimi mweyewe ni Mkristo.
Mkuu Sun Wu, Unaamini kwamba bahari inaweza kugawanyika pande mbili kwa mtu kuinyooshea kidole? Hukuiona, Unaaminije kuwa ni kweli? (hii ni kama wewe ni mkristo)
Najua jibu la haraka linaweza kuwa hayo ni mambo ya imani. Good. sasa kama unaweza kuwa na imani kuwa bahari inaweza kutenganishwa katikatiwhy not also Ungo kupaa kwa Sayansi ambayo bado ipo juu ya ufahamu wetu wa kawaida??
Unaamini kwamba watu walifika mwezini mwaka 1969? unaaminije? ulishuhudia?
Kwa Tv? Picha?
Unaamini kwamba kuna UFO, Unidentified Flying Objects, vyombo vya anga vinavyosadikiwa kutoka anga za mbali kuja kuvinjari anga la dunia?
Kama unaamini, umevishuhudia kwa macho yako mwenyewe?
Kama huamini, kwa nini wakati hii inaendana na Sayansi inayokuzuia kuamini kuwa ungo unaweza kuruka kwa maana ya kwamba kama vipo kweli, bado hakuna ajuaye vinatumia nini kutoka huko vinakotoka hadi kufika anga letu?
Umetumia sana google ku-crash hoja ya watu wa aina ya Uli Gerrer kuwa na. uwezo wa kupindisha kijiko.
Je tuamini kwamba kweli duniani hakuna watu wa aina hiyo na kwamba wote wanaofanya hivyo ni tricks tu?
Nilisoma mahali kwamba huyu bwana alipatwa hata kualikwa kwenye jumba kuu la Malikia wa Uingereza kwa ajili ya kuuenzi uwezo wake huo.
Je walifanya hivyo kuuenzi uwezo wake wa kufanya magic tricks ya kupindisha vijiko na uma ama walifanya hivyo kwa kuuenzi uwezo wa ziada alio nao wa kuweza kufanya yale yaliyo juu ya uwezo wa kawaida wa binadamu?
Nimependa hayo maneno yako niliyo-bold.Naamini pia kuwa Waliotusomesha walifanya hivyo ili kutupa uwezo wa kuchanganua mambo. Hatupaswi kuhukumu moja kwa moja kwamba HAIWEZEKANI mtu kuruka kwa Ungo.
What if it is really Possible????